Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia This is an official FACEBOOK PAGE for Ministry of Education, Science and Technology in Tanzania
(2)

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ujenzi wa vyuo vya VETA na utoaji wa ujuzi ni ajenda y...
15/08/2026

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ujenzi wa vyuo vya VETA na utoaji wa ujuzi ni ajenda ya kitaifa inayogusa moja kwa moja vijana, ajira na kuchochea maendeleo ya nchi na kwamba ni vigumu kuzungumzia ajira za vijana bila kuzungumzia ujuzi.

Waziri Mkenda amesema hayo Agosti 15, 2026 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Bahi kilichopo Mkoani Dodoma ambapo amesema ajenda hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye amesisitiza ujenzi na uboreshaji wa vyuo vya VETA katika wilaya mbalimbali nchini ili kuongeza ajira.

Ameongeza kuwa ajenda ya ujuzi ni sehemu ya agenda ya maendeleo ya nchi, kwa sababu vijana wenye ujuzi na shughuli za kiuchumi huwa na nafasi kubwa ya kushiriki moja kwa moja katika maendeleo ya taifa.

โ€œOngezeko la idadi ya vijana nchini linamaanisha kuwa kila mwaka kuna watu wengi zaidi wanaoingia katika uchumi na kuhitaji ajira au fursa za kujiajiri. Idadi hii kubwa ya watu ni baraka kwa taifa na Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu, ujuzi na ajira na ndicho tunachokifanya,โ€ amesisitiza Prof. Mkenda.

Prof. Mkenda ameongeza kwamba jitihada zinafanyika ili kuunganisha vyuo vya VETA na waajiri ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanaendana na mahitaji halisi ya soko la ajira.

Ameeleza kuwa Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kuunganisha vyuo na waajiri, pamoja na kuunda kamati zinazoshirikisha wataalamu kutoka sekta binafsi katika kupitia mitaala na kutoa ushauri kuhusu ujuzi unaohitajika.

โ€œVETA imeanza kufanya ufuatiliaji wa wahitimu (tracer study) kwa kuwasiliana na wahitimu na waajiri ili kubaini wanachofanya baada ya kuhitimu, namna wanavyotumia ujuzi walioupata na maeneo ambayo yanahitaji maboresho. Hatua hii inalenga kuhakikisha mitaala inaboreshwa mara kwa mara na wahitimu wanakuwa na uwezo unaokidhi mahitaji ya waajiri, amesisitiza Waziri Mkenda.



๐—•๐—”๐—›๐—œ ๐—œ๐—ก๐—”๐—ฉ๐—ฌ๐—ข๐—ช๐—˜๐—ž๐—˜๐—ญ๐—” ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ž๐—” ๐—˜๐—Ÿ๐—œ๐— ๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐—จ๐—™๐—จ๐—ก๐——๐—œ ๐—ก๐—” ๐—™๐—จ๐—ฅ๐—ฆ๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ฉ๐—œ๐—๐—”๐—ก๐—”Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imeonyesha mfano wa namna halm...
15/08/2026

๐—•๐—”๐—›๐—œ ๐—œ๐—ก๐—”๐—ฉ๐—ฌ๐—ข๐—ช๐—˜๐—ž๐—˜๐—ญ๐—” ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ž๐—” ๐—˜๐—Ÿ๐—œ๐— ๐—จ ๐—ฌ๐—” ๐—จ๐—™๐—จ๐—ก๐——๐—œ ๐—ก๐—” ๐—™๐—จ๐—ฅ๐—ฆ๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ฉ๐—œ๐—๐—”๐—ก๐—”

Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imeonyesha mfano wa namna halmashauri zinavyoweza kutumia mapato ya ndani kuwekeza katika elimu ya ufundi na kuwaandalia vijana fursa za kujiajiri. Kupitia Mfuko wa Elimu, Bahi inatenga shilingi milioni 100 kutoka mapato yake ya ndani, kusaidia vijana wa wilaya hiyo kupata elimu na ujuzi katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Bahi.

Hayo yameelezwa Agosti 15, 2026 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi, Mwanamvua Muyonga, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Bahi ambapo amesema kati ya wanafunzi 90 waliodahiliwa Chuoni hapo, 45 wanalipiwa ada na Halmashauri hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mfuko wa Elimu na juhudi za kuhakikisha vijana wanapata elimu inayowawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

โ€œHalmashauri yetu haiishii kwenye kulipa ada tu, tumejenga mfumo wa kuunganisha mafunzo, uwezeshaji na fursa za kiuchumi. Kupitia ushirikiano na VETA, vijana 127 wamepatiwa mafunzo ya udereva na baadaye kuwezeshwa mikopo yenye thamani ya takribani shilingi milioni 210, pamoja na kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kujiajiri,โ€ amesema DAS Muyonga.

