National Health Insurance Fund

National Health Insurance Fund The Management of the Fund is vested in the Board of Directors.

The Official Account of the National Health Insurance Fund (NHIF) of Tanzania I Ukurasa Rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 🇹🇿

Customer Service Toll Free - 199
Fraud Reporting Toll Free - 0800111163

www.nhif.or.tz The National Health Insurance Fund is a statutory health insurance scheme which was established by Parliamentary Act No.8 of 1999,in order to facilitate access to health services b

y the principal members and their dependants. The main objective for the establishment of the Fund was to administer the scheme and to formulate and promulgate policies for sound administration of the scheme. However, the day to day operations of the Fund are executed by the Director General on behalf of the Board of Directors. Generally, employers and employees in the public sector are obliged by the Law to register themselves and contribute to the Fund a total of six percent of employee’s salary,equally shared between the employer and the employee, except uniformed service men1 whose contribution is 6.25% and where paid by Government.The Fund covers members,their spouses and up to four children and/or dependants. The Membership size of the Fund has increased from 332,650 in June 2009 to 373,326 by June 2010, an increase equivalent to 12.2%.The beneficiaries have been increasing gradually from 1,830,375 in June 2009 to 1,971,251 as of 30th June 2010, equivalent to an increase of 7.7%. Extension of membership coverage has been made possible through the amendments of the NHIF Act,which extended the coverage to include all public servants2 instead of the previous Central Government employees . The following groups were taken on board namely public servants, councilors, and members of the Police force, Prisons, Immigrations, Fire and Rescue as well as other groups of persons. As the scope of membership and beneficiaries increases, the Scheme is expected to ultimately assume its national role as the major universal social health insurance provider. The Fund’s benefits package comprising of Registration and Consultation Fees, Outpatient Services, Medicines, Diagnostic Tests, Inpatient Services, Surgical Services, Physiotherapy and Optical Services. An important inclusion and enhancement in the package was the introduction of the Retirees benefits for the rest of their lives, a great stride in the Scheme’s milestones.The services are provided to beneficiaries through the Fund’s accredited health facilities which include Government, Faith Based and Private facilities that are located throughout the country. During the first two years of operations, the scheme encountered various challenges which hindered its smooth operation.In order to tackle the challenges,the focus was mainly on awareness creation to key stakeholders to ensure that they understand the Scheme and packages offered by NHIF. Now than ever before, stakeholders have started to understand the concept of social health insurance which has lead to increased applications of the excluded groups requesting to join the Fund.This is reflected by the increase of the membership base from 164,708 in 2001/02 to 373,326 observed by June 2010, accounting to an average annual growth rate of 14.1%.

30/08/2026

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uko kwenye mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura ya 395, kwa lengo la kupanua wigo wa wanachama, kuendana na mahitaji ya sasa ya huduma za afya na kuimarisha uendelevu wa Mfuko.

Marekebisho hayo pia yanalenga kuimarisha udhibiti wa matumizi mabaya ya Mfuko, ikiwemo udanganyifu unaoweza kufanywa na baadhi ya wanachama, waajiri na watoa huduma za afya lakini kwenda sambamba na sheria Mama ya Bima ya Afya kwa Wote.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!

Wizara Ya Afya Msemaji Mkuu wa Serikali Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania

SHERIA YA NHIF KUPANUA WIGO WA WANACHAMA NA KUBORESHA HUDUMAMfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uko kwenye mchakato wa...
30/08/2026

SHERIA YA NHIF KUPANUA WIGO WA WANACHAMA NA KUBORESHA HUDUMA

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uko kwenye mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura ya 395, kwa lengo la kupanua wigo wa wanachama, kuendana na mahitaji ya sasa ya huduma za afya na kuimarisha uendelevu wa Mfuko.

Marekebisho hayo pia yanalenga kuimarisha udhibiti wa matumizi mabaya ya Mfuko, ikiwemo udanganyifu unaoweza kufanywa na baadhi ya wanachama, waajiri na watoa huduma za afya lakini kwenda sambamba na sheria Mama ya Bima ya Afya kwa Wote.

Akizungumza Agosti 27, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa NHIF, Kinondoni, Dar es Salaam, wakati wa kupokea maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya sheria hiyo, Meneja wa Huduma za Sheria wa NHIF, Matamus Fungo, amesema sheria hiyo iliyotungwa mwaka 1999 inahitaji maboresho ili iendane na mabadiliko yaliyopo katika sekta ya afya na mwelekeo wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.

“Tunataka sheria yetu iweze kuboreshwa ili iwezeshe watu wengi zaidi kujiunga na pia kuziba mianya ya matumizi mabaya ya kadi yanayofanywa na baadhi ya wanachama wasio waaminifu” amesema.

