06/08/2026
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Agrey Mwanri, akizungumza wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma, amesema kuwa yuko tayari kutekeleza kwa moyo wote dhamana aliyoaminiwa na Chama.
Amesema viongozi wanapaswa kusimama imara katika kutekeleza majukumu yao kwa kujituma, uaminifu na uwajibikaji.
βTunanyanyuka kwenda kuitenda kazi tuliyoaminiwa nayo. K**a kazi zinaweza kuua, basi tutafia kazini,β amesema Ndugu Mwanri, akisisitiza dhamira yake na Viongozi wote kutekeleza majukumu aliyopewa.
______
CCMIpoKazini