Ofisi ya Rais-UTUMISHI

Ofisi ya Rais-UTUMISHI Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA TASAF KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO, YA...
14/08/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA TASAF KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO, YASISITIZA KUENDELEZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA KUFIKIA WALENGWA WALIOKUSUDIWA ILI KUTIMIZA MALENGO YA PSSN III

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 14 Agosti, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III) na kutoa maelekezo ya kuendeleza misingi ya utekelezaji wenye ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika kufikia walengwa waliokusudiwa na kutimiza malengo ya PSSN III.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezungumza hayo leo tarehe 14 Agosti, 2026 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kilicholenga kupokea taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III).

Vilevile, Mhe. Dkt. Ndumbaro ameipongeza TASAF kwa utekelezaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi kwenye sekta ya elimu na afya.

“Kwa niaba ya Kamati yangu nitoe pongezi nyingi kwa ofisi hii, kwa hakika mnafanya kazi nzuri katika mpango wa kunusuru kaya maskini, lakini pia mnatekeleza vizuri Miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi kwenye sekta ya elimu na afya, mnamwakilisha vizuri Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi hii’’ Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro

Awali akiwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa kuhusu hatua ya mchakato wa maandalizi, matarajio na hatua za utekelezaji wa kipindi cha tatu cha mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN III), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema, PSSN III iliidhinishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia tarehe 10 Aprili 2026, na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi kabla ya kuanza utekelezaji.

Naibu Waziri Qwaray amesema kuwa, katika maandalizi ya utekelezaji wa PSSN III, hatua muhimu zimekamilika ikiwemo kukamilisha usanifu wa Mpango, kuandaa nyaraka mbalimbali za utekelezaji, miongozo ya kiutendaji na kuimarisha mifumo ya TEHAMA inayosimamia shughuli za Mpango.

Aidha ameongeza kuwa, mchakato wa utambuzi wa Mamlaka za Maeneo ya Utekelezaji yatakayoshiriki kwenye utekelezaji wa Mpango unaendelea na unaojumuisha timu ya wataalamu kutoka TASAF, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), pamoja na wataalamu wa mazingira ambapo uchambuzi na uchakataji huo utazingatia viwango vya umaskini katika ngazi ya Halmashauri pamoja na viashiria vya athari za kimazingira, ikiwemo uwezekano wa maeneo kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na majanga mbalimbali.

Vilevile, Mhe. Qwaray amesema kupitia mpango huo unatarajiwa kuongeza uwezo wa kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi kukabiliana na changamoto za kiuchumi, kijamii na kimazingira, kuongeza ujuzi na taaluma kwa vijana kutoka kaya maskini na zinazoishi katika mazingira hatarishi zitakazoweza kujiajiri na kuajiriwa, kuwa na masijala ya kitaifa (kanzi data) yenye taarifa muhimu ya kaya maskini na zilizopo katika mazingira hatarishi pamoja na urasimishwaji wa TASAF k**a taasisi ya umma ya kutekeleza na kusimamia utoaji wa huduma za msaada ya kijamii itakayohakikisha uendelevu, ufanisi na uratibu wa utoaji wa huduma hizo nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Shedrack Mziray ameishukuru Kamati hiyo kwa maoni na ushauri mbalimbali ambao wameutoa na kuahidi kufanyia kazi ili kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIELEKEZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUTOA HUDU...
13/08/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIELEKEZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUTOA HUDUMA KIDIJITI

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 13 Agosti, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa ya utendaji wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambapo imeielekeza Taasisi hiyo kujikita zaidi kidijiti katika utoaji wa huduma mbalimbali kuhusu namna Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inavyofanya kazi jambo ambalo litawasaidia Viongozi wanaowajibika chini ya Sheria ya Maadili kuhusu Ujazaji wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni pamoja na Hati ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma na Uwajibikaji wa pamoja ili waweze kukamilisha kwa wakati taarifa zitakazohitajika katika ujazaji wa fomu hizo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akihitimisha kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kilichokuwa na lengo la kupokea taarifa ya Utendaji wa Taasisi hiyo kuhusu usimamizi na ushughulikiaji wa maadili ya Viongozi wa Umma ikiwemo uhakiki wa uzingatiaji wa ahadi za uadilifu, tamko la mali na madeni na ushughulikiaji wa malalamiko na mashauri.

