WCF Tanzania

WCF Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from WCF Tanzania, Government Organization, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Jengo la Kambarage, Ghorofa ya Tatu, 1 Barabara ya Kambarage, S. L. P 329, 41101 Dodoma, Dodoma.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263] kwa lengo la kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Idara ya Kazi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira...
04/09/2026

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Idara ya Kazi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano zimepanga kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa elimu kwa wadau kuhusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi.
Maeneo hayo ni pamoja na kujengeana uwezo na uelewa juu ya haki, wajibu na taratibu za madai ya fidia kwa wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha haki stahiki inapatikana kwa wakati kwa wafanyakazi wanaoumia au kupata ugonjwa unaotokana na kazi zao.
Hayo yamejiri jijini Dodoma leo wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Kazi kwa mwaka 2025/26 kilichowakutanisha maafisa kazi wafawidhi kutoka mikoa yote nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho, Kamishna wa Kazi Bi. Susan Mkangwa aliwakumbusha maafisa kazi juu ya wajibu wao katika kuimarisha usimamizi wa sheria ya kazi nchini, kufanya kaguzi zenye tija na kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ili kuimarisha ustawi wa nguvu kazi kazi ya Taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, pamoja na kuwapongeza maafisa kazi kwa namna wanavyoshirikiana na WCF katika kutoa elimu kwa wadau kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi, aliwataka pia kuongeza mkazo katika elimu ya haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi katika kuhakikisha sheria ya fidia kwa wafanyakazi inazingatiwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Maelezo News Msemaji Mkuu wa Serikali

TANGAZO LA MNADAHon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News
03/09/2026

TANGAZO LA MNADA

Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News



31/08/2026

Ushuhuda wa mnufaika wa WCF

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News




SALAMU ZA PONGEZIBodi ya Wadhamini, Menejimenti na Watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), inakupongeza Mhe. ...
29/08/2026

SALAMU ZA PONGEZI

Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), inakupongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuthibitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais

Ikulu Tanzania Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Deo Ndejembi Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News



Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unaendelea kushiriki katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea ka...
28/08/2026

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unaendelea kushiriki katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea katika Viwanja vya Jamhuri, Mkoani Morogoro.

WCF inaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea banda lake kwa kutoa elimu kuhusu Fidia kwa Wafanyakazi, mafao yanayotolewa na WCF pamoja na huduma za WCF Kidijitali. Aidha, wananchi wamepata fursa ya kuuliza maswali, kupata ufafanuzi wa huduma mbalimbali na kutoa mrejesho kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unashiriki katika tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea Katika Viwan...
27/08/2026

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unashiriki katika tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea Katika Viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro, kwa kutoa elimu kuhusu Fidia kwa Wafanyakazi, Mafao yanayotolewa na WCF, huduma za WCF Kidijitali pamoja na kupokea mirejesho kutoka kwa wananchi.

Tamasha hilo lenye kaulimbiu “Utamaduni Wetu: Nguzo ya Maadili, Uchumi Jumuishi na Utaifa, Karibu AFCON 2027” limeanza Agosti 24, 2026 litaendelea hadi 29 Agosti 2026.

📍 Karibu kwenye banda la WCF!
📅 Tupo hadi 29 Agosti 2026, siku ya kilele.

Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News



Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanawatakia Waislamu na Watanzania...
25/08/2026

Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Maulid.

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Zuhura Yunus Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News



24/08/2026

Ushuhuda wa mnufaika wa WCF baada ya kupata ajali kazini

Ofisi ya Waziri Mkuu Hon Deus Sangu Dr. Evaline Wilbard Munisi Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News




Address

Mkurugenzi Mkuu, Mfuko Wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), Jengo La Kambarage, Ghorofa Ya Tatu, 1 Barabara Ya Kambarage, S. L. P 329, 41101 Dodoma
Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222926107

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WCF Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to WCF Tanzania:

Shortcuts

Share