Geological Survey of Tanzania

Geological Survey of Tanzania The GST is a Government Institution established under the Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, No. 7 of 2017. It is under the Ministry of Minerals

The government executive agency under the ministry of Energy and Minerals entrusted in collecting, analyzing, archieving and disseminating national geo-scientific data and information

29/08/2026
07/08/2026

GST kufanya tafiti zaidi ili kuwezesha kufikiwa kwa Dira 2050

GST KUONGEZA KASI YA UTAFITI WA MADINI KUFANIKISHA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050📍DodomaTaasisi ya Jiolojia na Utafiti ...
06/08/2026

GST KUONGEZA KASI YA UTAFITI WA MADINI KUFANIKISHA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

📍Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeeleza kuwa inaongeza kasi ya kufanya tafiti za jiosayansi nchini ili kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini, kuongeza ajira, mapato ya Serikali na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa GST, Mha. Ally Samaje, amesema taasisi hiyo ndiyo msingi wa mnyororo mzima wa sekta ya madini kwa kuwa hukusanya, kuchakata, kuhifadhi na kusambaza taarifa muhimu za jiosayansi kwa wawekezaji na wadau wengine.

Amesema hadi sasa GST imekamilisha utafiti wa jiolojia kwa asilimia 98 ya eneo lote la Tanzania, huku utafiti wa jiofizikia wa skeli ndogo (low resolution airborne geophysical survey) ukifikia asilimia 100. Hatua hiyo imeendelea kuwapa wawekezaji taarifa za awali zinazowawezesha kutambua maeneo yenye fursa za madini na kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji.

Kwa upande wa utafiti wa jiofizikia wa kina (High Resolution Airborne Geophysical Survey), Mha. Samaje amesema umefikia asilimia 16 ya eneo la nchi. Hata hivyo, maandalizi ya kuongeza kiwango hicho yanaendelea kupitia programu mpya ya urushaji ndege katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Amefafanua kuwa awamu ya kwanza ya programu hiyo itahusisha utafiti katika eneo linalokadiriwa kuwa asilimia 18 ya ukubwa wa Tanzania, hatua itakayoongeza kiwango cha utafiti huo hadi asilimia 34 baada ya kukamilika. Amesema mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo tayari amepatikana.

Aidha, amesema awamu inayofuata itafanyika katika eneo la katikati ya Tanzania lenye ukubwa wa takribani asilimia 19 ya nchi, jambo litakalowezesha kufikia zaidi ya asilimia 50 ya utafiti wa kina wa jiofizikia, lengo ambalo Serikali imejiwekea kulifikia kabla ya mwaka 2030.

Akizungumzia utafiti wa jiokemia, Mha. Samaje amesema GST imefikia asilimia 24 ya eneo la nchi, na katika mwaka huu wa fedha taasisi itafanya tafiti katika maeneo mapya 18 ili kuongeza kiwango hicho hadi asilimia 30.

Ameeleza kuwa maeneo mengi yatakayofanyiwa utafiti yamechaguliwa kutokana na uwepo wa wachimbaji wadogo, ambapo taarifa zitakazopatikana zitawawezesha kufanya uchimbaji kwa uhakika badala ya kubahatisha, kuongeza uzalishaji, kuboresha kipato na kupunguza hasara za kuwekeza bila kuwa na taarifa za jiosayansi.

Kwa mujibu wa Mha. Samaje, taarifa hizo pia zitawasaidia wachimbaji wadogo kupata mikopo kutoka taasisi za fedha, huku GST ikiwa tayari imethibitisha matokeo ya tafiti zake ili kuongeza imani ya taasisi hizo kwa wachimbaji.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa programu hizo unawezeshwa na Mfuko wa Utafiti wa Madini unaofadhiliwa na Serikali kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya Sekta ya Madini kwa ajili ya kuzielekeza kwenye kufanya tafiti za madini nchini.

"Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuanzishwa kwa mfuko huo ambao utawezesha kuongeza kasi ya kufanya tafiti za madini nchini" aliongeza Mha. Samaje.

Amesisitiza kuwa upatikanaji wa taarifa sahihi za kijiosayansi utapunguza hatari kwa wawekezaji, kuongeza uwekezaji katika utafiti na uchimbaji wa madini, kuchochea uanzishaji wa migodi mipya, kuimarisha viwanda vinavyotumia madini k**a malighafi na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa taifa, hatua itakayosaidia kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

05/08/2026

"Nawasihi wachimbaji na wadau wote wa sekta ya madini kuwatumia wataalamu wa GST kupata taarifa sahihi za jiolojia kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji." — Bi. Neema Morice Mhagama.

04/08/2026

Madini ni Sayansi, Tajirika na GST.
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania (GST) itakuongoza katika shughuli zako za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini ili kuongeza uzalishaji.

GST Yahimiza Wachimbaji Wadogo kufanya tafiti katika shughuli zao za utafutaji na uchimbaji madini.📍DodomaWachimbaji wad...
04/08/2026

GST Yahimiza Wachimbaji Wadogo kufanya tafiti katika shughuli zao za utafutaji na uchimbaji madini.

📍Dodoma

Wachimbaji wadogo wa madini nchini wamehimizwa kuachana na uchimbaji wa kubahatisha na badala yake kutumia mbinu za kisayansi kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), ili kuongeza tija, kupunguza hasara na kuboresha matokeo ya shughuli zao za uchimbaji.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa GST, CPA. Timotheo Mbulla wakati alipotembelea banda la GST katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Malecela jijini Dodoma.

Mbulla amesema kuwa ni wakati muafaka kwa wachimbaji wadogo na wadau wengine wa sekta ya madini kuitumia GST k**a mshirika wao mkuu katika shughuli za utafiti na uchunguzi wa madini.

"Madini ni sayansi, na sayansi hii inaanzia porini ambako wataalamu wetu hufanya shughuli za utafiti wa madini. Baada ya hapo, sampuli hukusanywa na kuletwa katika maabara za GST kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini madini yaliyopo na kiwango chake," amesema Mbulla.

Ameeleza kuwa matokeo ya tafiti hizo zinazofanywa na GST huwasaidia wachimbaji kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuanza uchimbaji, hivyo kuongeza uwezekano wa kupata matokeo yenye tija na kupunguza gharama zinazotokana na uchimbaji usiozingatia tafiti za kisayansi.

Sambamba na hilo, amewahimiza wadau wa sekta ya madini pamoja na maabara zinazofanya uchunguzi wa sampuli za madini kutumia vyungu vya uchunguzi wa dhahabu (crucibles) vinavyozalishwa na GST.

Amesema vyungu hivyo vimetengenezwa na wataalamu wa ndani, vina ubora unaokidhi viwango vya kitaalamu na vina uwezo mkubwa wa kutumika katika shughuli za uyeyushaji wa madini kwa ufanisi wa hali ya juu.

Amesisitiza kuwa GST ndiyo taasisi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inayozalisha vyungu hivyo, ambavyo vinachangia kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi huku vikiongeza thamani ya teknolojia na ubunifu wa ndani.

Kwa upande wake, Meneja wa Fedha na Uhasibu wa GST, CPA Simon M***a, amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Taasisi katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma na majukumu yake.

Amesema utoaji wa elimu hiyo unaongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma za GST, jambo linalowezesha wachimbaji na wadau wengine wa sekta ya madini kuzitumia ipasavyo kwa maendeleo yao binafsi na kwa ustawi wa sekta ya madini na uchumi wa taifa kwa ujumla.

GST Yashiriki Jukwaa la LCCF 2026, Yaonesha Fursa za Utafiti na Huduma za Madini📍MwanzaTaasisi ya Jiolojia na Utafiti wa...
22/07/2026

GST Yashiriki Jukwaa la LCCF 2026, Yaonesha Fursa za Utafiti na Huduma za Madini

📍Mwanza

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki Jukwaa la Tano la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (Local Content Compliance Forum - LCCF 2026), linalofanyika katika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza kuanzia Julai 22 hadi 24, 2026.

