Tanzania Insurance Regulatory Authority

Tanzania Insurance Regulatory Authority Official page of Tanzania Insurance Regulatory Authority

TIRA YAPOKEA MAONI YA WADAU WA MASUALA YA UDHIBITI UDANGANYIKA KATIKA BIMALeo tarehe 2 Septemba 2026, TIRA kupitia Kiten...
02/09/2026

TIRA YAPOKEA MAONI YA WADAU WA MASUALA YA UDHIBITI UDANGANYIKA KATIKA BIMA

Leo tarehe 2 Septemba 2026, TIRA kupitia Kitengo cha Udhibiti Udanganyifu imefanya kikao kazi na kampuni za bima lengo likiwa ni kupokea maoni na kujadili masuala mbalimbali ya Rasimu ya Mwongozo wa Udhibiti Udanganyifu ambao utatumika katika kutekeleza mapambano ya masuala hayo katika sekta ya bima.

Mwenyekiti wa kikao hicho; Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware ametoa wito kwa kampuni za bima kushirikiana na TIRA katika kudhibiti udanganyifu katika soko lakini na kuendelea kujielimisha kuhusu masuala ya udanganyifu katika bima. Kamishna pia amesisitiza juu ya uaminifu wa watumishi hao ili kulinda sekta ya bima kwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika soko.

Aidha, Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Dar es Salaam (NPS) imeshiriki kwa kutoa elimu kwa watoa huduma hao kuhusu makosa ya jinai yanayotokana na shughuli za biashara ya bima nchini yakiwemo kuhusu udanganyifu katika bima pia wametoa rai kutoa taarifa za udanganyifu katika soko ili wahusika washughulikiwe na vyombo vya sheria.

Naye, Meneja Udhibiti Udanganyifu TIRA Bw. Okoka Jailo Mgavilenzi amesema kikao hicho kimekuwa cha mafanikio makubwa kwa kupokea maoni na mapendekezo mengi ambayo yataboresha mwongozo huo na sekta itapata mwongozo ambao ni jumuishi kwa kuzingatia maoni ya sekta na siku za hivi karibuni mwongozo huo utatolewa kwa ajili ya matumizi ya soko, wadau wote wa biashara ya bima pamoja na wananchi kwa jumla. Zaidi Mwongozo huo utaeleza kuhusu kugundua, kuzuia na kutoa taarifa za udanganyifu.

Stay tuned for more details…
01/09/2026

Stay tuned for more details…

Tunakutakia kila la heri, Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kutek...
29/08/2026

Tunakutakia kila la heri, Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kutekeleza majukumu yako mapya ya kuendelea kuwatumikia Watanzania. 🇹🇿

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) tunakuahidi ushirikiano wa dhati katika utekelezaji wa majukumu yako kwa maendeleo na ustawi wa Taifa! 🇹🇿

TIRA YAUNGA MKONO POLISI JAMII CUP 2026 RUFIJI, YASISITIZA USALAMA BARABARANIMamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA...
28/08/2026

TIRA YAUNGA MKONO POLISI JAMII CUP 2026 RUFIJI, YASISITIZA USALAMA BARABARANI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa msaada wa jezi kwa ajili ya mashindano ya Polisi Jamii Cup 2026 yanayotarajiwa kufanyika mapema Septemba 2026; wilayani Rufiji mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi katika shughuli za kijamii na uhamasishaji wa usalama barabarani.

Aidha, Leo tarehe 28 Agosti 2026; SACP Protas Mutayoba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji (RPC) pamoja na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi wamefanya kikao cha kimkakati na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware katika Ofisi za TIRA, Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili na boresha mahusiano lakini pia kutoa shukrani kwa msaada huo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Saqware, amesema TIRA itaendelea kudhamini mashindano hayo na kuwa karibu na Jeshi la Polisi, hususan katika masuala yanayohusu usalama barabarani, pia amesisitiza kuwa TIRA itashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi Septemba 2026.

