Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development

Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development Site for Ministry Of Lands, Housing and Human Settlement Development Contact Centre for sharing information with Customers.

Customers will share documents with the Ministry through this site

29/08/2026
WANANCHI WATAKIWA KUTHAMINI UTAMADUNI KWA KUIMARISHA UMOJA NA UZALENDOMOROGOROWananchi wametakiwa kuthamini na kuendelez...
27/08/2026

WANANCHI WATAKIWA KUTHAMINI UTAMADUNI KWA KUIMARISHA UMOJA NA UZALENDO

MOROGORO

Wananchi wametakiwa kuthamini na kuendeleza utamaduni wao kwa kuwa ni msingi wa kuwaunganisha Watanzania, kuimarisha umoja na kujenga uzalendo kwa nchi yao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Adam Malima, wakati akizindua Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Mkoani Morogoro.

Mheshimiwa Malima amesema tamasha hilo linawakutanisha Watanzania kutoka makabila mbalimbali, hivyo ni fursa muhimu ya kuendeleza umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa.

Amesema Watanzania wanapothamini na kuhifadhi tamaduni zao, wanachangia kujenga taifa lenye umoja na wananchi wenye uzalendo.

Katika tamasha hilo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeshiriki kikamilifu kwa kutoa elimu kuhusu huduma za ardhi, huku wananchi wakipata fursa ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo kupokea hati zao za umiliki wa ardhi.

Tamasha hilo linaendelea katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, likilenga kuenzi, kukuza na kuendeleza utamaduni wa Tanzania na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 29 Agosti 2026.

27/08/2026

JAMII YAHIMIZWA KUKOMESHA TAMADUNI KANDAMIZI WANAWAKE KUMILIKI ARDHI

Jamii imetakiwa kuachana na tamaduni kandamizi zinazowazuia wanawake kumiliki ardhi, na badala yake kuhakikisha wanawake wanapata haki sawa ya kumiliki na kutumia ardhi kwa maendeleo yao na familia zao.

Wito huo umetolewa na Bw. Canon Peter Pangapanga, mkazi wa Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro, tarehe 27 Agosti 2026, baada ya kukabidhiwa Hati ya Umiliki wa Ardhi katika Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, lililopo Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

"Twendeni pamoja kuachana na tamaduni zinazowakandamiza wanawake. Mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi na kutumia ardhi kwa maendeleo yake na familia yake.” amesema

Kwa mujibu wa Bw. Pangapanga, Tamasha la 4 la Utamaduni linalofanyika mkoani Morogoro ni fursa muhimu kwa wananchi kupata elimu na huduma za ardhi, hivyo amewahimiza wananchi, hususan wanawake, kutumia fursa hiyo kujipatia Hati za Umiliki wa Ardhi na kulinda haki zao.

27/08/2026

KAULI YA WAZIRI WA ARDHI KUHUSIANA NA MALALAMIKO YA BAADHI YA WANANCHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI

27/08/2026

Hati Miliki, Furaha ya Wananchi Morogoro

Wananchi mkoani Morogoro tarehe 27 Agosti 2027 wameeleza furaha na kuridhishwa kwao na huduma zinazotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi baada ya kupatiwa Hati Miliki za Ardhi kupitia Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi lililopo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Huduma hiyo imetolewa sambamba na Tamasha la Nne la Utamaduni, linaloendelea mkoani Morogoro, likiwa na Kauli Mbiu: “Utamaduni Wetu, Nguzo ya Maadili, Uchumi Jumuishi na Utaifa – Karibu AFCON 2027.”

DKT. AKWILAPO ATOLEA UFAFANUZI MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHIDodomaWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo...
27/08/2026

DKT. AKWILAPO ATOLEA UFAFANUZI MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI

Dodoma

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, ametolea ufafanuzi malalamiko yanayohusu migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, huku akisisitiza wananchi kuzingatia sheria na taratibu za umiliki na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro na hasara zinazoweza kujitokeza.

