Mbeya Zonal Referral Hospital

Mbeya Zonal Referral Hospital Ukurasa rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya

Mbeya Zonal Referral Hospital cordially invites you to visit our exhibition booth at the upcoming 98th Agricultural and ...
21/07/2026

Mbeya Zonal Referral Hospital cordially invites you to visit our exhibition booth at the upcoming 98th Agricultural and Commercial Show in Lusaka, Zambia.

The event will take place from July 29th to August 3rd, 2026, at the zambia, Lusaka Showgrounds, under the theme "Fostering Trade and Investment".

As a premier tertiary healthcare provider in the region, we are proud to showcase our advanced medical services, specialized diagnostic capabilities, and cross-border referral networks.

We offers a valuable platform to meet our senior medical consultants, explore strategic healthcare partnerships, and learn more about our medical tourism initiatives within the SADC region.

We look forward to welcoming you to our pavilion.


HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KWA MAPINDUZI YA MAENDELEO JIJINI MBEYAHospitali ya Rufaa y...
21/07/2026

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA KWA MAPINDUZI YA MAENDELEO JIJINI MBEYA

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imetunukiwa Tuzo ya Heshima na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, k**a ishara ya pongezi kwa kutambua mchango , mkubwa katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na huduma za kijamii mkoani Mbeya pamoja na juhudui zilizofanikisha sherehe za maandalizi ya kitaifa.

Uongozi wa Mkoa wa Mbeya na wadau wa maendeleo wamempongeza Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali pamoja na Watumishi wa hospitali kwa uzalendo na utendaji uliotukuka katika kuunga mkono miradi ya maendeleo ya jiji hilo.

Tuzo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya k**a ishara ya pongezi kwa namna Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inavyojitoa kikamilifu kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuboresha huduma za kijamii mkoani hapa.
Hatua hii imetajwa na wadau wa maendeleo mkoani Mbeya k**a chachu itakayohamasisha wadau mbalimbali wa taasisi za umma na binafsi kuongeza ushirikiano na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka.

Mambo yalivyo leo kwenye viwanja vya Sokoine! Mamia ya watumishi wa MZRH na wakazi wa Mbeya wamejitokeza kwenye michezo ...
11/07/2026

Mambo yalivyo leo kwenye viwanja vya Sokoine! Mamia ya watumishi wa MZRH na wakazi wa Mbeya wamejitokeza kwenye michezo mbalimbali kwenye Tamasha la Michezo na Vipaji, likiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Godlove Mbwanji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), Dkt. Godlove Mbwanji, leo ameongoza mamia ya watumishi ...
11/07/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), Dkt. Godlove Mbwanji, leo ameongoza mamia ya watumishi wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na wananchi wa Jiji la Mbeya katika mbio za pole (jogging).

Mazoezi hayo yamefanyika ikiwa ni sehemu ya kufunga rasmi kilele cha maadhimisho ya Tamasha la Michezo na Vipaji 2026 katika viwanja vya michezo Sokoine jijini Mbeya.

Tamasha hilo la wiki moja limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba, pamoja na burudani za kuonyesha vipaji vya sanaa

10/07/2026

Wananchi wote Mnakaribishwa

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA (MZRH) NA  MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA) ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAPATIA WAFAN...
03/06/2026

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA (MZRH) NA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA) ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAPATIA WAFANYAKAZI TPA HUDUMA ZA MATIBABU YA DARAJA LA JUU

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zimesaini rasmi makubaliano ya kutoa huduma za matibabu ya kibobezi na daraja la juu (VIP) kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo, huku hospitali ikitangaza mapinduzi makubwa ya kimatibabu yaliyolenga kuifanya kuwa kituo kikuu cha tiba utalii kwa nchi za SADC.

Hatua hiyo imefikiwa leo, Juni 3, 2026, baada ya pande zote mbili kuridhia na kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) pamoja na Mkataba wa Kiwango cha Huduma (SLA). Nyaraka hizo zimesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MZRH, Dkt. Godlove Mbwanji, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbosa mara baada ya kuwasilishwa na Mashaka Karume, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika mapema leo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameelezea kuwa ushirikiano huo ni sehemu ya mikakati ya hospitali hiyo kusogeza huduma za afya maeneo ya kazi, sambamba na kuonyesha maboresho makubwa ya kibingwa yaliyofanyika katika kuanzishwa kwa upasuaji wa moyo na kukaribia kukamilika kwa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa mishipa ya damu (Cathlab), Kuimarika kwa huduma za upasuaji wa ubongo, moyo na mishipa ya fahamu pamoja huduma za kibingwa za kubadilisha na kupandikiza nyonga na magoti.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndg. Mashaka Karume, amebainisha kuwa mkataba huo unaenda kuleta mageuzi makubwa kiutendaji kwa kuondoa vikwazo vya kiafya vinavyowakabili wafanyakazi wa mamlaka hiyo, hasa wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Timu ya Wataalam wa Bohari ya Dawa (MSD) imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), lengo likiwa ni kuimarish...
03/06/2026

Timu ya Wataalam wa Bohari ya Dawa (MSD) imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH), lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi na kuboresha mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Ziara hiyo iliyoongozwa na David Rugamalila, imehusisha mazungumzo ya kina na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Godlove Mbwanji yaliyolenga kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati, kutatua changamoto za ugavi, na kuhakikisha huduma bora za matibabu zinaendelea kutolewa kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini.

Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tunakupongeza Mhe. Ummy Mwalimu  kwa kuteuliwa na Rais wa ...
03/06/2026

Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tunakupongeza Mhe. Ummy Mwalimu kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. Kila la heri katika majukumu yako mapya.

Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tunakupongeza Bi. Ummy Mwalimu kwa kuteuliwa na Rais wa Ja...
03/06/2026

Menejimenti na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya tunakupongeza Bi. Ummy Mwalimu kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mshauri wa Rais katika Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto. Kila la heri katika majukumu yako mapya.

Shukrani: Ujio wenu na maneno yenu ya heri yameendelea kutupa chachu na hamasa ya kutoa huduma bora, zenye viwango na up...
02/06/2026

Shukrani:
Ujio wenu na maneno yenu ya heri yameendelea kutupa chachu na hamasa ya kutoa huduma bora, zenye viwango na upendo kwa jamii yetu.

Address

Hospital Street
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbeya Zonal Referral Hospital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mbeya Zonal Referral Hospital:

Shortcuts

Share