Mhe. Dkt Ndumbaro pia amesisitiza suala la kuongeza juhudi za kutoa elimu zaidi ya namna ya kujaza fomu mbalimbali za Maadili kwa Viongozi ili kuepukana na changamoto ya kuchelewesha ujazaji wa taarifa kwani, kuna baadhi ya Viongozi wanakuwa wapya katika uongozi hivyo inawalazimu kupewa uelewa mpana utakaowaongoza katika ujazaji wa fomu hizo.

Ameongeza kuwa, utoaji wa elimu zaidi utasaidia jamii kuona namna Taasisi hiyo inavyofanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi.

“Ni vema kuongeza elimu zaidi kuhusu ujazaji wa fomu za maadili kwa Viongozi wanaowajibika chini ya sheria ili kuepukana na changamoto mbalimbali, wakati mwingine tunapata Viongozi wapya ambao hawana uelewa mpana juu ya ujazaji wa fomu hizo, hivyo elimu itakapotolewa itasaidia kupunguza changamoto hizo na kujaza kwa wakati fomu husika lakini pia elimu hiyo itawapa wananchi uelewa zaidi wa namna Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi,’’ Amesema Mhe. Dkt. Ndumbaro

Akiwasilisha taarifa hiyo, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.

Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri wa ofisi hiyo, Mhe. Regina Qwaray amesema Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ina jukumu la kusimamia tabia na mienendo ya Viongozi wa Umma ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Maadili.

Mhe. Qwaray amesema, Majukumu ya Msingi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni pamoja na kupokea na kufanya uhakiki wa Matamko ya Viongozi wa Umma kuhusu Rasilimali, kufanya utafiti juu ya hali ya Maadili na kushauri na kuweka mikakati katika masuala yanayohusu Uadilifu nchini, kufanya uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa maadili yaliyotajwa na Sheria, kupokea na kushughulikia malalamiko na taarifa za ukiukwaji wa Maadili kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka kwa wananchi pamoja na kutoa elimu ya Maadili kwa Viongozi wa Umma.

Naibu Waziri Qwaray ameongeza kuwa, Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Juni 2026, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetekeleza kazi za usimamizi na ushughulikiaji wa maadili ya viongozi wa umma ikiwemo uhakiki wa uzingatiaji wa ahadi za uadilifu, tamko la mali na madeni na ushughulikiaji wa malalamiko na mashauri pamoja na kusaini hati husika pindi viongozi wanapoteuliwa, kuajiriwa au kuchaguliwa.

Pia Mhe. Qwaray amesema, elimu ya maadili itaendelea kutolewa katika shule na vyuo kupitia klabu za maadili ili kuweza kujenga na kuimarisha maadili ya kitaifa na kuyafanya yawe sehemu ya jamii pamoja na kuzuia mmomonyoko wa maadili nchini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Sheria ya Ulinzi wa watoa taarifa ambayo inamhakikishia usalama na ulinzi.

Akitoa neno la shukrani kwa Kamati hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa kuendelea kutoa miongozo na maelekezo ya kiutendaji ambayo yanaongeza chachu na ufanisi katika kuboresha na kuimarisha utendaji kazi na kuleta tija katika kuwahudumia Viongozi na Wananchi kwa lengo la kujenga na kuimarisha Utawala Bora nchini.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, YASISITI...
12/08/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA, YASISITIZA UTOAJI WA ELIMU KUHUSU RUFAA NA MALALAMIKO KWA WATUMISHI WA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 12 Agosti, 2026

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea taarifa ya utendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma na kusisitiza kutolewa kwa elimu zaidi kwa Watumishi wa Umma ili waweze kuwasilisha rufaa na malalamiko kwa wakati na mahali husika kwa lengo la kutimiza haki na wajibu katika utendajikazi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokuwa akiongoza kikao cha Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Tume ya Utumishi wa Umma kilicholenga kupokea taarifa ya Utendaji wa Tume hiyo katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira.