Jukwaa hilo, ambalo limefunguliwa rasmi na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, linawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo wa thamani wa madini, kukuza biashara za ndani na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma, sekta binafsi na wawekezaji.

Katika maonesho yanayoambatana na jukwaa hilo, GST inaendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu huduma zake mbalimbali ikiwemo utafiti wa jiolojia, uchunguzi wa madini, huduma za maabara na taarifa za kijiolojia zinazowawezesha wawekezaji na wachimbaji kufanya maamuzi sahihi katika shughuli za utafutaji na maendeleo ya miradi ya madini.

Ushiriki wa GST katika LCCF 2026 unadhihirisha dhamira ya taasisi hiyo ya kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini katika kuimarisha matumizi ya tafiti za kisayansi, kuongeza thamani ya rasilimali madini na kuchochea maendeleo endelevu ya sekta hiyo kwa manufaa ya Watanzania.

GST Yahimiza Wachimbaji Kutumia Maabara Kuongeza Tija ya Madini.📍Dar es salaam.Wadau wanaojihusisha na shughuli za utafu...
07/07/2026

GST Yahimiza Wachimbaji Kutumia Maabara Kuongeza Tija ya Madini.

📍Dar es salaam.

Wadau wanaojihusisha na shughuli za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini wamehimizwa kutumia huduma za Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuongeza tija, kupunguza gharama zisizo za lazima na kuboresha uzalishaji wa madini.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkemia wa Maabara ya GST, Bi. Delphina Alex, kwa wadau waliotembelea banda la GST katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Bi. Delphina amesema wachimbaji wanapaswa kufanya uchunguzi wa sampuli za udongo, miamba na madini katika kila hatua ya mnyororo wa shughuli za madini kuanzia utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji hadi biashara ya madini. Alieleza kuwa hatua hiyo huwasaidia kufahamu aina na kiwango cha madini kilichopo, hivyo kufanya maamuzi sahihi kuhusu kuendelea au kusitisha shughuli za uchimbaji kulingana na matokeo ya uchunguzi.

Amebainisha kuwa baadhi ya wachimbaji wadogo huendelea na uchimbaji bila kupeleka sampuli maabara, jambo linaloweza kusababisha upotevu wa muda, rasilimali na kufanya kazi bila tija kutokana na kutofahamu kiwango halisi cha madini kilichopo katika eneo husika.

Aidha, Bi. Delphina ameeleza kuwa uchunguzi wa maabara husaidia kubaini tabia ya mwamba unaobeba madini, jambo linalomwezesha mchimbaji kuchagua njia sahihi ya kusaga, kuchenjua na kuvuna madini kwa ufanisi zaidi. Pia husaidia kufahamu aina na kiwango sahihi cha kemikali zinazohitajika katika mchakato wa uchenjuaji, hivyo kuongeza ufanisi wa uzalishaji.

Amesisitiza kuwa wachimbaji, hususan wachimbaji wadogo, wanapaswa kupeleka sampuli zao maabara katika kila hatua ya shughuli zao ili kuongeza tija, kuboresha uzalishaji na kufanya biashara ya madini kwa kuzingatia taarifa sahihi za kitaalamu.

Kwa upande wa ubora wa huduma, Bi. Delphina amesema Maabara ya GST ina vifaa vya kisasa, wataalamu wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu pamoja na ithibati ya kimataifa, hivyo majibu yake yanatambulika na kukubalika popote duniani. Alitoa wito kwa wadau wote wa Sekta ya Madini kutumia huduma za maabara hiyo ili kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa ufanisi na matokeo yenye tija

Address

903, Kikuyu Avenue
Dodoma
903

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255262323020

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Geological Survey of Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Geological Survey of Tanzania:

Shortcuts

Share