Nipige TAFU

Nipige  TAFU Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Nipige TAFU, Social service, Umoja, Kasulu.

Ukurasa rasmi wa kikundi jamii chenye usajili namba
KSTC/CBO/1024
(Community Base Organization)
Call/SMS:+255762223499
WhatsApp:+255762223499
Email:[email protected]
Area:Kasulu Kigoma Tz🇹🇿
TUNAGUSWA TUNASAIDIA
🚫

02/08/2026

Ujumbe kutoka NIPIGE TAFU GROUP KASULU wa Leo tarehe 02 AUGUST 2026

23/07/2026

TAASISI YA NIPIGE TAFU GROUP YASHIRIKI KIKAO CHA JUKWAA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs) WILAYA YA KASULU

Taasisi ya Nipige Tafu Group ni miongoni mwa mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoshiriki katika Kikao cha Pili cha Robo ya Mwaka cha Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Wilaya ya Kasulu, kilichowakutanisha mashirika 43 kujadili utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika kwa ushirikiano na Serikali katika kipindi cha Machi hadi Juni, 2026.

Katika kikao hicho, mashirika yasiyo ya kiserikali yameaswa kuanzisha vyanzo vya mapato vya ndani vitakavyowezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo, badala ya kutegemea wafadhili pekee. Hatua hiyo imelenga kuimarisha uendelevu wa taasisi na kuongeza uwezo wake wa kutoa huduma kwa jamii.

Mgeni Rasmi wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Ndugu Isack Mwakisu, ambapo alisisitiza umuhimu wa mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali, kutekeleza afua za maendeleo kwa uwajibikaji, pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati.

Nipige Tafu Group inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii kupitia huduma, elimu, uwezeshaji na shughuli nyingine zenye manufaa kwa wananchi.

"TUNAGUSWA, TUNASAIDIA."

14/07/2026

🌍When your partner is in trouble, what benefit do you get?

Mwenzako anapopata shida wewe unapata faida gani?

26/06/2026

WATU NI WALE WALE PEOPLE ARE THE ONES

21/06/2026
16/06/2026

1.Leo, 16 Juni 2026, tunaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kusimama kwa ajili ya haki, elimu, ulinzi na ndoto za kila mtoto. Mtoto wa Afrika anastahili kusikilizwa, kuthaminiwa na kupewa nafasi ya kung’aa.Kila mtoto wa Afrika ana ndoto, ana sauti, na anastahili kulindwa, kupendwa, na kupewa nafasi ya kufikia kesho iliyo bora. Tusiwaone tu k**a watoto wa leo, bali viongozi wa kesho.


katilihaendimbinguni

2.Today, 16 June 2026, we celebrate the Day of the African Child by standing up for the rights, education, protection and dreams of every child. The African child deserves to be heard, valued and given a chance to shine. Every African child has a dream, a voice, and deserves to be protected, loved and given a chance to achieve a better tomorrow. Let us not just see them as the children of today, but the leaders of tomorrow.

DayOfTheAfricanChild AfricanChild ChildrenRights EducationForChildren
katilihanendimbinguni

09/06/2026

1.Tunawaomba maafisa usafirishaji (boda boda) kuacha tabia ya kuwapelekea chipsi wanafunzi wa k**e kwa nia ya kuwashawishi au kuwatega kwa malengo mabaya. Watoto ni kundi linalostahili kulindwa, kuheshimiwa na kupewa mazingira salama ya kujifunza. Tushirikiane kupinga vitendo vyote vinavyoweza kusababisha ukatili, unyanyasaji na uharibifu wa maisha yao ya baadaye.

2.We request transport officers (boda boda) to stop the practice of delivering sweets to female students with the intention of tempting them or ensnaring them for nefarious purposes. Children are a group that deserves to be protected, respected and given a safe learning environment. Let us work together to oppose all actions that can lead to violence, abuse and the destruction of their future lives.

1.Wa tatu kutoka kushoto kwa walio simama ni mwanachama na mlezi na.2 wa NIPIGE TAFU GROUP, Madame Godella Athanasi Hali...
09/06/2026

1.Wa tatu kutoka kushoto kwa walio simama ni mwanachama na mlezi na.2 wa NIPIGE TAFU GROUP, Madame Godella Athanasi Halimenshi, alikuwa mwakilishi wa taasisi katika uzinduzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Women Empowerment Network (TWEN).

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Antony Isack Mwakisyu, aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Theresia Mtewele.

Sambamba na uzinduzi huo, pia yalifanyika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani. Tukio hilo lilifanyika tarehe 05/06/2026, siku ya Ijumaa, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

2.Third from the left of those standing is the Patron No. 2 of NIPIGE TAFU GROUP, Madame Godella Athanasi Halimenshi, who was the institution's representative at the launch of the Tanzania Women Empowerment Network (TWEN) NGO.

The guest of honor at the event was the Kasulu District Commissioner, Colonel Antony Isack Mwakisyu, represented by the Kasulu District Administrative Secretary (DAS), Theresia Mtewele.

In conjunction with the launch, World Environment Day was also celebrated. The event was held on 05/06/2026, Friday, at the Kasulu Town Council Hall.

Address

Umoja
Kasulu
MURUBONA

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nipige TAFU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category