28/05/2026
๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Halmashauri ya Mji Masasi imefanikiwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na vyoo matundu sita ya elimu ya awali katika Shule ya Msingi Kitunda yaliyowavutia wazazi wengi zaidi kuwaandikisha watoto wao katika elimu ya awali.
Utekelezaji wa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi 67,300,000 kutoka katika Mradi wa Boost, ukiwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisasa zaidi ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa elimu ya awali pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za elimu katika eneo la Kitunda.
Akizungumza Mwalimu Mkuu Shule hiyo, Mwl. Cyprian Ndaka, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuipatia shule hiyo mradi huo bora, Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Waheshimiwa Madiwani na Mkurugenzi wa Mji kwa maelekezo mbalimbali na usimamizi wa mradi huo bora.
Amesema kuwa mradi huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na hivyo kuvutia wazazi wengi zaidi kuwaandikisha watoto wao katika elimu ya awali.
Vilevile, mradi huo unatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wa ngazi ya awali.