Chama Cha Mapinduzi

Chama Cha Mapinduzi Ukurasa rasmi wa Chama Cha Mapinduzi. Chama Tawala Tanzania

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Akutana na Uongozi wa TISEZA Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, Dar es Salaam, 17 Agosti 2026.Ka...
17/08/2026

Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Akutana na Uongozi wa TISEZA Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba, Dar es Salaam, 17 Agosti 2026.

Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jamal Kassim Ali, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Uchumi ya Tanzania (TISEZA) Ndugu Gilead John Teri kuhusu fursa za kimkakati za uwekezaji na namna ya kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa.

Mazungumzo hayo yalijikita katika maeneo yenye uwezo mkubwa wa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza mapato, hususani uchukuzi na usafirishaji, madini, ardhi na majengo (real estate), pamoja na uwekezaji katika maeneo yenye fursa za kiuchumi.

Aidha, pande hizo zilijadili namna Chama kinavyoweza kuendelea kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kutekeleza kwa ufanisi vipaumbele vilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030, hususan katika kukuza uwekezaji, uzalishaji, ajira na mapato, kuelekea kufikia malengo makubwa ya uchumi yaliyowekwa na Taifa.

Ndugu Jamal alisisitiza umuhimu wa Chama kuwa na mtazamo wa muda mrefu katika kutambua na kutumia fursa za uwekezaji, huku akisisitiza kuwa ushirikiano na taasisi za Serikali, wawekezaji na sekta binafsi ni muhimu katika kubadili fursa zilizopo kuwa shughuli halisi za kiuchumi zenye tija.
Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za Chama Cha Mapinduzi za kujenga ushirikiano na wadau wa uchumi na uwekezaji, kwa lengo la kuongeza ufanisi, mapato na mchango wa rasilimali za Chama katika maendeleo ya Taifa.

πŸ“Έ ππˆπ‚π‡π€: Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahmoud Abdi, akiwa ameambatana na Katibu wa Kamati Maalumu ya NE...
16/08/2026

πŸ“Έ ππˆπ‚π‡π€: Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahmoud Abdi, akiwa ameambatana na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) CCM Zanzibar, Ndugu Khadija Salum Ali, kumpokea Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Ndugu Sophia Shaningwa, aliyewasili Visiwani Zanzibar.

Mapokezi hayo yanaonesha kuendelea kuimarika kwa uhusiano na ushirikiano wa kindugu kati ya CCM na SWAPO, pamoja na umuhimu wa kuendeleza mshikamano na mahusiano ya karibu kati ya vyama hivyo.

πŸ“† Agosti 15, 2026
πŸ“ Airport, Zanzibar

Tembelea: www.ccm.or.tz
_____________



CCM–SWAPO Zaimarisha Uhusiano wa Kihistoria KISIWANDUI, ZANZIBAR | 15 AGOSTI 2026 Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose...
16/08/2026

CCM–SWAPO Zaimarisha Uhusiano wa Kihistoria

KISIWANDUI, ZANZIBAR | 15 AGOSTI 2026

Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amempokea Katibu Mkuu SWAPO, kutoka Namibia, Ndugu Sophia Shaningwa, na kufanya naye mazungumzo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar.

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria kati ya CCM na SWAPO, hususan kwa kuongeza ushirikiano na mafunzo ya uongozi kwa vijana, wanawake na taasisi za vyama.

Viongozi hao pia wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa vyama vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika.

MWANRI ASISITIZA VIONGOZI KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA NA WANANCHI.Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzani...
15/08/2026

MWANRI ASISITIZA VIONGOZI KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA NA WANANCHI.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Aggrey Mwanri (MCC), leo Agosti 15, 2026, amekuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Hadhara wa Jimbo la Ubungo, ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Kabla ya kushiriki mkutano huo, Ndugu Mwanri alipokewa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Sekretarieti ya CCM Mkoa, chini ya Katibu wa CCM Mkoa, Ndugu Mkandawire.

Aidha, alipokea taarifa fupi kuhusu utendaji wa Chama katika Mkoa huo na kuwashukuru viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa usimamizi mzuri wa Chama na Serikali.

Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Mwanri amesisitiza umuhimu wa Wabunge, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuwapa wananchi mrejesho kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na CCM wakati wa Uchaguzi.

Aidha, amewasihi wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Kwa upande wake, Prof. Kitila Mkumbo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wananchi wa Jimbo la Ubungo, akieleza hatua zilizochukuliwa katika kuboresha miundombinu, hususan sekta ya barabara.

Prof. Kitila amesema ataendelea kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi na Serikali katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanaendelea kupata huduma na maendeleo yanayostahili.

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.

Makamu Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Stephen Wasira  amemjulia hali, Mama Fatma Karume, Mjane wa Rai...
15/08/2026

Makamu Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Ndg. Stephen Wasira amemjulia hali, Mama Fatma Karume, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba Zanzibar. Tarehe 15 Agosti 2026.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akifurahi na Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar ...
15/08/2026

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akifurahi na Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,Bi Fatma Karume, alipokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya Lumumba Zanzibar anapoendelea kupatiwa matibabu leo Tarehe 15 Agosti 2026.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharozi Migiro, amemjulia hali, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanziba...
15/08/2026

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharozi Migiro, amemjulia hali, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, ambaye anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba Zanzibar. Tarehe 15 Agosti 2026. Pichani Katibu Mkuu akiwa na wanafamilia na daktari hospitali ya Rufaa Lumumba.

VYAMA SITA VYA UKOMBOZI BARANI AFRIKA KUENDELEA  KUJIFUA KIUONGOZIAgosti 14, 2026 na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha ...
15/08/2026

VYAMA SITA VYA UKOMBOZI BARANI AFRIKA KUENDELEA KUJIFUA KIUONGOZI

Agosti 14, 2026 na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Ndugu Sophia Shaningwa akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Aggrey Mwanri amefungua mafunzo ya uongozi kwa vyama sita vya ukombozi barani Afrika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo makada kutoka Vyama hivyo na kuwaandaa kuwa wakufunzi watakaoweza kutoa mafunzo kwa makada wengine katika vyama vyao. Vyama hivyo ni CCM cha Tanzania, SWAPO cha Namibia, MPL cha Angola, ZANU PF cha Zimbabwe, ANC cha Afrika Kusini pamoja na FRELIMO cha Msumbiji.

15/08/2026

πŠπ€π–π€πˆπƒπ€: π‚π‚πŒ πˆππ€π–π„π™π€ πŠπ”πŠπ”π…π€ππ˜π€ π”πŠπ€π–π€ πŒπ€π€π‘π”π…π” 𝐍𝐀 πˆππ€π–π„π™π€ πŠπ”π‚π‡π”πŠπ”π€ π”πŒπ€π€π‘π”π…π” π–π€πŠπŽ

Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC), amesema hakuna mtu yoyote ambaye ni mkubwa kuliko Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwani Chama hicho kinaweza kumpa mtu umaarufu na kinaweza pia kuchukua umaarufu wake.

Ndugu Kawaida amesema hayo Agosti 7, 2026, akizungumza na Viongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu katika ufunguzi wa mafunzo yaliyofanyika Ihemi, mkoani Iringa.

Amewataka vijana kuendelea kukijenga Chama Cha Mapinduzi, akisisitiza kuwa watu huja na kuondoka, lakini CCM inaendelea kuwepo kutokana na uimara wake.

Tembelea: www.ccm.or.tz
__________



Address

Dodoma
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chama Cha Mapinduzi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Chama Cha Mapinduzi:

Shortcuts

Share