Gerson Msigwa

Gerson Msigwa The Permanent Secretary of Information, Arts and Sports & Chief Government Spokesperson|Former DPC.
(1)

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMERIDHIA KUJIUZULU KWA MAKAMU WA RAIS.
25/08/2026

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMERIDHIA KUJIUZULU KWA MAKAMU WA RAIS.

25/08/2026

Mrembo wetu Latricia Ian anaitangaza vyema bendera ya Tanzania huko Vietnam kuelekea fainali za urimbwende Duniani (Miss World 2026) tarehe 5 Septemba, 2026.

Uweze mkubwa wa Latricia hasa anapoelezea jambo ni kivutio kikubwa kwa wote wanaofuatilia mashindano haya Duniani kote na hii ni fursa muhimu na adhimu inayoitangaza nchi yetu Tanzania katika Dunia.

Kila la kheri
Asante na
Asanteni kwa kutupa jukwaa hili sisi Watanzania.

Mwakani 2027 Dunia yote atatupa macho yake Tanzania, tutakapokuwa wenyeji wa Miss World kwa mara ya kwanza katika historia.

Asante Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha tunapata na tunaitumia fursa hii muhimu.

WATANZANIA TUJIPANGE SASA KUKAMATA FURSA, TUPUNGUZE MANENO, VITENDO VIZUNGUMZE ZAIDI. HUKU AFCON, HUKU MISS WORLD.

23/08/2026

TUPO VIZURI.

Wanaopinga mazuri ya Tanzania, KILA MMOJA ATACHANGANYIKIWA KWA WAKATI WAKE.

23/08/2026

SIKU TANO ZA MOTO MOROGORO.
//
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema kuwa, Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika kila mwaka lina lenga kufungamanisha Uchumi, Utalii na Urithi wa Tanzania pamoja na kuusherehekea.

Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 23, 2026 katika ya Kambi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini iliyopo eneo la Mazimbu, Mkoani Morogoro, kuhusu Tamasha la 4 la Kitaifa la Utamaduni linaloanza tarehe 25 hadi 29 katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani hapo.

Amesema Tamasha hilo litakua na matukio mbalimbali ikiwemo mdahalo wa maadili na kuwaomba watanzania kujitokeza kujadili namna ya kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili. Akiongeza kuwa kurakua na Mbio ( Jogging), Michezo ya asili k**a vile karata, bao na drafti, mashindano ya ngoma, muziki na maonesho ya vyakula.

"Watanzania tulinde tamaduni ikiwemo mavazi, ngoma na vyakula vyetu vya asili pia tuendelee kujenga Utanzania wenye Umoja na mshik**ano" amesema Msigwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watanzania wa mkoa wa Morogoro na mikoa jirani kushiriki Tamasha hilo ili kusherehekea Utamaduni na kuweza kuurithisha kizazi cha sasa na baadae.Akiongeza kuwa washiriki tayari wameanza kuingia mkoani hapo kusherehekea mila na deaturi za kitanzania.

22/08/2026

Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe.

Moja ya mazao ya viongozi wa kisiasa anayetambua mipaka ya siasa na utaifa. Mwalimu wa wanasiasa wengine wenye mlengo wa upinzani na anayetambua wakati gani wa kutokukubaliana na wakati gani kukubaliana. Mtu aliyejaa busara, nidhamu, ustahimilivu na akili nyingi.

Halafu Mwana saaaana na yuko mbele ya muda kinyama.

Ishi sana Kaka Freeman Mbowe. Nimefurahi kukuona leo ukihudhuria sherehe za nchi yetu kuandika historia muhimu ya kimageuzi ambayo ni uzinduzi wa mradi mkubwa wa shilingi Trilioni 7.45 wa uzalishalishaji wa megawati 2,115 za umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere licha ya majukumu yako makubwa ya kibiashara.

22/08/2026

Ndoto, Uamuzi Mgumu, Utekelezaji, Ustahimilivu na hatimaye jahazi SALAMA SALMINI.

Asante Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na watangulizi wako wote kwa kuifanikisha ndoto iliyodumu zaidi ya nusu karne.

Ni rasmi mradi wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme wa Watanzania umekamilika na upo kuiinua Tanzania na kuwainua Watanzania.

21/08/2026

Leo ni siku ya kihistoria kwa nchi yetu Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atazindua mradi mkubwa wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere lililopo katika Mto Rufiji, mradi ambao utaingiza katika gridi ya Taifa Megawati 2,115 za umeme baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa takribani shilingi Trilioni 7.4.

Mengi tutayasikia wakati wa sherehe za uzinduzi lakini ni muhimu kukumbushana kuwa mafanikio ya mradi huu ni jambo la kujivunia sana kwa Watanzania kwa kuwa kwa miaka nenda rudi iliaminika kuwa ni mradi usiowezekana.

Sisi Wakinga tuna msemo usemayo “The Sky is a limit”

Mzee NONGWA na wahubiri wengine wa kila kitu Tanzania ni kibaya karibuni katika uzinduzi wa mradi wa Bwawa la Nyerere, ukishindwa kuja fuatilia kupitia runinga, au hapo nyumbani mwako washa taa ya umeme uliozalishwa Bwawa la Nyerere na furahia matunda ya uhuru.

TUMEWEZA

20/08/2026


Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam umezaa matunda makubwa ya kimageuzi katika matibabu ya kibingwa ya ugonjwa huo kwa wananchi sio tu wa Tanzania bali pia nchi jirani.

Tumenufaika kwa mawili, matibabu kwa Watanzania na utalii wa tiba.

MSIKILIZE Dkt. Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road akieleza mageuzi haya makubwa.

Kudos
Asante Mheshimiwa Rais Dkt. kwa dhamira ya dhati na ya vitendo ya kuimarisha matibabu ya kibingwa hapa nchini.

18/08/2026

Huu hapa mradi mkubwa wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma, na kutoka Chalinze kwenda Dar es Salaam.

Msikilize Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akieleza namba mradi huu utakavyoleta uhakika wa upatikanaji wa umeme nchini.

Address

Kisasa
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gerson Msigwa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Gerson Msigwa:

Shortcuts

Share