UWT TAIFA

UWT TAIFA Political Organisation

03/09/2026

kikao Cha Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) alipozungunza na Kamati ya Wabunge wa CCM (CAUCUS),September 2,2026 White House Jijini Dodoma Kenani Kihongosi

WASIRA ATETA NA WABUNGE WA CCM. MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM - Bara), Stephen Wasira, amekutana na kuzu...
03/09/2026

WASIRA ATETA NA WABUNGE WA CCM. MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM - Bara), Stephen Wasira, amekutana na kuzungumza na Kamati ya Wabunge wa CCM, tarehe 2, Septemba 2026, katika Ukumbi wa White House Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma. Katika kikao hicho Wasira aliambatana na ujumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro.

Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC)* akiwasili Bungeni  ...
01/09/2026

Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC)* akiwasili Bungeni kushiriki Kikao cha Tano cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 13 leo Septemba 1, 2026.

Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC)* akiwasili Bungeni  ...
31/08/2026

Mwenyekiti wa UWT Taifa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC)* akiwasili Bungeni kushiriki Kikao cha Nne cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 13 leo Agosti 31, 2026.

CHATANDA: NDEJEMBI ANA UWEZO MKUBWA WA KUMSAIDIA MAJUKUMU RAIS WETUNA: MWANDISHI WETU, DODOMAMakamu wa Rais, Deogratius ...
31/08/2026

CHATANDA: NDEJEMBI ANA UWEZO MKUBWA WA KUMSAIDIA MAJUKUMU RAIS WETU

NA: MWANDISHI WETU, DODOMA

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameelezwa kuwa kiongozi mahiri, muadilifu na mzalendo, mwenye uwezo wa kumsaidia majukumu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, Agosti 30, 2026, ofisini kwake Dodoma, siku moja baada ya kukamilika uapisho wa kiongozi huyo, Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Chatanda ameeleza, Ndejembi ni kiongozi wa vitendo na katika majukumu aliyoaminiwa tangu akiwa Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Mbunge, Naibu Waziri na Waziri kamili katika wizara mbalimbali.

"Kule Kongwa Dodoma akiwa Mkuu wa wilaya alifanya kazi nzuri na katika kilimo alisimamia kwa mafanikio makubwa kampeni yake aliyoiita ONJAKO yaani Ondoa Njaa Kongwa. Alihimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame k**a mtama, mihogo, ufuta na alizeti ili kuwaepusha wananchi na kadhia ya njaa," amesema Chatanda.

Ameongeza kuwa, kampeni ya ONJAKO ilipokelewa vizuri na wakulima wa Kongwa kutokana na mwanzo kutilia mkazo zao la mahindi ambalo mara kwa mara walikuwa wakipata mazao kidogo kutokana na changamoto ya ukame wilayani humo.

Akisisitiza utendaji uliotukuka wa Ndejembi, Chatanda amesema, Wizara kadhaa alizohudumu zikiwemo Tamisemi, Vijana, Ardhi, Nishati, ameacha alama kubwa kwa kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za wananchi.

"Ndejembi si mtu wa kukaa ofisini kusubiri taarifa, anakwenda mwenyewe kujionea utekelezaji wa majukumu na maagizo mbalimbali. Ndiyo maana nasema, Rais Dk. Samia amepata msaidizi mchapakazi na hodari kwelikweli," ameongeza.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa, ametoa rai kwa wananchi kumuombea Rais Dk. Samia, Makamu wa Rais, Ndejembi na viongozi wengine ili waweze kusimamia mipango iliyopo ambayo imejikita katika kukuza ustawi na maendeleo ya wananchi.

Awali, katika uapisho huo, Rais Dk. Samia amemuasa Makamu wa Rais Mteule kuwatumikia Watanzania bila kujali tofauti zao ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 na Dira ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo (2050).

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunga...
29/08/2026

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.

Hongera Ndg.Deogratius John Ndejembi kwa kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
29/08/2026

Hongera Ndg.Deogratius John Ndejembi kwa kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

29/08/2026

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.DKT.SAMIA SULUHU HASSAN BAADA YA UAPISHO WA MHE.DEOGRATIUS JOHN NDEJEMBI KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

29/08/2026

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi alivyoapa kushika wadhifa huo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

29/08/2026

UWT YAPONGEZA NDEJEMBI KUTHIBITISHWA KWA ASILIMIA 100 UMAKAMU WA RAIS

Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), chini ya Mwenyekiti wake Ndg.Mary Pius Chatanda (MCC) umepongeza uamuzi wa wabunge kumthibitisha Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais kwa kura 324, sawa na ushindi wa asilimia 100.

Address

Uhuru
Dodoma
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UWT TAIFA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to UWT TAIFA:

Shortcuts

Share