Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais Ukurasa rasmi wa Facebook wa Ofisi ya Makamu wa Rais

05/09/2026
Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha wananchi wananufaika na Biashara ya Kaboni kupitia ...
04/09/2026

Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha wananchi wananufaika na Biashara ya Kaboni kupitia misitu ikiwemo mikoko wanayopanda katika maeneo ya pwani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ameliarifu Bunge jijini Dodoma leo Septemba 04, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kiwani Mhe.Hija Hassan Hija aliyetaka kujua kwa namna gani wananchi hasa wa visiwani wanafaidika na mfumo wa kupata mitaji na elimu ya biashara ya kaboni.
Akijibu swali hilo, alisema Serikali imeendelea kujenga uwezo kwa jamii kupitia mafunzo na huduma za ushauri, kuunganisha miradi ya biashara ya kaboni na masoko ya kimataifa hatua iliyochangia miradi 117 kusajiliwa.
Ili kuendelea kuleta manufaa kwa upande wa Zanzibar, Mhe. Kwagilwa alimuelekeza Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) kushirikiana na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika kuwajengea uwezo wananchi wa ili wafaidike na biashara ya kaboni.
Aidha, Naibu Waziri huyo alieleza kuwa pamoja na kuwa suala la mazingira linalojumuisha NCMC si la Muungano, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ina inashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza hifadhi ya mazingira.
“Kwenye eneo hili tuna maelekezo mahsusi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyotoa alipofanya kikao na Wizara yetu alituelekeza kuhakikisha tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wanuifaike kwa kuhakikisha tunasajili miradi tunatoa huduma za kiushauri kwenye eneo la biashara ya kaboni,” alisema Mhe. Kwagilwa.
Akijibu swali la Mbunge huyo kuhusu Serikali imeweka mikakati gani ya kuwawezesha wananchi kuongeza wigo wa kufanya biashara ya kaboni, Mhe. Kwagilwa alisema NCMC imeendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani kwa kuandaa mikakati na miongozo ya upatikanaji wa fedha ili kuvutia wawekezaji wa ndani katika miradi ya kaboni.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemwakilisha Ra...
03/09/2026

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji wa tuzo za 19 za Rais za Wazalishaji Bora Viwandani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wazalishaji wa saruji nchini, kuhakikisha wanatafuta suluhu ya haraka ili kurejesha bei ya kawaida ya saruji kwa wananchi. Amesema maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanaweza kununua mfuko wa saruji kwa gharama nafuu hivyo ni lazima kuoanisha uzalishaji wa malighafi zote zinazochangia katika uzalishaji wa saruji ili bidhaa hiyo ipatikane kwa urahisi.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kufanya tathimini ya ukuaji wa viwanda hapa nchini ili kutambua ukuaji huo k**a unaviwezesha viwanda kuwa na ushindani wa masoko katika kanda, Afrika na Dunia kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wafanyabishaara wote wanaojihusisha na biashara haramu za uingizaji bidhaa bandia ambazo hukwepa kodi na tozo mbalimbali stahiki ambapo, zinaathiri ukuaji wa viwanda, kusababisha upotevu wa mapato ya serikali pamoja na kupunguza ushindani wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi.

Amewataka wazalishaji wa viwandani hapa nchini, kufanya jitihada za kuongeza uchakataji wa malighafi ndani ya nchi kwa kuhakikisha wanaongeza thamani, hatua itakayosaidia katika kuongeza ajira kwa watanzania na ukuaji wa uchumi kwa kasi.

Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakiki takwimu sahihi za idadi ya viwanda vilivyopo ili kuweka mikakati ya namna ya kuongeza wanachama wa Shirikisho la Viwanda Tanzania, hali itakayorahisisha uwepo wa chombo kimoja kinachowawakilisha wazalishaji wa viwandani.

Makamu wa Rais amesema katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania, sekta ya viwanda ina nafasi kubwa kwa kuwa ndiyo chimbuko la maendeleo ya haraka na ni muhimili mkuu katika uongezaji thamani wa malighafi zilizopo, utoaji ajira kwa wananchi, kuongeza mapato ya Serikali pamoja na fedha za kigeni. Pia, amesema sekta ya viwanda ni muhimu katika kuboresha sayansi na teknolojia na kuongeza uzalishaji, na hivyo kukuza ubunifu, uvumbuzi, uchumi, na kuondoa umasikini nchini.

Amesema kutokana na wingi wa rasilimali zilizopo nchini ikiwemo misitu na madini mbalimbali, ni muhimu kukuza sekta ya viwanda na kuendelea kujenga mahusiano kati ya sekta ya viwanda na nyingine ili kuongeza ufanisi, kuharakisha maendeleo jumuishi na hatimaye kuongeza kipato cha Watanzania walio wengi.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ili kuharakisha maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, amesema Wizara hiyo imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuhakikisha lengo lake la kuendeleza sekta ya viwanda linafanikiwa. Amesema Sekta hiyo imeendelea kujiimarisha ili kuongeza nafasi katika mchango wa pato la Taifa na kuongeza ufanisi kwa lengo la ukuaji wa sekta hiyo muhimu.

Amesema tayari Wizara imekamilisha na itazindua Sera ya Maendeleo endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya jasiriamali ndogo na za kati ya mwaka 2003 Toleo la mwaka 2025 ikiwa na lengo la kwenda sambamba na Dira 2050 ambayo inategemea uendelevu wa Viwanda.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Hussein Suphian Ally ameipongeza Serikali kwa mafanikio mbalimbali yanayoendelea kuimarisha mchango wa sekta ya viwanda nchini ikiwemo uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miradi ya kimkakati ambayo imeendelea kuongeza ushindani katika sekta ya viwanda.

Amesema CTI inapongeza juhudi za Serikali za kuendelea na ujenzi wa miradi ya Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa mitandao ya barabara pamoja na uwekezaji katika nishati na miundombinu mingine ya kiuchumi ambayo kwa pamoja imeendelea kupunguza gharama za usafirishaji, kurahisisha biashara na kuongeza uwezo wa bidhaa zinazozalishwa nchini kufikia masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.

Katika hafla hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezawadia tuzo ya heshima kwa kutambua mchango wake katika uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na viwanda nchini.

Hafla hiyo imewakutanisha wazalishaji wakubwa, wakati na wadogo, wafanyabiashara pamoja na wadau wengine wa sekta ya viwanda na biashara, huku tuzo hizo zikiendelea kuwa jukwaa la kuhamasisha ubora, ubunifu, uwekezaji, matumizi ya teknolojia na uzalishaji endelevu nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
03 Septemba 2026
Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki uapisho wa Wakuu wa Mikoa wanne na...
02/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameshiriki uapisho wa Wakuu wa Mikoa wanne na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo – Tunguu Zanzibar leo tarehe 02 Septemba 2026.

Viongozi walioapishwa ni pamoja na Mhe. CP Salum Rashid Hamduni, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mhe. Jumanne Abdallah Sagini, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Aidha, Ndg. Richard Marcellino Kayombo ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amemtembelea na kumjulia hali, Rais Mstaafu ...
02/09/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, amemtembelea na kumjulia hali, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, katika makazi yake Kibele, Mkoa wa Kusini Unguja, leo tarehe 02 Septemba 2026.

Address

Mtaa Wa Ofisi Ya Makamu Wa Rais, Mji Wa Serikali
Dodoma

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:30
Tuesday 08:00 - 15:30
Wednesday 08:00 - 15:30
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Makamu wa Rais posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Makamu wa Rais:

Shortcuts

Share