27/11/2025
FIFA YATOA MAFUNZO YA GRASSROOT MANYONI – KAIMU MKURUGENZI C. KISWAGA AFUNGA RASMI
Manyoni, 27 Novemba 2025
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Bw. Cainan Kiswaga, leo amefunga rasmi mafunzo ya Grassroot yaliyoendeshwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa kushirikiana na TFF, kwa walimu wa michezo na makocha wa ngazi ya jamii.
Mafunzo hayo ya siku 5 yamefanyika wilayani Manyoni kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu na makocha juu ya mbinu bora za kufundisha mpira wa miguu kwa watoto na vijana wadogo kuanzia ngazi ya msingi.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo, Bw. Kiswaga aliipongeza FIFA na TFF kwa kuchagua Manyoni kuwa sehemu ya mpango huo wa kukuza soka la vijana, na kusisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano ili vipaji vipatikane mapema na kulelewa kitaaluma.
"Grassroot ni msingi wa mafanikio ya mpira wa miguu wa taifa. Tunapowajengea uwezo makocha hawa, tunajenga kesho ya soka la Tanzania," alisema Kiswaga.
Washiriki waliopata mafunzo wamesena kuwa mafunzo hayo kwao imekua ni bahati na kitu muhimu kwao na kuahidi kuendeleza walichojifunza kwa vitendo mashuleni na katika jamii zao.
Kwa upande wake, Raymond Gweba Mkufunzi wa FIFA, aliyeongoza mafunzo hayo, alitoa pongezi kwa Halmashauri ya Manyoni ikiongozwa na Mkurugenzi kwa maandalizi mazuri na ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa washiriki.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida Hamisi Kitila amewashukuru TFF kwa kukubali kuja kutoa Mafunzo hayo na ameshukuru pia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kuwapongeza waliopata mafunzo.
"Nawapongeza sana kwa mafunzo haya mliyoyapata kwa Siku hizi na sasa k**a Mkoa tutarajie Mapindizi makubwa kwenye Mpira wa Miguu"