Mtoa Secondary School

Mtoa Secondary School Huu ni ukurasa mahususi kwa ajili ya taarifa za shule ya sekondari Mtoa.

KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA – MTOA SEKONDARINdugu Wanajumuiya wote wa Mtoa Sekondari Wazazi, Wanafunzi, Walimu, Wafany...
24/12/2025

KHERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA – MTOA SEKONDARI

Ndugu Wanajumuiya wote wa Mtoa Sekondari Wazazi, Wanafunzi, Walimu, Wafanyakazi na Wadau wa Elimu,

Tunapoukaribia mwisho wa mwaka 2025, uongozi wa shule unayo furaha kubwa kuwashukuru kwa ushirikiano wenu wa karibu na wa dhati katika safari yetu ya kukuza elimu bora.

Tunawatakia heri ya Krismasi na mwaka mpya 2026, tukiwaombea amani, afya njema, furaha na mafanikio tele katika familia zenu.

Mwaka huu 2025 umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Mtoa Sekondari, ikiwemo:

Kuzaliwa kwa shule mpya ya Sekondari Mtoa Darajani, mradi uliofadhiliwa na Serikali kupitia SEQUIP kwa zaidi ya Tsh milioni 544, tunaishukuru sana Serikali kwa upendo na upeo wake katika sekta ya elimu.

Wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu tayari wameanza masomo rasmi kuanzia mwezi Julai 2025, na tunatarajia shule hiyo kukamilika kwa kidato cha pili na cha nne mwaka ujao.

Vilevile, tumefanikisha ujenzi wa matundu 10 ya vyoo(wanaume na wanawake) katika shule mama ya Mtoa Sekondari ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia mradi uligharimu kiasi Cha Tsh 16,800,000.

Kwa mafanikio haya na mengine, tunawashukuru sana kwa kila namna mlivyoshiriki kutufikisha hapa.

Tukiukaribisha mwaka mpya 2026, tuuchangamkie kwa Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya!

Swali kwa wanafunzi wote waliopitia Mtoa Sekondari tangu 2007 hadi sasa:

"Ni mwalimu gani amekuvutia zaidi na kwa nini?"

Karibuni tushirikiane kumbukumbu nzuri na kuuenzi mchango wa walimu wetu.

Heri ya sikukuu ya X-mass na mwaka mpya!!

Imetolewa na;
Kitengo Cha Habari Mtoa ss.

Wakati tunaelekea kuufunga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026, shule zikiwa zimefungwa, wanafunz wapo likizo, walimu ...
16/12/2025

Wakati tunaelekea kuufunga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026, shule zikiwa zimefungwa, wanafunz wapo likizo, walimu wapo majumbani na mtaani kumechangamka.

Ukiona hii picha, unakumbuka wapi na mshikaji wako gani ambae unahisi kwenye H (hayupo) zilikua nyingi kuliko alama ya kuwepo school?

Sema kuna magwiji wa utoro hadi bodi ya shule yenyewe ikikaa inashindwa kuwajadili mana hawajui k**a mtu bado anasoma au nae kashakua mwalimu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

29/11/2025

"Ujumbe ambao nataka kuwapa awa ambao wanabaki shuleni ni kwamba waendelee kujitahidi katika masomo Yao,Hivyo tu"

Evaline Phanuel, Monitress form four 2025

20/11/2025

Miongoni mwa vijana wa scouts walioleta burudani ya Hali ya juu siku ya mahafali ya 16 Mtoa ss tar 02/10/2025 JKT48 Pacome Zouzua

 Admin anataka kujulikana zaidi... Je, mnafikiri niposti picha yake au niwe na siri hii milele? Tupe maoni yako!    "
19/11/2025



Admin anataka kujulikana zaidi...

Je, mnafikiri niposti picha yake au niwe na siri hii milele?

Tupe maoni yako!

"

Asante sana Pacome Zouzua!!
17/11/2025

Asante sana Pacome Zouzua!!

17/11/2025

KILA LA KHERI KIDATO CHA NNE 2025 SHULE YA SEKONDARI MTOA

Leo tunasimama kwa moyo mmoja k**a familia ya Mtoa Secondary School kuwatakia wanafunzi wetu 82 wa kidato cha nne kila la kheri wanapoanza rasmi mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari.

Tunawaombea kwa Mungu awajalie hekima, utulivu, afya njema, na kumbukumbu sahihi ili kila mmoja aweze kufanya vizuri kwa kiwango cha juu kabisa.

Tukiwa waalimu, wazazi na walezi wenu tunawaamini na tunawaombea kwa dhati kuwa mtaibuka na ushindi, hakuna atakayefeli, hakuna atakayekatishwa tamaa.

Mitihani hii ni daraja tu kuelekea hatua nyingine ya maisha. Tunajivunia juhudi zenu, tunatambua michango ya kila mmoja sasa ni muda wa kuvuna kilicho pandwa.

Endeleeni kuwa waaminifu, tumieni muda vizuri, na kila kitu kitakuwa sawa.

Mungu awatangulie sana wanafunzi wa Mtoa Sec. Mnaweza, na mtashinda!

Ewe mdau na mwanajamii wa Mtoa SS ungana nasi kuwaombea na kuwatakia kila la kheri wanafunzi Hawa wafanye vyema.



