TASAF Tanzania

TASAF Tanzania Ukurasa rasmi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

Tunawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya siku ya Saba Saba
07/07/2026

Tunawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya siku ya Saba Saba

Viongozi na wageni mbalimbali wameendelea kutembelea banda la   katika  maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyi...
23/06/2026

Viongozi na wageni mbalimbali wameendelea kutembelea banda la katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika jijini Dodoma.

Miongoni mwa wageni hao ni pamoja na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Ndege Qwaray, Mkuu wa Mkoa Singida Mhe.Halima Dendego pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga Mhe.Gift Msuya.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF tunashiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Jijini Dodoma katika ...
16/06/2026

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF tunashiriki Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Jijini Dodoma katika Viwanja vya Chinangali.

Ushiriki wa   katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...
16/06/2026

Ushiriki wa katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, unaongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za TASAF pamoja na kukuza uwazi na uwajibikaji.

Tumeungana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika azma ya kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za...
05/06/2026

Tumeungana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika azma ya kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo jumuishi katika mkutano wa kimataifa ulioongozwa na mgeni rasmi Mhe. Dkt Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

04/06/2026

tunajivunia kushirikiana na Chuo cha Ustawi wa Jamii katika Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Uwezeshaji na Ustawi (ICPEW 2026), utakaofanyika Ijumaa, tarehe 5 Juni 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo jumuishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa   Shedrack Mziray kwa kushirikiana na Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii , Dkt Joyce Nyoni leo wame...
03/06/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Shedrack Mziray kwa kushirikiana na Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii , Dkt Joyce Nyoni leo wamekutana na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Uwezeshaji na Ustawi (ICPEW 2026), utakaofanyika Ijumaa, tarehe 5 Juni 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo jumuishi.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii   kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  unatoa elimu na huduma ya...
27/05/2026

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu unatoa elimu na huduma ya upatikanaji wa viambatanisho kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Zoezi hili linafanyika katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mbeya, Dar es Saalaam, Kagera, Kilimanjaro, Tabora, Zanzibar (Unguja na Pemba) ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia wanafunzi na wadau kupata taarifa sahihi kuhusu mchakato wa maombi ya mikopo.

Menejimenti ya   ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  imekutana  na Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia...
06/05/2026

Menejimenti ya ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji imekutana na Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa na kuwasilisha taarifa ya utelekezaji wa shughuli za TASAF, pamoja na maandalizi ya Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

  inawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
01/05/2026

inawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.

Address

S. L. P 2719
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TASAF Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to TASAF Tanzania:

Shortcuts

Share