Cosoza Zanzibar

Cosoza Zanzibar The Copyright Society of Zanzibar Dealing with Registration, Protection of Artistic works & Provide

MAANA YA HAKIMILIKI

Hakimiliki ni haki ya kipekee aliyonayo msanii kutokana na kazi yake ,haki ya kumruhusu au kumzuwia mtu/taasisi kufanya yafuatayo dhidi ya kazi yake :-

kutoa nakala ( reproduction)
kutafsiri (translation)
kukodisha (rental)
kufanya maonyesho (public performance)
kuisafirisha nakla za kazi husika
kuitangaza kazi
au kwa namna nyengine yoyote kuiwasilisha kazi husika kwa

jamii

HISTORIA YA SHERIA YA HAKIMILIKI (COPYRIGHT ACT NO.14, 2003)

Dhana na ulinzi wa hakimiliki si mpya k**a jamii ya watu wa Zanzibar inavyofikira kwani Sheria ya hakimiliki (Copyright Act No. 14 of 2003) ilikuja kuifuta sheria ya Order in Council ya mwaka 1962 ambayo pia ilifatiwa na Englisha Copyright Act 1956 ambazo zote hizo kwa pamoja zilikuwepo kwa ajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wakoloni zaidi na sio wazanzibar kwa ujumla. Ndipo mnamo mwaka 2003 Serikali iliamua kuifanyia marekebisho ili kuendana na wakati uliopo. KAZI ZINAZOLINDWA NA SHERIA YA HAKIMILIKI

vitabu,vitini,makala,program za computer,maandishi ya kisayansi na
Kisanaa pamoja ma kazi nyengine za kimaandishi;

mihadhara ,hotuba ,mahubiri na kazi nyengine zenye muelekeo k**a huo. kazi za maigizo na zile za muziki wa maigizo ,maigizo bubu,na upigaji wa vinanda na kazi nyengine zinazoandzliwa kuoneshwa jukwaani. kazi za kimuziki ( wa sauti na ala) zenye kujumuisha au bila kujumuisha
Maneno. kazi za vielelzo vya kusikia na kuona

kazi za usanifu wa majengo

kazi za kuchora,kuchora kwa kutumia rangi ,usanifu wa majengo,sanaa na
uchongaji vinyago,sanaa ya utunzi nakshi ,sanaa ya litografia na mapambo

kazi za sanaa ya upigaji picha ,ikiwa ni pamoja na kazi zinazotolewa kwa
Njia zinazoambatana na upigaji picha. kazi za sanaa tumizi,ziwe za mikono au zinazotengenezwa katika viwango
Vya viwandaji. vielelzo,ramani,plani,michoro na kazi za mawanda matatu zinazohusiana
na jiografia,usanifu wa majengo au sayansi

UANZISHWAJI WA AFISI YA MSAJILI WA HAKIMILIKI NA KAZI ZAKE

Afisi ya Msajili wa Hakimiliki ilianzishwa mnamo mwaka 2005 kwa ajili ya kufanya kazi zifuatzo:-

Kusajili kazi nilizozitaja hapo juu. Kulinda na utetea maslahi ya wasanii

Kutoa leseni kwa ajili ya matumizi halali ya kazi za hakimiliki

Kukusanya mirabaha kwa matumizi halali ya kazi za hakimiliki

Kugawa mirabaha kwa wanaostahili kupipwa

Kuelimisha jamii juu ya masuala ya hakimiliki

Kutoa ushahidi mahak**ani pale inapohitajikana inapoonekana kuna uvunjwaji wa hakimiliki

Kutoa ushauri wa kisheria kuhusiana na masuala ya hakimiliki

Kutayarisha na kupitia mikataba inayohusiana na hakimiliki.

Address

Mazizini/Opposite To Mazizini Police Post, MINISTRY OF JUSTICE AND CONSTITUTIO
Mazizini
P.O.BOX4085,ZANZIBAR

Opening Hours

Monday 07:00 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255776664040

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Cosoza Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Cosoza Zanzibar:

Share