Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga Ukurasa rasmi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga (Waga Wildlife Management Area)

VIJANA NA UHIFADHI WA MALIASILI  WAGA YAENDELEA KUJENGA UWEZO KWA  JAMIITarehe 31 Agosti na 01 Septemba 2026, timu ya wa...
02/09/2026

VIJANA NA UHIFADHI WA MALIASILI WAGA YAENDELEA KUJENGA UWEZO KWA JAMII

Tarehe 31 Agosti na 01 Septemba 2026, timu ya watumishi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, kwa kushirikiana na wataalamu wa wanyamapori kutoka Ofisi za Wakurugenzi wa Mbarali, Iringa na Mufindi, ilifanikiwa kufikisha vifaa vya michezo kwa vijana katika vijiji vya Kisilwa, Mahuninga na Ihanzutwa.

Katika zoezi hilo, jumla ya jezi 48 za mpira wa miguu na mipira 3 zilikabidhiwa kwa vijana, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwafikia, kuwajengea ushirikiano na kuwashirikisha vijana katika agenda ya uhifadhi wa maliasili na wanyamapori.

Michezo ni nyenzo muhimu ya kuwaunganisha vijana na Uhifadhi. Kupitia shughuli hizi, tunaamini vijana wanaweza kuwa sehemu muhimu ya kulinda na kuhifadhi rasilimali za wanyamapori kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Katika ziara hizo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga Bi. FATUMA MBEMBATI alitoa elimu kwa wananchi na vijana kuhusu umuhimu wa uhifadhi, pamoja na faida zinazotokana na uwepo wa Hifadhi ya Wanyamapori Waga.

Uhifadhi si jukumu la mtu mmoja — ni jukumu letu sote,Tukiwafikia vijana leo, tunajenga mabalozi wa uhifadhi wa kesho. Linda maliasili, linda maisha, linda kizazi kijacho

,
NaUhifadhi

VIJANA WAKIJIFUNZA, UHIFADHI UNAENDELEAMnamo tarehe 24 Agosti, wanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Sekondari Nya...
25/08/2026

VIJANA WAKIJIFUNZA, UHIFADHI UNAENDELEA

Mnamo tarehe 24 Agosti, wanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule ya Sekondari Nyamakuyu walitembelea katika ofisi ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa ajili ya kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na mazingira.

Katika ziara hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu: ,Tabia na mwenendo wa wanyamapori,Umuhimu wa kuhifadhi mazingira na misitu,Namna ya kutunza na kulinda rasilimali za asili,Wajibu wa jamii katika kuhakikisha uhifadhi endelevu

Ziara k**a hizi ni muhimu katika kuwajengea vijana uelewa na moyo wa kulinda wanyamapori, misitu na mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Uhifadhi ni jukumu letu sote.
, ,

Katika kutekeleza moja ya malengo ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa mwaka wa fedha 2026/2027, uongozi wa jum...
18/08/2026

Katika kutekeleza moja ya malengo ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga kwa mwaka wa fedha 2026/2027, uongozi wa jumuiya umejipanga kukarabati na kuboresha barabara yenye urefu usiozidi kilomita 8 kuanzia Nyakadete hadi mwanzoni mwa Mto Mhanga, uliopo katika Kitongoji cha Soligona, Kijiji cha Nyakadete.

Barabara hiyo imekuwa changamoto kubwa, hasa wakati wa msimu wa mvua, hali inayosababisha usumbufu kwa watumishi wa jumuiya, hususan askari wanyamapori, pamoja na wageni mbalimbali wanaoingia katika maeneo ya hifadhi kwa shughuli mbalimbali.

Aidha, barabara hiyo ni muhimu kwa wakulima wanaofanya shughuli zao katika maeneo hayo.

Kutokana na changamoto hiyo, mnamo Tarehe 17/08/2026 uongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga, ukiongozwa na Katibu wa Jumuiya, Ndugu John Samwel Mbulu, ulifanya mazungumzo na mdau Ndugu Luqman Merharabu, kwa lengo la kuomba ushirikiano na msaada katika ukarabati na uboreshaji wa barabara hiyo.

Tunamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kufanikisha jambo hili. Aidha, tunatoa shukrani za dhati kwa Ndugu Luqman Merharabu kwa kukubali kushirikiana na jumuiya katika kufanikisha ukarabati wa barabara hiyo.

Zoezi la ukarabati linatarajiwa kuanza wiki ijayo, mara baada ya kufanikisha upatikanaji wa vifaa muhimu vya ujenzi, ikiwemo katapila na greda,
Carbon tanzania
Ahsante

JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAGA KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2026 – MBEYAKuanzia tarehe 5–8,Aug 2026  mtaalam kuto...
10/08/2026

JUMUIYA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI WAGA KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2026 – MBEYA

Kuanzia tarehe 5–8,Aug 2026 mtaalam kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halimashauri ya Mufindi Bi rachelflowers0787055335 na Mhasibu wa jumuiya walishiriki Maonesho ya Nanenane jijini Mbeya, ambapo wataalam wetu walitoa elimu kwa wananchi na wageni mbalimbali kuhusu uhifadhi wa wanyamapori, faida za uhifadhi, ufugaji wa nyuki na ufugaji wa samaki.

Wanafunzi na wageni mbalimbali walipata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu WAGA WMA, shughuli tunazofanya na namna uhifadhi unavyoweza kwenda sambamba na maendeleo ya jamii.

Tuhifadhi leo, tunufaike leo na kulinda kesho

08/08/2026
Nyuma ya kila mnyama aliye salama, kuna shujaa anayelinda bila kuchokaSiku ya tarehe 31 Julai 2026 tulisherekea Siku ya ...
01/08/2026

Nyuma ya kila mnyama aliye salama, kuna shujaa anayelinda bila kuchoka

Siku ya tarehe 31 Julai 2026 tulisherekea Siku ya Rangers Duniani pamoja na wanajamii, askari wa uhifadhi na uongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA.

Maadhimisho haya yalipambwa na michezo mbalimbali iliyounganisha wadau wote, kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu za wanyamapori.

Tunatoa pongezi na shukrani kwa Rangers wote kwa kujitolea, ujasiri na kazi kubwa wanayoifanya kila siku katika kulinda urithi wetu wa asili. Kwa pamoja, tunaendelea kujenga jamii inayothamini na kushiriki kikamilifu katika uhifadhi. Uhifadhi ni jukumu letu sote.
SarahRehner foundation, ,
Conservation ProtectWildlife

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga (WAGA) imeendelea kuonesha dhamira yake katika kuimarisha uhifadhi shirikishi kwa...
18/07/2026

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga (WAGA) imeendelea kuonesha dhamira yake katika kuimarisha uhifadhi shirikishi kwa kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori Tanzania Chantal uliofanyika jijini Dodoma kuanzia tarehe 13–15 Julai.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi kutoka mashirika mbalimbali na menejimenti za Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori kutoka maeneo mbalimbali nchini kujadili masuala ya kimkakati yanayolenga kuimarisha utendaji wa Jumuiya, kuongeza ushawishi wa kisera, na kuboresha usimamizi endelevu wa rasilimali za wanyamapori.
Katika mkutano huo, wajumbe walijadili na kupitisha Katiba ya CWMAC, pamoja na Mpango Kazi wa Muungano wa mwaka 2026/2027 ,ambao utaongoza utekelezaji wa shughuli za Muungano katika kipindi kijacho. Aidha, mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa, zikiwemo usimamizi wa mitandao ya kijamii, uwezeshaji wa wanawake na vijana, pamoja na mikakati ya kuongeza manufaa ya uhifadhi kwa jamii.