Kwa upande wake, RPC Rufiji amesema TIRA na Jeshi la Polisi ni wadau wakubwa katika masuala ya usalama barabarani na kuishukuru TIRA kwa msaada huo huku akieleza kuwa Polisi Jamii Cup ni fursa muhimu ya kuhamasisha usalama katika jamii, hususan kwa kundi la waendesha bodaboda.

TIRA YATOA ELIMU YA BIMA NA KUIBUA FURSA ZA BIASHARA KWA UTUMISHI SACCOS - UNGUJAMamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (...
26/08/2026

TIRA YATOA ELIMU YA BIMA NA KUIBUA FURSA ZA BIASHARA KWA UTUMISHI SACCOS - UNGUJA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Unguja tarehe 25 Agosti 2026 imefanya kikao maalum na Uongozi wa Utumishi SACCOS kwa lengo la kutoa elimu ya kina kuhusu masuala ya bima pamoja na kuainisha fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika sekta ya bima.

Kikao hicho kimelenga kuwajengea uelewa viongozi wa SACCOS kuhusu aina mbalimbali za bima, majukumu ya TIRA na namna chama hicho kinavyoweza kutumia fursa zilizopo katika sekta ya bima k**a sehemu ya kuongeza vyanzo vya mapato na kukuza shughuli zake za uwekezaji.

Meneja wa TIRA Kanda ya Unguja Bw. Said Salum aliueleza Uongozi wa SACCOS majukumu ya Mamlaka huku akisisitiza umuhimu wa uelewa wa bima katika kuchangamkia fursa zinazotokana na ukuaji wa sekta hiyo.

Naye, Afisa Bima wa TIRA Kanda ya Unguja, Bw. Adam Magori, ametoa elimu kuhusu aina mbalimbali za bima na kueleza kwa kina fursa ya biashara ya uwakala wa bima, ikiwemo namna ya kuanzisha uwakala, uendeshaji wake na mfumo wa mgawanyo wa kamisheni katika aina mbalimbali za bima.

Kupitia elimu hiyo, Uongozi wa Utumishi SACCOS ulionesha nia ya kuchunguza uwezekano wa kuanzisha uwakala wa bima k**a moja ya shughuli za uwekezaji na vyanzo vya mapato vya SACCOS.

METRO LIFE ASSURANCE YAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA BIMA YA MAISHADar es Salaam, Agosti 26, 2026Katika kuendele...
26/08/2026

METRO LIFE ASSURANCE YAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA BIMA YA MAISHA

Dar es Salaam, Agosti 26, 2026
Katika kuendeleza ziara zake kwa kampuni za bima nchini Tanzania, Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo Saqware, leo ametembelea Metro Life Assurance Company, ambapo amefanya mazungumzo na uongozi wa kampuni hiyo kuhusu hali ya utoaji wa huduma za bima, uendelevu na uhimilivu wa kampuni katika soko la bima, pamoja na mchango wa sekta ya bima katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.

Katika ziara hiyo, Metro Life Assurance kupitia Ndugu Amani Boma ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni, imeeleza kufurahishwa na ushirikiano wa karibu unaotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), hususan kupitia watendaji na wafanyakazi wake. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ushirikiano huo umekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa kampuni, kuimarisha shughuli zake katika soko na kuhakikisha mwendelezo wa utoaji wa huduma kwa wateja.

Aidha, kampuni imewasilisha mipango mbalimbali inayolenga kuimarisha na kuboresha huduma za bima, hususan bima ya maisha. Miongoni mwa mipango hiyo ni kuongeza juhudi za elimu kwa umma kuhusu bima kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, kuanzisha mifumo ya mawasiliano na vipindi vya majadiliano kwa njia ya webinar, pamoja na kuwawezesha wafanyakazi kushiriki mafunzo na masomo mbalimbali kwa lengo la kuongeza ujuzi, weledi na ufanisi katika utoaji wa huduma.

