Ofisi ya Rais - Tamisemi

Ofisi ya Rais - Tamisemi Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI
(2)

Prime Minister’s Office, Regional Administration, and Local Governments (TAMISEMI) is a government Ministry under the Prime Minister’s office.

MKUU WA MKOA WA TANGA ATOA WITO WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA OWM SABASABANa. OWM- TAMISEMI,Dar es salaamMkuu wa Mkoa wa ...
13/07/2026

MKUU WA MKOA WA TANGA ATOA WITO WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA OWM SABASABA

Na. OWM- TAMISEMI,Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupata elimu ya masuala mbalimbali katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Ametoa wito huo hii leo (12 Julai, 2026)
alipotembelea na kujionea namna ofisi hiyo inavyoendelea kutoa huduma kwa wananchi na kuwasihi waendelee kujitokeza kwa wingi na kupata taarifa na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake.

Dkt. Batilda amepongeza namna Ofisi ya Waziri Mkuu ilivyojipanga na kuhakikisha inawafikia wananchi kwa utoaji wa huduma bora na kuzingatia viwango huku wakiendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii kupitia maonesho hayo.

Aidha amewakumbusha watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwa na program mbalimbali za elimu kwa umma ili kuifikia jamii kwa ukumbwa wake na kuendelea kutangaza huduma zinazotolewa.

Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere chini ya kaulimbiu isemayo, "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ni Fahari ya Tanzania," yakilenga kukuza biashara, uwekezaji na ubunifu, nchini.

NYAKUNGA: WENYEVITI WA MITAA NI NGUZO YA ULINZI WA MIPAKA Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Usimamizi na Udhibiti wa...
12/07/2026

NYAKUNGA: WENYEVITI WA MITAA NI NGUZO YA ULINZI WA MIPAKA

Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Fakih Nyakunga, ameiomba Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kuendelea kuhamasisha wenyeviti wa mitaa kushirikiana kwa karibu na Idara ya Uhamiaji katika kuwatambua wageni wanaoingia na kuishi katika maeneo yao ya utawala.

Ameyasema hayo leo Julai 12,2026 wakati jalipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2026) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama ni nguzo muhimu ya kuimarisha usalama wa mipaka ya Tanzania.

Amesema wenyeviti wa mitaa na vijiji wako karibu zaidi na wananchi, hivyo wana nafasi ya kipekee ya kufahamu wageni wanaoingia katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapobaini viashiria vya ukiukwaji wa sheria za uhamiaji.

“Tunaiomba TAMISEMI kuendelea kuwaelimisha na kuwashirikisha viongozi wa serikali za mitaa ili wajenge utamaduni wa kufahamu watu wanaoingia katika maeneo yao. Ushirikiano huu utasaidia kuimarisha usalama wa wananchi na kulinda mipaka ya nchi yetu,” amesema Nyakunga.

Amesisitiza kuwa udhibiti wa mipaka si jukumu la Idara ya Uhamiaji pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo yao katika kutoa taarifa sahihi kwa wakati.

Kwa upande wake, viongozi wa Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI walieleza kuwa ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za ulinzi na usalama katika kuhamasisha viongozi wa serikali za mitaa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha usalama, utawala bora na maendeleo ya wananchi.

PROF. NAGU ARIDHISHWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA BANDA JUMUISHI LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABANa OWM–TAMISEMI, Dar es Sala...
11/07/2026

PROF. NAGU ARIDHISHWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA BANDA JUMUISHI LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA

Na OWM–TAMISEMI, Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya katika Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Tumaini Nagu, ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na kupongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Akiwa katika ziara hiyo, Prof. Nagu amepata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za banda hilo na kupokea maelezo kuhusu huduma na mifumo mbalimbali inayowezesha wananchi kupata taarifa na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake.

Amesema banda hilo limekuwa jukwaa muhimu la kuwaelimisha wananchi kuhusu utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za kijamii, hususan katika sekta ya afya, elimu, utawala bora na maendeleo ya serikali za mitaa.

Prof. Nagu amewapongeza watumishi wanaohudumu katika banda hilo kwa kujituma, kutoa elimu kwa ufasaha na kuhakikisha kila mwananchi anayefika anapata huduma na taarifa sahihi zinazomwezesha kufahamu shughuli zinazotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.

Aidha, amewataka kuendelea kutumia maonesho hayo k**a fursa ya kusikiliza maoni ya wananchi, kupokea changamoto zao na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu huduma zinazotolewa, ili kuongeza uelewa na kuimarisha uhusiano kati ya Serikali na wananchi.