“Elimu inahitajika zaidi kwa Watumishi wa Umma kwenye maeneo yao ya kazi ili kuongeza uelewa wa namna ya kushughulikia rufaa na malalamiko hayo ikiwa ni pamoja na kupata utatuzi wa migogoro katika Utumishi wa Umma,’’ Amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Ndumbaro amempongeza na kumshukuru Waziri Kikwete kwa taarifa nzuri aliyoiwasilisha kwa Kamati hiyo iliyoelezea kwa kina taarifa ya utendaji ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira ambayo itaongeza chachu ya utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameiahidi Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kuwa itashirikiana nayo katika usimamizi wa masuala mbalimbali ili kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

Awali akiwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa ya utendaji ya Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa na malalamiko kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Ajira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, Tume ya Utumishi wa Umma ni Mamlaka ya Rufaa kwa Watumishi wa Umma katika taasisi 554 waliopo kwenye makundi mbalimbali ya Watumishi wa Umma, Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Watumishi waliopo katika Taasisi za Umma.

Vilevile, Mhe. Kikwete amesema Tume hiyo ina jukumu la kupokea malalamiko na rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi wa mamlaka zao za ajira, mamlaka za nidhamu na waajiri baada ya uamuzi walioufanya na mamlaka hizo hivyo, elimu itakayotolewa kwa Watumishi wa Umma itasaidia kwa kiasi kikubwa kupata haki na wajibu kwa kila mmoja.

Aidha, Mhe. Kikwete ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kuwa na majadiliano mazuri na ofisi anayoiongoza ambayo wanaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi na utendaji wa majukumu yao.

“Mhe. Mwenyekiti, nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya ofisi ninayoiongoza mara zote tumepokea maoni, ushauri na michango mbalimbali kutoka katika Kamati yako inayolenga kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa lengo la kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Kamati hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kuiongoza Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwapatia maarifa mengi kutoka kwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo yenye kuleta tija katika kuwahudumia wadau mbalimbali na kuboresha utendajikazi.

UTUMISHI, BODI YA MIKOPO ZANZIBAR ZASAINI MAKUBALIANO KUBADILISHANA TAARIFANa Eric Amani, Mji wa Serikali Mtumba.Ofisi y...
12/08/2026

UTUMISHI, BODI YA MIKOPO ZANZIBAR ZASAINI MAKUBALIANO KUBADILISHANA TAARIFA
Na Eric Amani, Mji wa Serikali Mtumba.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesaini makubaliano ya ushirikiano na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHELB) kwa ajili ya kuwezesha kubadilishana taarifa kati ya Mfumo wa Taarifa za Watumishi wa Umma wa Tanzania Bara na mfumo wa Bodi hiyo.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo, Agosti 12, 2026 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Juma Selemani Mkomi na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar Ndugu Umrat Mohamed.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini, Katibu Mkuu Mkomi amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kutumia mifumo ya kidijitali kuboresha usimamizi wa taarifa na utoaji wa huduma kwa Watumishi wa Umma.

Amesema kubadilishana taarifa hizo kutasaidia kubaini wanufaika wa mikopo ambao ni watumishi wa umma na kuwezesha wale wenye madeni ya mikopo kutekeleza wajibu wao wa kurejesha fedha walizogharamiwa na Serikali.

“Utaratibu huu utasaidia kuhakikisha taarifa za watumishi wanaonufaika na mikopo zinapatikana kwa usahihi na kwa wakati, jambo litakalorahisisha urejeshaji wa mikopo na kuimarisha usimamizi wa fedha za Serikali,” amesema Mkomi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dkt. Mwanakhamis A. Ameir, ameishukuru Ofisi ya Utumishi kwa kuwezesha hatua hiyo, akieleza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuimarisha mifumo ya taarifa na usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu Zanzibar.

Amesema kuunganishwa kwa mifumo hiyo kutarahisisha upatikanaji na uhakiki wa taarifa za wanufaika, hivyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mikopo na urejeshaji wake.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa Taasisi hizo katika usimamizi wa taarifa, kuongeza usahihi wa taarifa za wanufaika wa mikopo na kuwezesha huduma kutolewa kwa haraka, uwazi na ufanisi zaidi, sambamba na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utendaji wa Serikali.

Hatua hiyo pia inaweka msingi wa mifumo ya taarifa za watumishi wa umma wa Tanzania Bara na Zanzibar kuwasiliana na kubadilishana taarifa kwa ufanisi, kwa kuzingatia taratibu za usalama na usiri wa taarifa.

NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA, BI. PRISCA LWANGILI AONGOZA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA OFISI HI...
11/08/2026

NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA, BI. PRISCA LWANGILI AONGOZA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA OFISI HIYO KWA LENGO LA KUIMARISHA AFYA ZAO

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI ASISITIZA UJUZI NA HAIBA YA UONGOZI KATIKA URITHISHANAJI MADARAKA KWA WATUMISHI WA UMMANa Ant...
10/08/2026

NAIBU KATIBU MKUU LWANGILI ASISITIZA UJUZI NA HAIBA YA UONGOZI KATIKA URITHISHANAJI MADARAKA KWA WATUMISHI WA UMMA

Na Antonia Mbwambo - Dodoma
Tarehe 10 Agosti, 2026

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Prisca Lwangili, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujenga ujuzi wa kitaalamu na haiba ya uongozi katika kuwaandaa warithi wa madaraka ili kuhakikisha kunakuwa na mwendelezo wa utendaji na utoaji wa huduma bora katika Taasisi za umma.

Bi. Lwangili ameyasema hayo leo, Agosti 10, 2026, wakati akihitimsha mafunzo ya uelewa kuhusu Urithishanaji Madaraka yaliyofanyika katika eneo maalumu la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma.

Amesema maandalizi ya urithishanaji madaraka yanapaswa kuanza mapema kwa kuwajengea uwezo unaohitajika katika nafasi za uongozi wanazotarajiwa kuzishika.

Aidha, Bi. Lwangili ameongeza kuwa ujuzi wa kitaalamu (Technical Skills) humwezesha Mtumishi kuwa na maarifa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, huku haiba ya uongozi ikimsaidia kuwasiliana vizuri, kujiamini, kushirikiana na wengine, kuwa mwadilifu, kufanya maamuzi na kuwajibika.

“Kuwa na ujuzi wa kitaalamu pekee hakutoshi. Mtumishi anayejengwa kuwa Kiongozi wa baadaye anapaswa pia kuwa na haiba inayomjengea uwezo wa kuwasiliana vizuri, kujiamini, kushirikiana na wengine, kuwa mwadilifu, kufanya maamuzi na kubeba majukumu kwa uwajibikaji,” amesema Bi. Lwangili.

Pia Bi. Lwangili amesisitiza kuwa, Urithishanaji Madaraka si kumwandaa mtu kuchukua nafasi ya Kiongozi aliyepo pekee, bali ni kuimarisha Taasisi kwa kuwa na Watumishi wenye uwezo wa kuendeleza majukumu na huduma za umma.

Kwa upande wake, Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Bertha Bomani, ameeleza kuwa Urithishanaji Madaraka ni mchakato wa kuwaandaa mapema Watumishi wenye uwezo na sifa stahiki kwa ajili ya majukumu ya uongozi.

Bi. Bomani amebainisha mikakati ya Urithishanaji Madaraka katika Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya uelewa na kujenga uwezo kwa Viongozi na Watumishi kuhusu manufaa ya kuandaa na kutekeleza Mpango wa Urithishanaji Madaraka, pamoja na kuwakumbusha Waajiri kutenga fedha katika bajeti za Taasisi zao kwa ajili ya uandaaji na utekelezaji wa mpango huo.

Heri Ya sikukuu ya Wakulima
08/08/2026

Heri Ya sikukuu ya Wakulima

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE, APONGEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHINa. Mwandishi Wetu-DodomaKati...
07/08/2026

KATIBU MKUU MKOMI ATEMBELEA MAONESHO YA NANENANE, APONGEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI

Na. Mwandishi Wetu-Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika Maonesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Mkomi, amepongeza utoaji wa huduma zinazotolewa kwa Watumishi wa Umma na Wananchi ambapo amewahimiza kufika katika maonesho hayo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

“Nashukuru nami nimepata nafasi ya kufika katika viwanja hivi kuona shughuli na huduma mbalimbali ambazo zinatolewa katika viwanja hivi, nipongeze waandaaji wa Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (Nanenane), huduma zinazotolewa ni nyingi hivyo niwahimize Watumishi wa Umma na Wananchi kufika katika maonesho hayo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali”, amesema Bw. Mkomi

KIKWETE AFUNGUA PAREDI YA MIFUGO NA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NANENANENa Eric Amani, DodomaWaziri wa Nchi Ofisi ya Rai...
05/08/2026

KIKWETE AFUNGUA PAREDI YA MIFUGO NA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NANENANE

Na Eric Amani, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesisitiza wafugaji kuendelea kutumia mbinu bora za ufugaji katika kuongeza thamani ya mifugo ili kukidhi matakwa ya soko la ushindani wa mifugo ndani na nje ya nchi.