Metro Life Assurance pia imeeleza mafanikio iliyopata katika utekelezaji wa shughuli zake, huku ikibainisha kuwa mikakati na mipango hiyo inalenga kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizoibuliwa wakati wa kikao hicho na kuongeza ufanisi wa kampuni katika kuwahudumia wananchi. Aidha, Ndugu Amani Boma ameeleza kufurahishwa na ziara ya Kamishna na ujumbe wake kutoka TIRA Kwani umesaidia kuibua Maeneo yenye tija na kuzaa matunda katika utendaji.

TIRA YAFANYA MABADILISHANO YA UZOEFU NA TAASISI ZA BIMA KUTOKA ZIMBABWEMamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imep...
26/08/2026

TIRA YAFANYA MABADILISHANO YA UZOEFU NA TAASISI ZA BIMA KUTOKA ZIMBABWE

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imepokea ujumbe wa wageni kutoka Zimbabwe kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya usimamizi na uendelezaji wa sekta ya bima nchini Tanzania.

Ujumbe huo umetoka Wizara ya fedha nchini Zimbabwe na taasisi mbalimbali za bima ikiwemo Insurance and Pensions Commission (IPEC), Insurance Council of Zimbabwe (ICZ) pamoja na Washauri wa Bima. Ziara hiyo inalenga kuwawezesha wageni hao kujifunza kuhusu uzoefu wa Tanzania katika maeneo ya bima ya afya kwa wote (Universal Health Insurance) pamoja na Bima ya Usafiri wa Baharini (marine insurance).

Katika ziara hiyo ya siku mbili, tarehe 24 na 25 Agosti 2026, ujumbe huo umepata fursa ya kufahamu kwa kina mifumo, mikakati na uzoefu wa Tanzania katika kusimamia na kuendeleza huduma za bima, hususan katika maeneo hayo mawili.

Kwa upande wa bima ya afya kwa wote, wageni hao wanatarajiwa kujifunza kuhusu namna Tanzania inavyotekeleza na kusimamia mifumo inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za bima ya afya kwa wananchi, pamoja na nafasi ya wadau mbalimbali katika kuhakikisha huduma hizo zinawafikia watu wengi zaidi.

Katika eneo la Bima ya usafiri wa baharini (marine insurance), ujumbe huo umepata fursa ya kujifunza kuhusu usimamizi wa bima zinazohusiana na shughuli za usafirishaji na biashara za majini, ikiwemo mifumo ya udhibiti, ufuatiliaji wa shughuli za bima na namna sekta hiyo inavyosaidia kulinda maslahi ya wafanyabiashara na wadau wanaojihusisha na shughuli za usafirishaji majini.

Ziara hiyo pia inatoa fursa kwa TIRA na taasisi hizo za Zimbabwe kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto, mafanikio na mbinu bora katika usimamizi wa sekta ya bima. Mabadilishano hayo yanatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuwezesha taasisi hizo kujifunza kutoka katika uzoefu wa kila nchi.

Kwa ujumla, ziara hiyo inaonesha umuhimu wa ushirikiano na kubadilishana maarifa miongoni mwa mamlaka na taasisi za bima barani Afrika, kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa sekta, kuongeza ufanisi wa huduma za bima na kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya

Kheri ya Maulid al-Nabii ﷺ! 🌙✨Tunawatakia Watanzania wote Maulid yenye amani, upendo na baraka tele.Kheri ya Maulid al-N...
25/08/2026

Kheri ya Maulid al-Nabii ﷺ! 🌙✨

Tunawatakia Watanzania wote Maulid yenye amani, upendo na baraka tele.