Amesema marekebisho hayo yanatarajiwa kuongeza idadi ya wanachama, kuimarisha uendelevu wa Mfuko na kuweka mifumo madhubuti zaidi ya kudhibiti udanganyifu na matumizi yasiyofaa ya huduma za bima ya afya.

Kuzingatia Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mwenda Tulalemwa, amesema marekebisho ya sheria yanapaswa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya wananchi pamoja na kuendana na Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, ili kuhakikisha hakuna mgongano wa kisheria.

Amesema wadau waliotoa maoni wamependekeza maboresho katika maeneo mbalimbali, ikiwemo mfumo wa malipo kwa vituo vya kutolea huduma za afya, huduma kwa watu wasio na uwezo na watu wenye ulemavu.

Aidha, miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa ni kuongeza umri wa watoto wanaotambuliwa k**a wategemezi kutoka miaka 21 hadi 25, hatua inayolenga kuendana na mahitaji ya familia na mazingira ya sasa.
Naye Wakili wa Mahak**a Kuu na mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Ferdinand Makole, amesema marekebisho ya sher

*USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF  WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI*Na Mwandishi Wetu, DodomaKamati ya Bajet...
28/08/2026

*USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI*

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kazi kubwa inayofanya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za bima ya afya nchini, pamoja na ushirikiano wake na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF).

Pongezi hizo zimetolewa leo, Agosti 26, 2026, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mariam Hamis Said, wakati Kamati hiyo pamoja na Menejimenti za ZHSF na NHIF ilipotembelea Makao Makuu ya NHIF kwa ajili ya kujifunza namna Mfuko huo unavyoendesha na kutoa huduma kwa wanachama.

Mhe. Mariam amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuwa Kamati imepata fursa ya kuelezwa na kujionea kwa vitendo mifumo na huduma zinazotolewa na NHIF, kupitia ziara kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Pamoja na kutoa pongezi kwa NHIF, Kamati hiyo ilipata fursa ya kutaka kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya Mfuko, ikiwemo namna NHIF inavyopambana na udanganyifu, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.

Aidha, Kamati ilitaka kufahamu namna matumizi ya TEHAMA yameboresha utendaji wa NHIF na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji, pamoja na namna uwekezaji unavyosaidia kuimarisha Mfuko.

Masuala mengine yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na vyanzo vya mapato ya Mfuko, viashiria vinavyotumika kupima mafanikio na uendelevu wa NHIF, pamoja na mafunzo na uzoefu ambao Mfuko umeupata katika kipindi cha miaka 25 ya utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema ushirikiano kati ya NHIF na ZHSF umeleta matokeo makubwa katika hatua mbalimbali za uanzishaji na uendelezaji wa ZHSF, huku akieleza kuwa uzoefu na msaada uliotolewa na NHIF umeiwezesha Zanzibar kuanza na kuendelea vizuri katika safari ya kuimarisha huduma za bima ya afya.

“Kamati inapongeza NHIF na ZHSF kwa mashirikiano makubwa wanayoyafanya ambayo yamewezesha ZHSF kuanza na kuendelea vizuri,” amesema Mhe. Mariam.

Dkt. Isaka amesema NHIF itaendelea kutoa ushirikiano una

USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF  WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHINa Mwandishi Wetu, DodomaKamati ya Bajeti ...
28/08/2026

USHIRIKIANO WA NHIF NA ZHSF WAVUTIA KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kazi kubwa inayofanya katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za bima ya afya nchini, pamoja na ushirikiano wake na Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF).

Pongezi hizo zimetolewa leo, Agosti 26, 2026, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mariam Hamis Said, wakati Kamati hiyo pamoja na Menejimenti za ZHSF na NHIF ilipotembelea Makao Makuu ya NHIF kwa ajili ya kujifunza namna Mfuko huo unavyoendesha na kutoa huduma kwa wanachama.

Mhe. Mariam amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuwa Kamati imepata fursa ya kuelezwa na kujionea kwa vitendo mifumo na huduma zinazotolewa na NHIF, kupitia ziara kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Pamoja na kutoa pongezi kwa NHIF, Kamati hiyo ilipata fursa ya kutaka kufahamu kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya Mfuko, ikiwemo namna NHIF inavyopambana na udanganyifu, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, pamoja na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.

Aidha, Kamati ilitaka kufahamu namna matumizi ya TEHAMA yameboresha utendaji wa NHIF na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji, pamoja na namna uwekezaji unavyosaidia kuimarisha Mfuko.

Masuala mengine yaliyotiliwa mkazo ni pamoja na vyanzo vya mapato ya Mfuko, viashiria vinavyotumika kupima mafanikio na uendelevu wa NHIF, pamoja na mafunzo na uzoefu ambao Mfuko umeupata katika kipindi cha miaka 25 ya utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema ushirikiano kati ya NHIF na ZHSF umeleta matokeo makubwa katika hatua mbalimbali za uanzishaji na uendelezaji wa ZHSF, huku akieleza kuwa uzoefu na msaada uliotolewa na NHIF umeiwezesha Zanzibar kuanza na kuendelea vizuri katika safari ya kuimarisha huduma za bima ya afya.

