01/06/2026
VIJANA WAHIMIZWA KUWA WAZALENDO NA KUTUMIA FURSA ZA MAENDELEO
Vijana wa Wilaya ya Bahi wamehimizwa kuwa wazalendo, kulinda amani na kutumia fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa
Wito huo umetolewa leo tarehe 1 Juni 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wakati wa Kongamano la Vijana na Uzinduzi wa Jukwaa la Vijana (Youth Platform) la Wilaya ya Bahi, lililowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo lililobeba kaulimbiu isemayo "Vijana Tuyajenge, Tanzania ni Yetu Sote", sambamba na kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru ya mwaka 2026 isemayo "Tanzania ni Yetu Sote, Tushik**ane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo"
Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Jane Ng'ondi, amewataka Vijana kuzingatia Maadili ya Taifa, kuunda vikundi, kujisajili na kuanzisha miradi mbalimbali ili kunufaika na fursa zinazotolewa na Serikali
"Vijana ni kioo cha taifa letu, tujiepushe na vurugu kwani vurugu zinaharibu amani yetu , tulinde amani ya nchi yetu na tuwe wazalendo," alisema Bi. Ng'ondi
Aidha, Bw. Omari Abdullah Pumzi kutoka k**ati ya Vijana Wazalendo, alipokuwa akifafanua kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, amewahimiza vijana kutumia Tekinolojia na mitandao ya kijamii kutafuta taarifa na fursa mbalimbali za maendeleo
"Wizara zote zinatutegemea sisi vijana Usigombane na watu wewe ng'ang'ania fursa, Fursa haikufuati nyumbani; ifuate mtandaoni, katika ofisi za maendeleo ya jamii na sehemu nyingine zinazotoa huduma za maendeleo," alisema Punai
Lengo la kongamano hilo lilikuwa kuchagua viongozi wa Jukwaa la Vijana la Wilaya ya Bahi na kuwawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo katika halmashauri likiambatana na mafunzo kuhusu elimu ya uraia na uzalendo, ujasiriamali, usimamizi wa biashara, elimu ya fedha, upatikanaji wa mikopo na fursa za uwezeshaji wa vijana, pamoja na ushiriki wa vijana katika shughuli za maendelo
Mada hizo zimewasilishwa na wataalamu kutoka taasisi mbalimbali akiwemo Dkt. Samson Msilu, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Serikali za Mitaa; CPSP Scholastica Nyabweke kutoka Hombolo(lgti)