Kalambo TV

Kalambo TV Kalambo TV ni jukwaa huru la habari, mijadala na sauti za wananchi. Hakikisha una Follow kwa habari zaidi tembelea πŸ‘‡
www.mbungekalambo.com

Tunakuletea ukweli, matukio na maoni kutoka kwa jamii kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha maendeleo.

27/08/2026

MHE. MBUNGE KANONI AIBANA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA AFYA KASANGA

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIAOfisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, k...
26/08/2026

NAFASI 200 ZA AJIRA ZA MAFUNDI ZATANGAZWA KWA KAZI NCHINI SAUDI ARABIA

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, kwa kushirikiana na Atilis Investment Limited, inawataarifu Watanzania wenye sifa stahiki kuhusu nafasi 200 za ajira za mafundi katika sekta ya ujenzi, zilizotolewa na kampuni ya Shade Corporation Limited ya nchini Saudi Arabia.

Kwa maelezo zaidi tembelea www.mbungekalambo.com

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA POLE KWA KIFO CHA KIJANA BARACKA LEONARD MSILIOfisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo...
25/08/2026

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA KALAMBO YATOA POLE KWA KIFO CHA KIJANA BARACKA LEONARD MSILI

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha kijana Baracka Leonard Msili, mkazi wa Santamaria, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa, kilichotokea katika eneo hilo.
Katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni anatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa.

Soma zaidi www.mbungekalambo.com

MHE. KANONI ATOA SALAMU ZA MAULIDI, AWASIHI WANAKALAMBO NA WATANZANIA KUDUMISHA AMANIMhe. Edefonsi Joackim Kanoni, Mbung...
25/08/2026

MHE. KANONI ATOA SALAMU ZA MAULIDI, AWASIHI WANAKALAMBO NA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, amewatakia Wanakalambo na Watanzania wote, hususan Waislamu, Maulidi njema yenye furaha, upendo, mshik**ano na amani.

Katika salamu zake za Maulidi, Mhe. Kanoni amesema sikukuu k**a hii ni wakati muhimu wa kutafakari na kujikumbusha kumrudia Muumba wetu, kuishi kwa kufuata mafundisho mema, kutenda mema, kusaidiana na kuwa na upendo na huruma kwa wengine.

Kusoma zaidi tembelea www.mbungekalambo.com

TAARIFA KWA WANANCHI WA JIMBO LA KALAMBO KUHUSU KERO YA BARABARAKuhusu Fedha za Matengenezo ya Barabara, Mikataba ya Wak...
24/08/2026

TAARIFA KWA WANANCHI WA JIMBO LA KALAMBO KUHUSU KERO YA BARABARA

Kuhusu Fedha za Matengenezo ya Barabara, Mikataba ya Wakandarasi na Hatua Zinazochukuliwa Katika Utekelezaji
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inapenda kuwashukuru wananchi wote wa Jimbo la Kalambo kwa kuendelea kutoa maoni, ushauri na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao, hususan changamoto ya barabara.
Ofisi ya Mbunge inatambua kwa kina umuhimu wa barabara katika kuchochea maendeleo ya wananchi, kurahisisha usafirishaji wa mazao, huduma za afya, elimu, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

Kusoma habari zaidi tembelea
www.mbungekalambo.com

22/08/2026

Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), Rufiji, Pwani

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwezesha kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa Taifa letu. Hii ni hatua ya kujivunia katika safari yetu ya kuendelea kufanya kazi ya kujikomboa kiuchumi, ili kuiishi maana halisi ya Uhuru wetu, pamoja na malengo na ndoto za waasisi wetu.

Hongera kwa kila Mtanzania.

TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA AWAMU YA PILIKatika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya M...
22/08/2026

TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA AWAMU YA PILI

Katika kutekeleza ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa vijana ndani ya siku 100 baada ya kuingia madarakani, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inautangazia umma kuanza kwa Awamu ya Pili ya utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana.

Malengo ya mikopo hiyo ni kuwawezesha vijana kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza biashara ndogo, biashara za kati na kampuni changa ili kujijengea kipato katika Sekta za Mifugo na Uvuvi.
Kupata habari kamili tembelea tovuti www.mbungekalambo.com

OFISI YA MBUNGE KANONI YATOA POLE, YALAANI VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI MADIBILAOfisi ya Mbunge wa Jimbo la K...
22/08/2026

OFISI YA MBUNGE KANONI YATOA POLE, YALAANI VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI MADIBILA

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Mhe. Edefonsi Joackim Kanoni, inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote walioguswa na kifo cha marehemu Daudy Amosi Mwimazi, aliyepoteza maisha katika tukio lililotokea katika Kijiji cha Madibila, Kata ya Mambwekenya, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa.

Kwa taarifa kamili tembelea tovuti ya www.mbungekalambo.com

21/08/2026

MAMBO MAKUBWA YA ELIMU YALIYOFANYWA NA MHE. KANONI KALAMBO
KALAMBO: Katika kipindi cha uongozi wake, Mhe. Edefonce Joackim Kanoni, Mbunge wa Jimbo la Kalambo, ameendelea kuweka msukumo katika kuboresha sekta ya elimu kwa kuwasilisha changamoto za wananchi Serikalini na kufuatilia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miundombinu ya shule.

Kusoma habari hii na nyingine nyingi zinazo husu jimbo la Kalambo tembelea www.mbungekalambo.com

20/08/2026

MHE. MBUNGE KANONI AKEMEA VITENDO VYA BAADHI YA WANANCHI KUUZA ARDHI

Address

Matai
Kalambo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kalambo TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share