Kheri ya Maulid al-Nabii ﷺ! 🌙✨

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inawatakia Watanzania wote Maulid yenye amani, upendo na baraka tele.
🤲🏽

TIRA YAMUAGA MWENYEKITI WA MABALOZI WA BIMA MHA. ZENA SAID, YAPONGEZA MCHANGO WAKE KATIKA KUKUZA SEKTA YA BIMAMamlaka ya...
21/08/2026

TIRA YAMUAGA MWENYEKITI WA MABALOZI WA BIMA MHA. ZENA SAID, YAPONGEZA MCHANGO WAKE KATIKA KUKUZA SEKTA YA BIMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) leo Agosti 21, 2026 imefanya hafla fupi ya kumuaga Mhe. Balozi Mhandisi Zena A. Said, ambaye amekuwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Bima tangu mwaka 2023, huku ikimpongeza kwa mchango wake katika kuhamasisha matumizi ya bima na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sekta ya bima.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Zena A. Said – Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia; amesema kupitia nafasi aliyoitumikia k**a Balozi wa Bima amejifunza mengi, ikiwemo mafunzo kuhusu bima na utatuzi wa migogoro. Ameipongeza TIRA kwa kazi nzuri inayofanya kwa kushirikiana na kampuni za bima, huku akihimiza kuendelea kutengeneza bidhaa na vifurushi vinavyokidhi mahitaji ya Watanzania, akitolea mfano Takaful inayozingatia misingi ya Sharia

Aidha, Kamishna wa Bima Dkt. Saqware ametaja mafanikio mbalimbali yalipotikana chini ya uongozi wa Balozi Zena ikiwemo kusukuma ajenda ya bima ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi na kuwaomba mabalozi wote kuendelea kuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya bima nchini.

Kwa upande wake, Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Bi. Margaret Mngumi, amemshukuru kiongozi huyo kwa hekima, uvumilivu na mchango wake katika kuimarisha ushirikiano na maridhiano ndani ya sekta ya bima. Pia Bi. Flora Minja akizungumza kwa niaba ya ATI amemshukuru Mhe. Zena kwa uongozi wake thabiti na kuahidi ushirikiano na Mkt. wa Mabalozi mpya katika masuala ya bima.

Nae Naibu Kamishna wa Bima Bi. Khadija Said, amemshukuru Balozi Zena kwa kwa kujitoa kwake katika shughuli mbalimbali za TIRA, na kuahidi kuendeleza kazi njema aliyoianza kwa kiongozi mpya na Mwenyekiti wa Mabalozi wa Bima ambaye ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansura Mossi Kassim.

TIRA YAFANYA TATHMINI YA UKATAJI WA BIMA KATIKA MIRADI YA SERIKALI ZANZIBARMaafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima T...
21/08/2026

TIRA YAFANYA TATHMINI YA UKATAJI WA BIMA KATIKA MIRADI YA SERIKALI ZANZIBAR

Maafisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), kwa kushirikiana na maafisa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma Zanzibar (ZPPRA) pamoja na Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar, wamefanya tathmini ya ukataji wa bima katika miradi ya Serikali ya majengo na miundombinu.

Tathmini hiyo imefanyika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, kwa lengo la kutathmini uzingatiaji wa matakwa ya bima katika utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa miradi ya Serikali inalindwa dhidi ya vihatarishi mbalimbali vinavyoweza kusababisha hasara, huku ikiimarisha uzingatiaji wa taratibu za ununuzi wa umma na matumizi sahihi ya bima katika mikataba ya miradi.

Aidha Meneja wa TIRA Kanda ya Unguja Bw. Salum Said amesema tathmini hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi za Serikali katika kuhakikisha bima inatumika ipasavyo k**a nyenzo muhimu ya kulinda mali, uwekezaji na maslahi ya Serikali na wananchi.

Kupitia zoezi hilo, TIRA inaendelea kusisitiza umuhimu wa taasisi za Serikali kuhakikisha mahitaji ya bima yanazingatiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya bima nchini.

Address

Dodoma
11104

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Insurance Regulatory Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Insurance Regulatory Authority:

Shortcuts

Share