KUMBUKIZI YA KIFO CHA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE  BABA WA TAIFALeo Jumuiya ya Mtoa Sekondari na Dunia kwa ujumla t...
14/10/2025

KUMBUKIZI YA KIFO CHA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE BABA WA TAIFA

Leo Jumuiya ya Mtoa Sekondari na Dunia kwa ujumla tunakumbuka miaka mingine tangu kuondoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, shujaa wa kweli wa Taifa la Tanzania na kiongozi wa mfano katika bara la Afrika. Mwalimu Nyerere si tu kwamba alikuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali pia alikuwa mtu mwenye maono, kiongozi aliyesimamia misingi ya haki, usawa, utu, na mshik**ano.

1. Ukombozi wa Tanganyika na Muungano:

Kupitia juhudi zake za kisiasa na kiu yake ya haki, Mwalimu aliongoza Tanganyika kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni mwaka 1961. Mwaka 1964 aliongoza Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar tukio la kipekee barani Afrika ambalo liliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliamini katika nguvu ya umoja na mshik**ano wa watu.

2. Elimu kwa wote:

Mwalimu Nyerere alitambua kuwa maendeleo huanzia kwenye elimu. Alianzisha sera ya Elimu ya Kujitegemea, iliyolenga kumpatia kila Mtanzania maarifa ya kumwezesha kuishi maisha ya kujitegemea. Shule nyingi zilijengwa na Watanzania wenyewe chini ya Azimio la Arusha. Hadi leo, misingi hiyo bado inasaidia Taifa letu.

3. Maadili na Uongozi wa Uadilifu:

Kupitia Azimio la Arusha, Mwalimu alisisitiza juu ya uongozi wa kimaadili – kiongozi kuwa mtumishi wa wananchi, si mtawala. Alipinga ufisadi, ubaguzi na kujilimbikizia mali. Aliishi maisha ya kawaida k**a raia wa kawaida hata baada ya kustaafu, akiwa mfano wa kweli wa unyenyekevu.

4. Mchango katika Ukombozi wa Afrika:

Tanzania chini ya uongozi wa Mwalimu ilikuwa ngome ya mapambano ya ukombozi wa Afrika Kusini, Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Namibia. Aliamini kuwa hakuna Mtanzania atakayekuwa huru kwa kweli hadi pale ndugu wa Afrika watakapokuwa huru.

5. Lugha ya Kiswahili na Utambulisho wa Taifa:

Mwalimu Nyerere pia alithamini sana lugha ya Kiswahili k**a nguzo ya umoja wa kitaifa. Aliifanya kuwa lugha ya kufundishia, ya kisiasa na ya kiserikali. Leo hii, Kiswahili kinazidi kutambulika duniani, ikiwa ni sehemu ya urithi wake.

Katika siku hii ya kumbukizi ya kifo chake (14 Oktoba), tunamuenzi Mwalimu kwa kuendeleza maono yake kwa kulinda amani, kuheshimu utu wa kila Mtanzania, kusimamia haki, na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa lenye misingi imara.

Mwalimu aliondoka kimwili, lakini fikra na maono yake yataendelea kuishi vizazi na vizazi.

β€œWatu hawawezi kula uhuru, lakini bila uhuru hawatakula.” Mwalimu Nyerere.

TULIKUPENDA, LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI. PUMZIKA KWA AMANI BABA WA TAIFA.

πŸ’ HERI YA SIKU YA WALIMU DUNIANI πŸ’Leo tunasherehekea nguvu, hekima na uvumilivu wa WALIMU wetu wote duniani!  Sisi k**a ...
05/10/2025

πŸ’ HERI YA SIKU YA WALIMU DUNIANI πŸ’

Leo tunasherehekea nguvu, hekima na uvumilivu wa WALIMU wetu wote duniani!

Sisi k**a Walimu wa Shule ya Sekondari Mtoa, tunajivunia nafasi yetu katika kujenga jamii yenye maarifa, maadili na matumaini.

Kwa siku hii adhimu, tungependa kuwasikia wanafunzi wetu waliopo na waliopita:
Ni kipi unachokikumbuka, kukithamini au kukipenda kuhusu walimu wako wa Mtoa Sec?

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Tumia sehemu ya comment kuandika salamu zako, shukrani au neno lolote kwa mwalimu aliyekugusa maisha yako!




Keki ya kisasa...
04/10/2025

Keki ya kisasa...

Shule yetu ya sekondari Mtoa ni taa ya elimu katika jamii yetu. Kwa miaka mingi, tumekuwa kikao cha kujifunza na kukuza ...
04/10/2025

Shule yetu ya sekondari Mtoa ni taa ya elimu katika jamii yetu.

Kwa miaka mingi, tumekuwa kikao cha kujifunza na kukuza vipaji vya wanafunzi wetu. Walimu wetu wana utaalamu na kujitolea, wakitoa elimu bora na malezi kwa wanafunzi wetu.

Tunajivunia matokeo bora ya kitaaluma, ushiriki katika shughuli za ziada, na maendeleo ya mwanafunzi wetu kijamii. Shule yetu ni mahali ambapo wanafunzi wanahamasishwa kufikia malengo yao na kuwa wanajamii wenye mchango.

Asante kwa kuwa sehemu ya jumuiya hii ya shule nzuri.

Address

Tyeme
Kiomboi
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mtoa Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mtoa Secondary School:

Share