Mhe. Dkt. Akwilapo amesema hayo Agosti 26, 2026, ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, alipokutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi kuhusu kuvunjiwa maendelezo waliyoyafanya kwenye maeneo mbalimbali nchini. Aidha, kumekuwa na malalamiko mengine yanayohusu matumizi na umiliki wa baadhi ya maeneo ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt. Akwilapo, ufuatiliaji wa karibu uliofanywa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi umebaini kuwa baadhi ya wananchi wanaowasilisha malalamiko hayo hawatoi taarifa sahihi kuhusu uhalisia wa masuala yao, huku wengine wakitumia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kutafuta huruma ya jamii.

Akitoa mifano ya baadhi ya matukio hayo, Mhe. Dkt. Akwilapo ametaja tukio la Agosti 18, 2026, linalomhusisha Bi. Rahel Suda dhidi ya Bi. Adelaida Mkoko kuhusu umiliki wa Kiwanja Na. 42, Kitalu B, kilichopo Kikuyu Extension jijini Dodoma, ambapo Wizara tayari imeshatoa ufafanuzi kuhusu suala hilo baada ya kupata maelezo ya kina.

“Maeneo mengine yenye malalamiko ni yale yanayohusu utekelezaji wa hatua za mamlaka zenye wajibu wa kisheria wa kusimamia hifadhi za umeme au reli katika maeneo ya Tegeta kwa Ndevu, Mavurunza na Kilungule, mkoani Dar es Salaam,” amesema Mhe. Dkt. Akwilapo.

Ameongeza kuwa Wizara inatambua umuhimu wa mitandao ya kijamii katika kufikisha taarifa na malalamiko ya wananchi serikalini, lakini akabainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia kutoa taarifa zisizo sahihi, licha ya kufahamu kuwa masuala yao tayari yameshughulikiwa kwa kuzingatia maamuzi ya mahakama au hatua za kisheria zilizochukuliwa na Serikali.

“Napenda kutoa rai kwa wananchi kuzingatia taratibu za kisheria katika kupata ardhi na kufanya ujenzi mijini na vijijini ili kuepuka kupata hasara kutokana na kubomolewa kwa mae

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba...
27/08/2026

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Kaspar Mmuya, kabla ya kuanza kwa Kikao cha Pili cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 13, leo tarehe 27 Agosti 2026, Bungeni jijini Dodoma.

Viongozi wa Vijiji vya Matongo na Nyangoto pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, wakiwa uwandan...
27/08/2026

Viongozi wa Vijiji vya Matongo na Nyangoto pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, wakiwa uwandani pamoja na wadau wa Mgodi wa North Mara, wakikagua na kubainisha maeneo yanayotarajiwa kuguswa na upanuzi wa shughuli za mgodi.

Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya zoezi la uthamini wa fidia na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu mchakato huo, unaotekelezwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

WANANCHI MATONGO NA NYANGOTO KUELIKIMISHWA KUHUSU UTHAMINI WA FIDIA NORTH MARANYAMONGO, MARAWizara ya Ardhi, Nyumba na M...
27/08/2026

WANANCHI MATONGO NA NYANGOTO KUELIKIMISHWA KUHUSU UTHAMINI WA FIDIA NORTH MARA

NYAMONGO, MARA

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupitia wataalamu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, imefanya kikao na Kampuni ya Barrick North Mara Gold Mine pamoja na viongozi wa Vijiji vya Matongo na Nyangoto, kwa lengo la kujadili maandalizi ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu zoezi la uthamini wa fidia linalohusishwa na upanuzi wa shughuli za Mgodi wa North Mara.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Diwani wa Kata ya Matongo, Mhe. Godfrey Mwita, amewataka viongozi wa Vijiji vya Matongo na Nyangoto kushirikiana kwa karibu na wataalamu pamoja na wadau wote wanaohusika katika mchakato huo, akieleza kuwa wananchi wa maeneo hayo wanatarajiwa kuguswa na upanuzi wa shughuli za mgodi.

Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano wa Kampuni ya Barrick, Bw. Francis Uhadi, amesema kampuni hiyo iko tayari kuanza mchakato huo kwa haraka, huku akisisitiza dhamira ya kampuni kuhakikisha haki na maslahi ya wananchi yanazingatiwa na kulindwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Akifafanua hatua zinazofuata, Mthamini Kiongozi kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, FRV. Baraka D. Mollel, amesema kikao hicho ni sehemu ya hatua muhimu kuelekea kuanza mchakato wa uthamini, baada ya hatua za awali zilizofanyika kwa kushirikisha Wizara ya Madini, ikiwemo tafiti na maandalizi mbalimbali.

Amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha zoezi la uthamini linafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, pamoja na kuwezesha wananchi kupata taarifa sahihi kuhusu mchakato huo.

Naye Mtunzaji wa Bwawa la Mgodi, Bw. Majuto Kipande, ameeleza kuwa, tafiti za awali zilizofanyika wakati wa uanzishwaji wa mgodi zilionesha kuwa shughuli za uzalishaji zingefikia ukomo mwaka 2027. Hata hivyo, amesema tafiti zinazoendelea hivi sasa zinaonesha uwezekano wa uzalishaji kuendelea hadi kati ya mwaka 2031 na 2040.

Kwa mujibu wa Kipande, hali hiyo imeongeza umuhimu wa upanuzi wa bwawa la kutunza mabaki ya uchenjuaji wa dhahabu kutokana na bwawa linalotumika sasa kutaraji kufikia ukomo wa matumizi mwaka 2031.

Ameongeza kuwa, ujenzi wa bwawa jipya la kutunza mabaki ya uchenjuaji wa dhahabu

WANANCHI WAPONGEZA HUDUMA ZA ARDHI KATIKA TAMASHA LA UTAMADUNIMOROGOROWananchi wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya A...
26/08/2026

WANANCHI WAPONGEZA HUDUMA ZA ARDHI KATIKA TAMASHA LA UTAMADUNI

MOROGORO

Wananchi wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushiriki katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, wakisema ushiriki huo umewawezesha kupata elimu na huduma za ardhi kwa urahisi.

Pongezi hizo zimetolewa na Bw. Kanoni Charles Pita Pangapanga, mkazi wa Manispaa ya Morogoro, baada ya kupokea hati yake katika banda la Wizara ya Ardhi lililopo katika uwanja huo.

Amesema anaiishukuru Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha huduma za ardhi, akibainisha kuwa wananchi sasa wanapata huduma kwa ufanisi na hati za miliki kutolewa kwa muda mfupi.

Aidha, amesema uwepo wa wataalamu wa ardhi katika tamasha hilo umewarahisishia wananchi kupata majibu ya changamoto zao, pamoja na kuelewa taratibu sahihi za umiliki na matumizi ya ardhi.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutumia matamasha na maonesho mbalimbali kusogeza huduma karibu na wananchi, kutoa elimu kuhusu masuala ya ardhi na kuwasaidia kupata huduma moja kwa moja.

Tamasha hilo lilizinduliwa tarehe 26 Agosti 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Adamu Malima, ambaye aliwataka Watanzania kuthamini, kulinda na kuendeleza utamaduni wao kwa kuwa ni msingi wa kujenga umoja, uzalendo na mshikamano wa kitaifa.

Amesema tamasha hilo pia ni fursa ya kuendeleza na kuhifadhi utamaduni wa Tanzania, huku Serikali ikiendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.

Address

2908
Dodoma
255

Opening Hours

Monday 00:00 - 23:45
Tuesday 00:00 - 23:45
Wednesday 00:00 - 23:45
Thursday 00:00 - 23:45
Friday 00:00 - 23:45
Saturday 00:00 - 23:45
Sunday 00:00 - 23:45

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development:

Shortcuts

Share