Maendeleo ya Jamii

Maendeleo ya Jamii Ukurasa rasmi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum
(1)

*SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUWATUMIA WATOTO KATIKA SHEREHE NA BURUDANI ZINAZOCHOCHEA MMOMONYOKO WA MAADILI*Na WWMJJWM, Do...
16/08/2026

*SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUWATUMIA WATOTO KATIKA SHEREHE NA BURUDANI ZINAZOCHOCHEA MMOMONYOKO WA MAADILI*

Na WWMJJWM, Dodoma, Agosti 16, 2026

Serikali, kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imepiga marufuku matumizi ya watoto, hususan watoto wa kiume, katika sherehe na burudani zinazochochea vitendo vya mmomonyoko wa maadili na kwenda kinyume na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka waandaaji wa sherehe na burudani za aina hiyo kujisalimisha katika kituo cha Polisi kilicho karibu nao ifikapo Agosti 19, 2026, akieleza kuwa endapo hawatafanya hivyo, atamwomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwezesha Jeshi la Polisi kufanya msako mahsusi kwa kushirikiana na jamii, ili kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Waziri Gwajima amewataka Maafisa Utamaduni pamoja na Watendaji wa Serikali za Mitaa na Vijiji kuongeza umakini katika uchambuzi wa maombi ya vibali vya sherehe na burudani, ili kubaini mapema viashiria vya shughuli zinazoweza kukiuka maadili na kutupilia mbali maombi yenye mashaka. Amesema hatua hiyo ihusishe pia sherehe zinazowahusisha watoto katika maonesho yasiyofaa, pamoja na michezo ya kuvua nguo hadharani, huku akisisitiza kuwa ukiukwaji utakapothibitika, hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.

Waziri Gwajima amewataka wananchi wenye mapenzi mema kutoa taarifa wanapobaini uwepo wa sherehe au burudani za aina hiyo, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda maadili ya jamii na kunusuru vizazi si la Serikali pekee, bali linaanzia kwa kila mwananchi katika malezi na makuzi ya watoto. Aidha, amewataka wananchi kukataa kutoa michango, hamasa au kuwa wafuasi wa vitendo hivyo mitandaoni, pamoja na kutojihusisha na sherehe zinazochochea mmomonyoko wa maadili katika jamii na Taifa kwa ujumla.

MAHUNDI AWASHTUA VIJANA IWAMBI KUTUMIA MICHEZO KUPATA AJIRA, KUJENGA IWAMBI BILA UHALIFUNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jam...
16/08/2026

MAHUNDI AWASHTUA VIJANA IWAMBI KUTUMIA MICHEZO KUPATA AJIRA, KUJENGA IWAMBI BILA UHALIFU

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka amewataka vijana kutumia michezo k**a fursa ya kujipatia ajira na kujenga maisha yao, huku wakiepuka vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na ukatili wa kijinsia.

Naibu Waziri Mahundi ameyasema hayo wakayi akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu 13 za Kata ya Iwambi jijini Mbeya.

Amesema michezo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuwaweka vijana pamoja, kuwajengea vipaji na kuimarisha amani na mshik**ano katika jamii huku akiwataka wananchi wa Iwambi kuunda timu moja imara itakayowakilisha kata hiyo katika mashindano mbalimbali na kuitangaza Iwambi kupitia michezo.

Aidha, amependekeza kuanzishwa kwa klabu ya mbio za pole (jogging) katika kata hiyo, akisema mazoezi ni muhimu katika kuimarisha afya na kusaidia jamii kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwani michezo inapaswa kuwa chombo cha kuimarisha upendo na mshik**ano ndani na nje ya Kata ya Iwambi, huku akitoa wito wa kushirikiana katika mapambano dhidi ya uhalifu.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Iwambi, Groria Ipopo Mwamajemba (Mchina), amemshukuru Mahundi kwa msaada huo, akisema amekuwa sehemu ya wakazi wa Iwambi na ameendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kata hiyo.

Mwamajemba amesema kupitia michezo, vitendo vya uhalifu vimepungua kwa kiasi kikubwa katika Kata ya Iwambi, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika michezo kwa vijana.

Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF), amekabidhi jozi mbili za vifaa vya michezo kwa kila timu pamoja na mpira mmoja kwa kila timu, katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Sekondari Iwambi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Diwani wa Kata ya Iwambi, Groria Ipopo Mwamajemba maarufu k**a Mchina, aliyeanzisha mashindano ya mpira wa miguu yaliyowakutanisha vijana kutoka mitaa mbalimbali ya kata hiyo

TAARIFA KWA UMMA📌
16/08/2026

TAARIFA KWA UMMA📌

WAZIRI DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JESHI LA POLISI  KUCHUNGUZA MATAMKO YA NABII TITOWaziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,...
15/08/2026

WAZIRI DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JESHI LA POLISI KUCHUNGUZA MATAMKO YA NABII TITO

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa matamko yanayodaiwa kutolewa na Tito Onesmo Machibya maarufu kwa jina la Nabii Tito.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito huo kupitia ukurasa wake wa Instagram Agosti 14, 2026, mara baada ya kupokea jumbe mbalimbali kutoka kwa wananchi waliomtaka kutoa msimamo na kuchukua hatua kuhusu matamko yanayodaiwa kutolewa na Nabii Tito dhidi ya viongozi wakuu wa nchi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara nchini, ambazo zimeibua mjadala miongoni mwa wananchi kutokana na lugha inayodaiwa kutokuwa na staha na isiyoendana na maadili ya Kitanzania.

Waziri Dkt. Gwajima amewataka wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii, kuendelea kutumia majukwaa hayo kwa kuheshimu utu wa wengine na kuepuka kusambaza maudhui yanayokwenda kinyume na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania au yanayoweza kuvuruga amani na mshik**ano katika jamii. Amesisitiza umuhimu wa kujenga jamii inayozingatia heshima, maadili na matumizi sahihi ya uhuru wa kutoa maoni.

MWISHO

Tunajivunia  kushiriki katika kuendeleza huduma za kidijitali nchini. 11 August 2026  tumekabidhi vishikwambi (tablets) ...
12/08/2026

Tunajivunia kushiriki katika kuendeleza huduma za kidijitali nchini. 11 August 2026 tumekabidhi vishikwambi (tablets) 400 kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ikiwa ni sehemu ya kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Tunaamini teknolojia ni chachu ya maendeleo, uwazi na ufanisi katika taasisi za umma.

* *Agosti 11, 2026 – DodomaKatibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,  Eliakim Cha...
12/08/2026

* *

Agosti 11, 2026 – Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eliakim Chacha Maswi, akipokea vishikwambi 400 kutoka Shirika la Dynatech Solutions kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kidijitali.

Akipokea Vishkwambi hivyo Maswi amelishukuru Shirika la Dynatech kwa kushirikiana na Serikali katika kuimarisha huduma za Ustawi wa Jamii kupitia teknolojia, kwani matumizi ya vishkwambi yanaendana na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inaweka mkazo katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika kuchochea maendeleo ya Taifa na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa vishkwambi hivyo vitasaidia watendaji wa ustawi wa jamii katika ukusanyaji wa taarifa, ufuatiliaji na utoaji wa huduma kwa wakati kwa kuzingatia takwimu.

12/08/2026
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Victor Nkya aki...
11/08/2026

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Victor Nkya akizungumza na Maafisa Viungo wa Ufuatiliaji na Tathmini wakati wa kikao kazi cha kuandaa viashiria vya upimaji wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka wa fedha 2026/2027 - 2030/31

Kikao kazi hicho cha siku tatu kinafanyika kuanzia Agosti 11 - 13, 2026 katika ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma.

08/08/2026

. Kuchukua na kusambaza picha mnato na Mjongeo za Watoto walio katika makao ni katazo la kisheria. Fahamu zaidi kutoka kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii sehemu ya Watoto, Happy Msimbe.

 Kamishna kutoka Jeshi la Uhamiaji Tanzania Divisheni ya Mafunzo Amiru Salim ametembelea banda la Wizara ya Maendeleo ya...
08/08/2026



Kamishna kutoka Jeshi la Uhamiaji Tanzania Divisheni ya Mafunzo Amiru Salim ametembelea banda la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika maonesho ya Sikukuu ya Wakulima ( nane nane) leo tarehe 8 Agosti, 2026 jijini Dodoma.

Kamishna Amiru ameeleza kufurahishwa na mfumo wa usajili wafanyabiashara ndogo ndogo na kupongeza juhudi hizo za kuwawezesha kukuza mtaji wake ili kufikia hatua ya kuchangia mapato ya nchi kwa kulipa kodi.

Address

573
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maendeleo ya Jamii posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Maendeleo ya Jamii:

Shortcuts

Share