WAGA itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuendeleza uhifadhi shirikishi wa wanyamapori, kulinda rasilimali za asili na kuhakikisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi zinaendelea kunufaika na uhifadhi .
, Carbon Project Developer

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga (WAGA) imeendelea kuonesha dhamira yake katika kuimarisha uhifadhi shirikishi kwa kushiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori Tanzania (CWMAC) uliofanyika jijini Dodoma kuanzia tarehe 13–15 Julai.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi na menejimenti za Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori kutoka maeneo mbalimbali nchini kujadili masuala ya kimkakati yanayolenga kuimarisha utendaji wa Jumuiya, kuongeza ushawishi wa kisera, na kuboresha usimamizi endelevu wa rasilimali za wanyamapori.
Katika mkutano huo, wajumbe walijadili na kupitisha Katiba ya CWMAC, pamoja na Mpango Kazi wa Muungano wa mwaka 2026/2027 ,ambao utaongoza utekelezaji wa shughuli za Muungano katika kipindi kijacho. Aidha, mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa, zikiwemo usimamizi wa mitandao ya kijamii, uwezeshaji wa wanawake na vijana, pamoja na mikakati ya kuongeza manufaa ya uhifadhi kwa j

Kuanzia tarehe  06–09, Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA ilifanya kikao cha Baraza la Robo ya Nne kwa mwaka wa fedh...
09/07/2026

Kuanzia tarehe 06–09, Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA ilifanya kikao cha Baraza la Robo ya Nne kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kilichowakutanisha wajumbe wa Baraza, wataalamu, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), pamoja na wawekezaji.
Miongoni mwa ajenda kuu ilikuwa ni uwasilishaji wa rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, ambapo wadau walitoa maoni na mapendekezo yenye lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya. Aidha, walisisitiza umuhimu wa Menejimenti ya WAGA kuendelea kubuni na kuendeleza vyanzo mbadala vya mapato kupitia shughuli za kiuchumi na uhifadhi, ikiwemo ufugaji wa nyuki, ufugaji wa samaki, pamoja na kuimarisha ulinzi na usimamizi endelevu wa rasilimali za maliasili.
Vilevile, Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Jumuiya, ambapo wajumbe walipongeza mafanikio yaliyopatikana, huku wakitoa ushauri na maoni ya kujenga kuhusu changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali, wakiwemo Honeyguide Foundation,Rural Development Organization (RDO), Six Rovers Africa,Wembere Hunting Safaris, pamoja na wataalamu kutoka Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Mbarali, Iringa na Mufindi. Ushiriki wao umeendelea kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa maliasili na maendeleo ya jamii.
Pamoja tunajenga uhifadhi endelevu wenye manufaa kwa jamii na vizazi vijavyo.

PONGEZI KWA VIJANA WA KIJIJI CHA NYAKADETEJumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inawapongeza vijana wa Kijiji cha Nyaka...
29/06/2026

PONGEZI KWA VIJANA WA KIJIJI CHA NYAKADETE

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inawapongeza vijana wa Kijiji cha Nyakadete, mwanachama wa WAGA, kwa ubunifu na uzalendo walioonesha kwa kutumia nembo ya WAGA kwenye bendera yao wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo.

Kitendo hiki kinaonesha jinsi vijana wanavyoitambua na kuithamini WAGA k**a chombo muhimu katika kuhamasisha uhifadhi, maendeleo na mshik**ano wa jamii.

Hafla ya ufunguzi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, huku mgeni rasmi akiwa Katibu wa Jumuiya Mhe. John Mbulu, ambaye alizindua rasmi mashindano hayo. Uwepo wake uliheshimisha hafla na kuwatia moyo vijana kushiriki kikamilifu katika michezo na shughuli za maendeleo.

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inawapongeza vijana wa Nyakadete kwa ubunifu wao na kuwatakia washiriki wote mashindano yenye ushindani wa haki, umoja, amani na mafanikio.
, ,

Address

Iringa
P.O.BOX223,MAFINGA-MUFINDI

Opening Hours

Monday 08:30 - 17:00
Tuesday 08:30 - 17:00
Wednesday 08:30 - 17:00
Thursday 08:30 - 17:00
Friday 08:30 - 17:00
Saturday 08:30 - 17:00
Sunday 08:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga:

Shortcuts

Share