Amesema Mfumo huo pia unaonekana katika mafunzo ya muda mfupi yanayotolewa kulingana na mahitaji ya jamii kwani vijana wa Bahi wamepatiwa mafunzo katika fani mbalimbali, ikiwamo uchomeleaji na upishi, huku baadhi ya waliohitimu mafunzo ya uchomeleaji wakiunda vikundi na kuanza kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Ameongeza kuwa juhudi hizo zimeenda sambamba na kuwaunganisha vijana wenye ujuzi na fursa za manunuzi ya umma na kwamba baadhi ya vikundi vya vijana vilivyopata mafunzo na mikopo kutoka halmashauri vimeanza kupata kazi katika miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, ikiwamo ujenzi wa madarasa, uchomeleaji, utengenezaji wa milango na madirisha na kufanya fedha zinazotengwa kuwezesha vijana kurejea tena katika uchumi wa eneo kupitia shughuli zao za uzalishaji.



Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Bahi,  Dodoma, kimejipanga kuimarisha huduma na kuongeza fursa za mafunzo ili kuwa k...
15/08/2026

Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Bahi, Dodoma, kimejipanga kuimarisha huduma na kuongeza fursa za mafunzo ili kuwa kitovu cha ujuzi na maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo jirani, hususan kwa kuwaandaa vijana wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.

Akizungumza leo, Agosti 15, 2026, wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Abdallah Ngodu, Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo hicho amesema Serikali imeendelea kusogeza fursa za elimu na mafunzo ya ufundi stadi karibu na wananchi.

Tangu kuanza kutoa mafunzo Oktoba 2024, Chuo hicho kimeongeza idadi ya wanafunzi kutoka 90 mwaka 2025 hadi 120 mwaka 2026, kikitoa mafunzo katika fani za ujenzi, uungaji na uundaji wa vyuma, umeme, ufundi wa magari, nguo na ushonaji, pamoja na mafunzo ya muda mfupi ya udereva, kompyuta na pikipiki.

Dkt. Ngodu amesema ongezeko hilo linaonesha mwamko wa wananchi, hususan vijana, katika kupata ujuzi wa kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri.

Aidha, VETA Bahi imejipanga kuboresha vifaa na mitambo ya kufundishia, kuongeza wigo wa mafunzo na kuwaendeleza wakufunzi ili kuendana na teknolojia na mahitaji ya soko la ajira ili kuandaa wataalamu wenye ujuzi na ubunifu watakaoshiriki katika maendeleo ya Taifa.



Tanga Tanga kumekucha! Viwanja vya Usagara vimepamba moto huku kipenga cha Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 kimeanza...
15/08/2026

Tanga Tanga kumekucha! Viwanja vya Usagara vimepamba moto huku kipenga cha Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 kimeanza rasmi.

Shughuli zimeanza kwa kishindo, zikileta pamoja Wizara, Taasisi, wabunifu na wadau wa elimu na teknolojia kuonyesha maarifa na suluhisho bunifu kwa taifa.

Wananchi wote mnakaribishwa kushuhudia ubunifu wa vijana, teknolojia mpya na elimu ya vitendo inayofungua milango ya kesho bora.

Hii ni nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kuchangamsha uchumi wa Taifa letu.

15/08/2026

๐—ช๐—ถ๐—ธ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—˜๐—น๐—ถ๐—บ๐˜‚, ๐—จ๐—ท๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—จ๐—ฏ๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ ๐—ถ๐—ธ๐—ผ ๐˜๐—ฎ๐˜†๐—ฎ๐—ฟ๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐—ฎ ๐—ณ๐˜‚๐—ฟ๐˜€๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ท๐—ถ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐˜‡๐—ฎ, ๐—ธ๐˜‚๐—ผ๐—ป๐—ฎ ๐—ฏ๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ถ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ด๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐˜‚๐—ฎ ๐—ณ๐˜‚๐—ฟ๐˜€๐—ฎ ๐—บ๐—ฝ๐˜†๐—ฎ.

๐—ง๐˜‚๐—ฝ๐—ผ ๐˜ƒ๐—ถ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ท๐—ฎ ๐˜ƒ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐˜€๐—ฎ๐—ด๐—ฎ๐—ฟ๐—ฎ - ๐—ง๐—ฎ๐—ป๐—ด๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ถ๐—ฎ ๐˜๐—ฎ๐—ฟ๐—ฒ๐—ต๐—ฒ ๐Ÿญ๐Ÿฑ - ๐Ÿฎ๐Ÿฐ ๐—”๐—ด๐—ผ๐˜€๐˜๐—ถ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ.

15/08/2026

๐—ช๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—ง๐—”๐—œ๐—™๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—˜๐—Ÿ๐—œ๐— ๐—จ, ๐—จ๐—๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—•๐—จ๐—ก๐—œ๐—™๐—จ
๐—ง๐—”๐—ก๐—š๐—”

Ungana nasi ndani ya Kipindi cha Meza Duara hapa 105.3 Mhz Maarifa FM tunazungumzia  ๐—ช๐—ถ๐—ธ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—˜๐—น๐—ถ๐—บ๐˜‚, ๐—จ๐—ท๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—จ๐—ฏ๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ...
15/08/2026

Ungana nasi ndani ya Kipindi cha Meza Duara hapa 105.3 Mhz Maarifa FM tunazungumzia
๐—ช๐—ถ๐—ธ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—˜๐—น๐—ถ๐—บ๐˜‚, ๐—จ๐—ท๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ป๐—ฎ ๐—จ๐—ฏ๐˜‚๐—ป๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฒ.

