29/11/2021
ULEVI, DAWA ZA KULEVYA SIYO KIKI, JITAMBUE.
Vijana nchini Tanzania wametakiwa kutambua nafasi yao katika jamii na kuishi kwa malengo, kujithamini na kuamini kuwa wao ni wazazi na viongozi wa Taifa watumainiwa.
Wito huo umetolewa na Naibu katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge Mh. Casper Muya akizindua Mdahalo wa vijana kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Jiijini Mbeya Tarehe 28/11/2021.
Mh. Muya amesema vijana ni asilimia 68 ya watanzania wote jambo la kujivunia kuwa Taifa lina nguvu kazi ya kutosha lakini k**a vijana hao watajiinginza kwenye dhahama ya ulevi wa kupindikia, matumizi ya dawa za kulevya, bangi, mirungi,na tabia hatarishi k**a kujiingiza katika tabia ya ngono isiyo salama wataangamia na taifa itapoteza rasilimali hiyo muhimu .
Mh. Muya amewahasa vijana wanaoshiriki mdahalo huo kupitia programu za NYP+, BEILA,TIMIZA MALENGO na DREAMS ambazo zote zinashugulika na masuala ya vijana nchini na kuwataka kuwekeza katika stadi za maisha na kujielimsha zaidi kuhusu afua za kinga, tiba na matunzo ya VVU na UKIMWI zinazoratibiwa na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto kupitia NACP kulisaidia taifa kufikia malengo ya kutokomeza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030.
Naibu Katibu Mkuu, aliwataka vijana kuwa mabalozi wa afua za tohara, kutumia kondomu, kuwa waaminifu katika mahusiano, kusikiliza na kujifunza kupitia mawaidha ya viongozi wa dini, na Kuamini katika matumizi sahihi ya ARV kwa wale wanaoishi na VVU.