28/12/2016
HIVI KWANZA MNAJUA ASILI YA KABILA LA
WAGOGO!!!!!??
KARIBUNI,
Wagogo (mmojawao anaitwa Mgogo) ni kabila
kubwa la Tanzania ya kati, wenyeji wa mikoa ya
Dodoma na Singida. Wanakadiriwa kuwa zaidi ya
1,500,000.
Lugha yao ni Cigogo (kwa Kiswahili hutamkika
Kigogo).
Dini ya wengi wao ni Ukristo, hasa wa
madhehebu ya Anglikana, halafu wa Kanisa
Katoliki.
Historia na maendeleo ya Wagogo viliathiriwa
sana na ukame na biashara ya watumwa, kiasi
kwamba hata leo ni kati ya makabila fukara zaidi
nchini Tanzania.
UTAWALA WA JADI
Wagogo walikuwa wakiongozwa na mtu aliyeitwa
Mtemi. Watemi kadhaa waliongoza kabila hilo
kabla ya mfumo wa uongozi kuvurugwa na
ukoloni.
Mtemi wa mwisho aliitwa Mazengo ambaye
alitokea katika kijiji cha Mvumi, wilaya ya
Dodoma vijijini.
NYUMBA ZA ASILI
Wagogo wamekuwa wakijenga nyumba ambazo
huitwa tembe"kwa kigogo itembe". Tangu zamani
kuta za tembe zilijengwa kwa fito (sito kwa lugha
yao) zilizosukwa kwa kupisha kuzuia mwanga na
maji. Vipande vya kuta vilivyosukwa kwa sito
vinaitwa "izizi".
Tembe huezekwa kwa udongo ambao hushikiliwa
na miti midogo midogo (walo). Walo huwa
unashikiliwa na miti mikubwa kidogo (mahapa) na
mahapa hushikiliwa na miti mikubwa (michichi).
Michichi ambayo ndiyo hubeba uzito wote
hushikiliwa na nguzo kubwa za miti imara na
migumu. Nguzo hizo hutiwa masumbili.
Kwa miaka ya karibuni kuta za tembe hujengwa
pia kwa matofali yanayotengenezwa kwa udongo.
SHUGHULI ZA UCHUMI
Wagogo ni miongoni mwa makabila ya Wakulima
na Wafugaji kwa asili na hufuga mifugo k**a
ng'ommbe, mbuzi na kondoo, kwa Kigogo
wanyama hao huitwa "ng'ombe, mhene na
ngholo" pamoja na punda "ndogowe" kwa ajili ya
ubebaji mizigo na wakati mwingine kulimia
wakitumika kukokota majembe ya kukokotwa,
k**a watumikavyo ng'ombe pia. Smbamba na
shughuli hiyo kilimo ndio shughuli kubwa na ya
wengi ijapokuwa kwa miaka mingi imekuwa
ikiathiriwa na kiwango kidogo cha mvua
zinazonyesha kutokana na jiografia ya Mikoa hiyo
miwili, yaani, Dodoma na Singida.
Mazo yanayolimwa kwa wingi ni mahindi
"mtama", mtama '[[uwele, na lugugu]. Siku za
hivi karibuni umeingia mtama unaokomaa kwa
muda mfupi k**a vile serena, lulu, tegemeo,
masia, okoa, n.k.]]', muhogo kiasi na katika
maeneo machache mpunga na zabibu, zao
ambalo ni mahususi kwa biashara.
CHAKULA KIKUU
Wagogo hula ugali wa uwele k**a chakula kikuu
na huchukulia ugali wa mahindi mtama k**a
chakula laini na chepesi kisicho na nguvu.
Miaka ya zamani mlo wa kawaida wa Mgogo
mwenye uwezo (yaani mwenye ng'ombe)
ulihusisha ugali, maziwa, mafuta ya ng'ombe,
kwa kigogo samuli na mboga k**a mlenda
"ilende", safwe, cidingulilu, nyakifwega, muhilile,
sanghala, munzimwa, cipali, ihaji, sagulasagula,
ikuwi, fwene, nghalabwajila (hasa wakati masika
inapoanza) n.k.
Kwa sasa Wagogo wamekuwa wakila chakula
cha kawaida k**a makabila mengine nchini
Tanzania.
LAFUDHI YA LUGHA
Kabila la Wagogo lina lahaja ndani yake ambazo
hutofautiana kutoka lahaja moja hadi nyingine
kwa jinsi ambavyo hutamka maneno, yaani
huongeza na kupunguza baadhi ya matamshi
kwenye neno, na pia katika msamiati. Kwa
ujumla kuna lahaja zipatazo 4, ambapo lahaja za
Cinyambwa na Cinyaugogo ndizo hujulikana zaidi.
1. Wanyambwa - Hili ni kundi linaloonekana wazi
kwenye kabila hili ambao huongea lafudhi ya
Kinyambwa. Wanyambwa hutokea vijiji vya
magharibi kwa mji wa Dodoma na sehemu ya
wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Mifano - matamshi - vipi? = ntaule?
-msamiati - panda darini = ukwine kitembe
2. Wanyaugogo - hawa huongea lafudhi iitwayo
Chinyaugogo. Wanyaugogo ambao ndio
wanaowakilisha kundi kubwa sana hutokea vijiji
vya mashariki na kusini kwa mji wa Dodoma na
pia wilaya ya Mpwapwa. Kwa sababu mtemi
Mazengo alikuwa mnyaugogo kutoka Mvumi
mahali ambapo palijengwa kijiji kinachoitwa
Mvumi Makulu (kwa maana kwamba ndipo
ilipokuwepo Ikulu ya Mtemi), inaaminika kuwa
lafudhi hii ndicho Kigogo cha asili isiyoathiriwa
na lugha za nje.
Mifano - matamshi: - vipi? = nhaule?
-msamiati - panda darini = unanuce kitembe
3. Wetumba - Hawa ni wagogo walioathiriwa
Kigogo chao na Kikaguru. Hupatikana katika
wilaya za Kongwa na Mpwapwa
Mfano - matamshi - jua limekuchwa - dizuwa
diswa. Wanyaugogo hapa husema "lizuwa laswa/
liswa"
4. Wetiliko - Hawa ni wagogo wenye asili au
mchanganyiko na wahehe, na hupatikana maeneo
ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Mfano - matamshi - twende = tibite. Wanyaugogo
hapa husema "cibite"
A MAJINA YA UKOO YA CIGOGO
Majina hayo ni k**a Mazengo, Cidosa, Cilongani,
Malecela, Mwaluko, Mavunde, Ndejembi,
Manyesela, Mbogambi, Mdachi, Kapaya, Matonya,
Mtunya, Kusila, Nhonya, Mhalanyuka, Mbenaa,
Chibile, Mdoli, Lusinde, Njamasi, Majenda,
Chiwamba, Chiwaligo, Mazoya, Ufinyu,
Chilyawanhu, Mahujilo, Magaya, Ngoli,
Chiwanga,Lenjima, Lubeleje, Makupila, Fukunyi,
Mondigwa, Ndasimi, Nhukuwala, Muhembano,
Masinga, Ndahani, Chedego, Chenda, Chonya,
Chimbwi, Cibehe, Mabwe, Malejehe, Madole
(endeleza)
SEMA SASA JUU YA WAGOGO UWAJUAVYO
WEWE..!!!
# WAGOGO_OYEEEEE_LEO_NIMEWAGUSA_
HAHAHAAA!!