14/08/2026

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko ameishukuru Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kutekeleza ahadi ya kupeleka maonesho ya elimu, ujuzi na ubunifu mkoani Tanga.

Aidha, amewakaribisha wananchi wa Mkoa huo na mikoa jirani kushiriki kikamilifu ili kujionea namna elimu, ujuzi na ubunifu inavyotekelezwa kwa vitendo.

Mhe. Sekiboko amesisitiza kuwa maonesho haya si tu fursa ya kujifunza bunifu mpya, bali pia kuchangamsha uchumi wa Tanga kupitia wageni watakaofika na kutumia huduma za mkoa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Rashid Kassim Mchata, tarehe 14 Agosti, 2026 amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ...
14/08/2026

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Rashid Kassim Mchata, tarehe 14 Agosti, 2026 amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kuanzia tarehe 15 - 24 Agosti 2026 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara.

๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐—ก๐—–๐—›๐—œ ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ๐—•๐—œ๐—ฆ๐—›๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฆ๐—›๐—œ๐—ฅ๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ช๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—ง๐—”๐—œ๐—™๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—˜๐—Ÿ๐—œ๐— ๐—จ, ๐—จ๐—•๐—จ๐—ก๐—œ๐—™๐—จ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ง๐—”๐—ก๐—š๐—”Na WyEST Tanga  Wananchi wa Mkoa wa Tang...
14/08/2026

๐—ช๐—”๐—ก๐—”๐—ก๐—–๐—›๐—œ ๐—ช๐—”๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ๐—•๐—œ๐—ฆ๐—›๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฆ๐—›๐—œ๐—ฅ๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ช๐—œ๐—ž๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ž๐—œ๐—ง๐—”๐—œ๐—™๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—˜๐—Ÿ๐—œ๐— ๐—จ, ๐—จ๐—•๐—จ๐—ก๐—œ๐—™๐—จ ๐—ก๐—” ๐—จ๐—๐—จ๐—ญ๐—œ ๐—ง๐—”๐—ก๐—š๐—”

Na WyEST Tanga

Wananchi wa Mkoa wa Tanga na mikoa jirani wanahamasishwa kushiriki katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi, itakayofanyika kuanzia tarehe 15 - 24 Agosti 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga, ili kujifunza, kubadilishana maarifa na kutumia fursa mbalimbali za elimu, ujuzi na ubunifu.

Akizungumza Agosti 14, 2026, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Rashid Kassim Mchata, amesema maonyesho hayo yatashirikisha taasisi zaidi ya 300 pamoja na wadau wa sekta ya elimu, sayansi na teknolojia. Aidha, kutakuwa na mashindano ya ubunifu na ujuzi katika fani mbalimbali ikiwemo ushonaji, ususi, umeme na mengineyo, ambapo washindi wa kitaifa watapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mchata ameongeza kuwa wadhamini mbalimbali wakiwemo mabenki wamejitokeza kudhamini miradi ya ubunifu na kuunga mkono wajasiriamali chipukizi.

Kwa upande wake, Prof. Ladislaus Mnyone, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, alisema lengo kuu la wiki hiyo ni kuwaleta pamoja wadau kujadili na kuweka mikakati ya pamoja kuhusu elimu, ujuzi na ubunifu.

Amebainisha kuwa matukio makuu yatakuwa ni maonesho ya teknolojia yanayoonyesha mchango wa sayansi katika sekta mbalimbali, pamoja na kongamano la elimu na ubunifu litakalojadili utekelezaji wa Dira 2050.

Prof. Mnyone amefafanua kuwa kongamano hilo litaangazia nyenzo tano kuu: utafiti na maendeleo, sayansi na ubunifu, teknolojia za kidijitali, nishati, na usafirishaji funganishi.

Kupitia mijadala na maonesho hayo, Wizara inalenga kufanikisha malengo ya taifa ikiwemo kufikia uchumi wa dola trilioni 1 ifikapo mwaka 2050, kipato cha wastani cha mtu mmoja kati ya Dola za Marekani 7,000 - 12,000, na ajira zenye staha kwa angalau asilimia 50 ya Watanzania.

Address

Mji Wa Serikali Mtumba/Mtaa Wa Afya S. L. P 10
Dodoma
40479DODOMA

Opening Hours

Monday 02:00 - 15:30
Tuesday 02:00 - 21:30
Wednesday 02:00 - 21:30
Thursday 02:00 - 21:30
Friday 02:00 - 09:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia:

Shortcuts

Share