Babati District Council

Babati District Council 1.1. Mwaka 2004 Halmashauri ya Wilaya ya Babati iligawanyika na kuanzishwa kwa Halmashauri ya Mji kwa mujibu wa GN 352 ya tarehe 17 Septemba, 2004.

HISTORIA FUPI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BABATI
Halmashauri ya Wilaya ya Babati ni mojawapo kati ya Halmashauri 2 za Wilaya ya Babati na ni moja kati ya Halmashauri 6 za Mkoa wa Manyara. Wilaya ya Babati ilizinduliwa rasmi Julai mwaka 1986 baada ya kuanzishwa rasmi kwa tangazo la gazeti la serikali namba 403 la tarehe 1 Oktoba, 1985 la kugawanywa Wilaya ya Hanang’ na kuundwa Wilaya mbili za Babat

i na Hanang’. MIPAKA NA ENEO LA WILAYA
Halmashauri ya Wilaya ya Babati iko Kaskazini mwa Tanzania kati ya Latitudo 30 – 50 Kusini mwa Ikweta na Longitudo 350 – 370 Mashariki ya Greenwich. Halmashauri ina eneo la kilometa za mraba 5,608.14 sawa na asilimia 92.4 ya eneo la Wilaya lenye ukubwa wa kilometa za mraba 6,069. Halmashauri inapakana na Wilaya ya Monduli kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kaskazini Magharibi, Wilaya ya Mbulu kwa upande wa Magharibi, Wilaya ya Hanang’ kwa upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Kondoa kwa upande wa Kusini na Wilaya ya Simanjiro kwa upande wa Kusini Mashariki.

Mkuu wa Wilaya ya Babati amewashukuru Vijana wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi lá akiba .Mkuu huyo ameyasema hayo katika ufu...
16/08/2018

Mkuu wa Wilaya ya Babati amewashukuru Vijana wanaoshiriki mafunzo ya Jeshi lá akiba .Mkuu huyo ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mafunzo ya jeshi lá akiba yanafanyika Kiwilaya Kata ya Kisangaji Kijiji cha Kisangaji Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Aidha amesisitiza Vijana hao kushiriki katika Kazi za maendeleo ili kujiletea maendeleo. Kabla ya Ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ameongea na Kamati za Maendeleo za kata za Magugu, Mwada na kisangaji. Mkuu wa Wilaya Pia ameongozana na wajumbe Kamati za ulinzi na usalama ambao wametoa Ujumbe na ufafanuzi wa mambo mbalimbali.

21/05/2017

Habari za jumapili wapendwa

Address

Babati
Manyara

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Babati District Council posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share