Mhe. Kikwete amebainisha hayo leo tarehe 5 Agosti, 2026 wakati akifungua Paredi ya Mifugo katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima maarufu k**a Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa paredi hiyo, Mhe. Kikwete alisema kuwa sekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa kupitia uzalishaji, biashara na ajira. Hivyo, hatuna budi kuongeza juhudi na jitihada za kuimarisha mbinu za ufugaji bora kwa maslahi ya taifa.

Vile vile, Mhe. Kikwete aliwataka wadau wa sekta ya mifugo kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa sera na programu mbalimbali zinazolenga kuboresha huduma za ugani, udhibiti wa magonjwa ya mifugo na kuimarisha miundombinu ya masoko.

“Nitumie fursa kuwahamasisha wafugaji wote nchini kubadilisha mtazamo wa ufugaji wa kimazoea kwenda ufugaji unaotumia sayansi, takwimu na teknolojia na pia kushiriki na kuleta mifugo yao kwa ajili ya gwaride na mashindano kwa mwaka ujao 2027” alisema Kikwete.

Aidha, Paredi hiyo ilihusisha maonesho ya aina mbalimbali za mifugo ikiwemo ng'ombe, mbuzi na mifugo mingine ambapo wafugaji na taasisi mbalimbali walipata fursa ya kuonesha ubora wa mifugo yao pamoja na teknolojia na ubunifu unaotumika katika kuendeleza sekta hiyo.

Waziri Kikwete pia alitoa rai kwa taasisi za fedha nchini kuendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu na kubuni huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wafugaji, hususan wanawake na vijana, ili waweze kuwekeza katika sekta hii.

Pamoja na ufunguzi wa paredi ya mifugo, Mhe. Kikwete amezindua rasmi kituo cha huduma kwa wateja cha Wizara ya Kilimo na Uvuvi ambacho kitakuwa mahususi kwa ajili ya kutoa nakupokea taarifa za Kilimo na Uvuvi.

Amewataka watumishi watakaokuwa katika kituo hicho kupokea na kujibu hoja za wakulima, wafugaji na wavuvi kwa wakati ili kurahisisha zoezi la uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za kilimo.

MHESHIMIWA KIKWETE AONGOZA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS – UTUMISHI BI. PRISCA LWANGILI Na. Mwandishi Wet...
05/08/2026

MHESHIMIWA KIKWETE AONGOZA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS – UTUMISHI BI. PRISCA LWANGILI

Na. Mwandishi Wetu-Dodoma
Tarehe 5 Agosti, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameongoza mapokezi ya
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Prisca Lwangili aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi kustaafu Utumishi wa Umma.

Bi. Prisca Lwangili, amepokelewa rasmi leo na Viongozi na Watumishi wa ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mheshimiwa Kikwete amemkaribisha Bi. Lwangili na kumsihi kutumia uzoefu wake katika kazi kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo ili kuongeza uwajibikaji katika kuhudumia wananchi kwa ustawi wa Taifa

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mheshimiwa Regina Qwaray, amemkaribisha Bi. Lwangili na kueleza kuwa Viongozi pamoja na Watumishi wa Ofisi hiyo wapo tayari kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake mapya, ili kuimarisha utendaji wa ofisi kwa manufaa ya umma.

Naye Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi, amesema uongozi na watumishi wa Ofisi hiyo wako tayari kushirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu huyo ili kuhakikisha majukumu ya Ofisi yanatekelezwa kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Kwa upande wake, Bi. Lwangili amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua katika nafasi hiyo ambapo ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa kujituma na kuongeza ubunifu ili kuhakikisha malengo ya ofisi hiyo yanafikiwa kwa manufaa ya Serikali na wananchi.

Aidha, ameishukuru ofisi hiyo kwa mapokezi aliyopata na kuahidi kufanya kazi kwa ufanisi katika kuwahudumia Wananchi.

Address

670
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Rais-UTUMISHI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Rais-UTUMISHI:

Shortcuts

Share

Category