KILIMANJARO YANG’ARA SABASABA: NAIBU WAZIRI JAFFAR SEIF AITANGAZA K**A KITOVU CHA UTALII, BIASHARA NA AFYANa.OWM-TAMISEM...
10/07/2026

KILIMANJARO YANG’ARA SABASABA: NAIBU WAZIRI JAFFAR SEIF AITANGAZA K**A KITOVU CHA UTALII, BIASHARA NA AFYA

Na.OWM-TAMISEMI,Dar es salaam

Mkoa wa Kilimanjaro umeendelea kujidhihirisha kuwa moja ya nguzo muhimu za uchumi wa Tanzania baada ya kuangazwa kwa mafanikio makubwa katika maadhimisho ya Siku ya Kilimanjaro yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afya, Mhe. Jaffar Seif, ambaye alisema mkoa huo umebeba sura ya Tanzania duniani kupitia utalii, biashara, utamaduni na mchango wake katika maendeleo ya jamii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Seif amesema Mlima Kilimanjaro si kivutio cha utalii pekee bali ni alama ya Taifa inayovutia maelfu ya wageni kila mwaka na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa. Alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia kampeni za utalii.

Aidha, Mhe. Dkt.Seif ametaka wananchi na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na rasilimali za asili zinazobeba sekta ya utalii, akieleza kuwa utunzaji wa misitu, vyanzo vya maji na wanyamapori ni msingi wa kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi.

Maadhimisho hayo yalipambwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali za Kilimanjaro, vyakula vya asili, sanaa za utamaduni na fursa za uwekezaji zilizovutia idadi kubwa ya wananchi waliotembelea banda la mkoa huo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.

DKT. JAFFAR SEIF APONGEZA BANDA LA OWM–TAMISEMI SABASABA, ASEMA LINARAHISISHA WANANCHI KUPATA HUDUMANa OWM–TAMISEMI, Dar...
10/07/2026

DKT. JAFFAR SEIF APONGEZA BANDA LA OWM–TAMISEMI SABASABA, ASEMA LINARAHISISHA WANANCHI KUPATA HUDUMA

Na OWM–TAMISEMI, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif, amewapongeza watumishi wa Ofisi hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa ubora wa maandalizi na utoaji wa huduma, akisema limekuwa kituo muhimu kinachowawezesha wananchi kupata huduma na ufumbuzi wa changamoto mbalimbali sehemu moja.

Dkt. Seif amesema hayo leo Julai 10, 2026, baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu lililojumuisha taasisi zote zilizo chini ya Ofisi hiyo na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari.

Amesema wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kupata maelezo na majibu ya changamoto zinazohusu utawala wa mikoa na serikali za mitaa bila kulazimika kutembelea halmashauri au ofisi mbalimbali.

“Ndani ya banda moja mwananchi anapata huduma nyingi kwa wakati mmoja. Badala ya kwenda halmashauri moja hadi nyingine au ofisi mbalimbali, hapa anapata maelezo, ufumbuzi wa changamoto zake na pale inapohitajika, anaunganishwa moja kwa moja na wataalamu waliopo katika maeneo husika,” amesema Dkt. Seif.

Ameeleza kuwa wataalamu kutoka idara na taasisi mbalimbali zilizo chini ya OWM- TAMISEMI wamejipanga kutoa huduma, ushauri na ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo elimu, ujenzi, uhamisho wa watumishi, vibali pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na mamlaka za serikali za mitaa.

Aidha, amesema wananchi pia wanapata elimu na huduma kutoka taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu zikiwemo zinazoshughulikia masuala ya mifuko ya hifadhi ya jamii, watu wenye ulemavu, udhibiti wa dawa za kulevya na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI  wakitoa elimu kwa wananchi  kuhusu ubadilishaji wa tahasusi na shule kwa wana...
09/07/2026

Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu ubadilishaji wa tahasusi na shule kwa wanafunzi walipangwa kidato cha tano kwa mwaka 2026 kwenye maonesho ya 50 ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl.Nyerere,Jijini Dar es salaami

Maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. Karibu tukuhudumie
08/07/2026

Maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. Karibu tukuhudumie

Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata huduma, elimu na ufafanuzi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waz...
08/07/2026

Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata huduma, elimu na ufafanuzi kuhusu shughuli na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI katika Banda la hilo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Julai 8, 2026.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatu...
06/07/2026

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Matavilla atembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI lililopo viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam leo Julai 6, 2026

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatu...
06/07/2026

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Matavilla atembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI lililopo viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam leo juni 6,2026

Address

Goverment City, Mtumba. TAMISEMI Street
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Rais - Tamisemi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Rais - Tamisemi:

Shortcuts

Share