24/10/2013
Mwalimu Nyerere na Mshahara wa Viongozi wetu:
Kutoka ktk TANU NA RAIA, April 1962, Ukurasa wa 6-7 nanukuu:
"Tulipopunguza mishahara ya Mawaziri (ambao pia ni Wabunge), tulisifiwa kwamba tumefanya jambo zuri. Na kweli tulifanya jambo zuri. Mshahara wa waziri wa kikoloni ulikuwa zaidi ya Shs.5,000 kwa mwezi, sisi tulipunguza ukawa Shs.3,000 ambao ktk sehemu nyingize za Afrika au dunia ni mshahara mdogo sana. Lakini kulinganisha mshahara wa Mawaziri wetu na mishahara ya mawaziri wa nchi nyingine, ambayo yaweza ikawa tajiri zaidi kuliko Tanganyika (Tanzania), siyo njia safi ya kulinganisha. Njia inayofaa kutumiwa, njia ambayo wana-TANU na wananchi wote hatuna budi tuitumie, ni kulinganisha mshahara huo na pato la ndugu zetu(wananchi wa kawaida). Basi njia safi ya kujua k**a mshahara wa Sh.3,000 kwa mwezi ni mkubwa au mdogo si ile ya kuulinganisha na mishahara ambayo Mawaziri (wakiwemo na Wabunge) wa nchi nyingine hupokea. Njia bora ni kulinganisha Sh.3,000 (iliyokuwa ikipokelewa na Mawaziri) kwa mwezi na Sh.75/50 au Shs.132 kwa mwezi (iliyokuwa ikipokelewa na Watumishi wa kawaida wakati huo). Hakuna mtu anayeridhika na fedha. Kwa hiyo Mawaziri (na wabunge) wetu wanazo shida kubwa, na tunazijua. Lakini shida zao ni za aina mbali kabisa na shida ya mtu ambaye anapata Shs.71/50 kwa mwezi!". Mwisho wa kunukuu.
Nadhani bado hoja hii ina mashiko kwa Tanzania yetu ya sasa!