03/06/2026
Wadau wa Sekta ya Maji Wajadili Maendeleo ya Sekta
Wadau wa Sekta ya Maji nchini wamakutana kujadiliana maendeleo ya Sekta ya Maji.
Kikao kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ya Maji Bi. Rose Zacharia Ambrose akifungua kikao amesema Sekta ya Maji ndiyo nguzo muhimu katika kuhakikisha mipango iliyopangwa inakuwa endelevu na kutimia.
Amesema ni muhimu kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji na maendeleo yaliyofikiwa.
Bi. Rose amesema Wizara ya Maji inatambua uwepo wa changamoto ya kifedha katika kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ya utafiti wa vyanzo vya maji nchini na inatumia vyanzo mmbadala kufanikisha hilo.
Amewataka wadau wa Sekta ya Maji nchini kuandaa mkakati kufanikisha miradi ya maji.
Katika kikao hicho imeelezwa kuwa mojawapo ya changamoto zinazoikabili Sekta ya Maji ni pamoja na ongezeko la mahitaji ya huduma ya maji, mabadiliko ya tabianchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, Bw. Robert Sunday amesema lengo la serikali ni kuhakikisha huduma ya ni yenye ubora kwa matumizi, na maji kuwa chanzo kikubwa cha kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili changamoto, mafanikio ya Sekta ya Maji na mpango mkakati ya kutekeleza malengo ya sekta kwa miaka ijayo Ili kuboresha huduma za maji nchini.