“Kamati inapongeza NHIF na ZHSF kwa mashirikiano makubwa wanayoyafanya ambayo yamewezesha ZHSF kuanza na kuendelea vizuri,” amesema Mhe. Mariam.

Ameongeza kuwa kazi iliyofanywa na NHIF katika kusaidia uanzishaji wa ZHSF ilihitaji uvumilivu na kujitolea kwa kiwango kikubwa, akieleza kuwa Zanzibar imenufaika na uzoefu wa NHIF katika kujenga mfumo wa bima ya afya.

“Kazi iliyofanywa na NHIF ni kazi iliyofanyika kwa uvumilivu mkubwa, lakini kwa kutubeba Zanzibar katika uanzishaji wa Mfuko wetu,” amesema.

Aidha, Mhe. Mariam ameipongeza Menejimenti ya NHIF kwa kuwawezesha kutembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambako wamejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa.

Amesema ziara hiyo imewapa fursa ya kuona kwa vitendo ubora wa huduma zinazotolewa, hususan huduma za kibingwa na kibingwa bobezi, ambayo ni mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumejionea namna wanachama wa NHIF wanavyopokelewa na kuhudumiwa. Hakika kazi hii ni kubwa na nzuri ambayo kwa ujumla tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo huduma za kibingwa na kibingwa bobezi zinapatikana hapa nchini,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, amesema Mfuko utaendelea kushirikiana kwa karibu na ZHSF ili kuhakikisha wananchi na wanachama wanapata huduma bora za afya kwa wakati na kwa ufanisi.

Dkt. Isaka amesema NHIF itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa ZHSF, hususan katika maeneo ya uzoefu, mifumo ya utoaji huduma na masuala mengine ya kitaalamu, kwa lengo la kuimarisha huduma za bima ya afya kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema ushirikiano huo ni sehemu ya dhamira ya NHIF ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wananchi popote walipo nchini, huku mifuko hiyo ikiendelea kujifunza na kubadilishana uzoefu katika kuboresha huduma kwa wanachama.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya taasisi zinazohusika na utoaji wa huduma za bima ya afya Tanzania Bara na Zanzibar.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!

Bima ya afya kwa Wote, Jiunge Sasa! Wizara Ya Afya Msemaji Mkuu wa Serikali Bima ya Afya kwa Wote
26/08/2026

Bima ya afya kwa Wote, Jiunge Sasa!

Wizara Ya Afya Msemaji Mkuu wa Serikali Bima ya Afya kwa Wote

NHIF DODOMA YAONGEZA KASI YA UHAMASISHAJI WA BIMA YA AFYA KWA WANANCHIDodoma;Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NH...
25/08/2026

NHIF DODOMA YAONGEZA KASI YA UHAMASISHAJI WA BIMA YA AFYA KWA WANANCHI

Dodoma;

Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Dodoma imeendelea na kampeni za uhamasishaji na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi katika makundi mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza idadi ya Watanzania wanaonufaika na huduma za afya kupitia bima ya afya. Kampeni hizo zinalenga kuwafikia wananchi moja kwa moja, hususan wanaojishughulisha na shughuli za sekta isiyo rasmi.

Katika kutekeleza kampeni hiyo, Ofisi ya NHIF Dodoma imeanza na maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya wananchi, ikiwemo masoko, ambapo siku ya Jumamosi, tarehe 22 Agosti 2026, ilifanya uhamasishaji katika Soko la Mnadani Msalato jijini Dodoma. Wananchi na wafanyabiashara walipata elimu kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya, huduma zinazotolewa na NHIF pamoja na namna ya kujiunga na bima.

Meneja wa NHIF Mkoa wa Dodoma Bi. Irene Kataraihya ameeleza kuwa Ofisi ya NHIF Dodoma itaendelea na kampeni hizo katika maeneo mbalimbali ili kuwafikia wananchi wengi zaidi, kutoa elimu sahihi na kuwahamasisha kuchukua hatua ya kujiunga na bima ya afya. Jitihada hizi ni sehemu ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, wenye lengo la kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma bora za afya bila kikwazo cha gharama.

Bima ya Afya kwa Wote, Jiunge Sasa!

Address

NATIONAL HEALTH INSURANCE FUND
Dodoma
P.OBOX1437

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 07:30 - 16:00
Wednesday 07:30 - 16:00
Thursday 07:30 - 16:00
Friday 07:30 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when National Health Insurance Fund posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to National Health Insurance Fund:

Shortcuts

Share