15/06/2026
BADO NAKUPENDA.
: Benedict.
ya Pili...
JOGOO ANAWIKA?
Rebeka aliendelea kumsogelea Beatho taratibu. Beatho, akiwa amechanganyikiwa, alijikuta akijigonga kwenye sofa na kuangukia hapo. Kabla hajajua afanye nini, Rebeka alikuwa tayari amemsogelea zaidi na kuanza kumpapasa na mkono yake laini.
"Rebeka, unataka nini?"
Aliuliza kwa sauti iliyochanganyika na mshangao.
Lakini Rebeka hakujibu. Ukimya uliotanda ulionekana kusema mengi kuliko maneno. Beatho alihisi mapigo ya moyo wake yakiongezeka kasi huku akishindwa kuzuia kilichokuwa kinaendelea mbele yake.
Ghafla, honi ya gari ilisikika nje ya nyumba.
Sauti hiyo ilimrudisha kila mmoja kwenye hali ya kawaida.
Haraka sana Rebeka aliondoka sebuleni na kukimbilia chumbani kwake. Beatho naye akajifanya kutulia kwa kuwasha televisheni, ingawa televisheni yenyewe haikuwa na tatizo lolote. Hapo ndipo alipotambua kuwa shida haikuwa TV, bali kulikuwa na jambo lingine kabisa lililokuwa limepangwa.
Muda mfupi baadaye, wazazi wake waliingia ndani.
"Mzima mwanangu? Naona umetutembelea."
Mama yake alimsalimia kwa upole.
"Nipo salama mama. Habari za majukumu?"
"Nzuri tu. Rebeka yupo?"
"Ndiyo, naamini yupo chumbani kwake."
Mazungumzo yaliendelea k**a kawaida, lakini akili ya Beatho ilikuwa mbali. Alikuwa bado akitafakari tukio la muda mfupi uliopita.
"K**a wazazi wake wasingefika ghafla, ingekuwaje?"
Swali hilo liliendelea kumzunguka kichwani.
Baada ya kukaa kwa muda, Beatho aliaga na kuondoka.
Mara tu alipoondoka, mama yake alimgeukia Rebeka..
"Vipi, umefanikiwa?"
Rebeka alijibu kwa kutikisa kichwa kuashiria ndiyo.
"Ni mzima kweli?"
Safari hii uso wa Rebeka ulijaa aibu.
"Jogoo anawika vizuri kabisa..."
Alijibu kwa sauti ya chini kiasi kwamba iliwalazimu wengine kutazamana kabla ya kucheka.
Hapo ndipo ilipoonekana wazi kuwa kile kilichotokea hakikuwa jambo la bahati mbaya. Kulikuwa na mkono wa wazazi wake Beatho nyuma ya pazia.
Usiku huo, Beatho alipofika nyumbani hakupata amani.
Kila alipojaribu kufikiria jambo lingine, sura ya Rebeka ilijikuta ikirudi tena akilini mwake.
"Huyu msichana ana nini hasa?"
Aliwaza.
Kadiri alivyokumbuka tabasamu lake, sauti yake na namna alivyokuwa akizungumza, ndivyo alivyozidi kupotea kwenye mawazo.
Hatimaye usingizi ulimchukua.
Lakini hata ndotoni, jina lililoendelea kujirudia lilikuwa moja tu.
Rebeka.
Siku iliyofuata, majira ya mchana, Beatho alikuwa akipita mitaani k**a kawaida yake.
Njiani alikatiza karibu na kundi la wasichana waliokuwa wakipiga stori.
Kwa sababu ya mawazo mengi, alipita bila hata kusalimia.
"Wewe Beatho!"
Mmoja wao alimwita.
Akageuka kwa heshima.
"Naam?"
"Mambo?"
"Poa. Habari yako?"
"Sio poa. Mbona unatupita bila salamu?"
Beatho akatabasamu kwa aibu.
"Samahani sana. Mawazo mengi."
"Sawa basi, umesamehewa handsome boy."
"Asante. Ngoja niwahi."
Akaendelea na safari yake.
Baada ya kuondoka, mabinti wale walianza kujadili.
"Wewe bwana! Umeanza tena kumpa sifa?"
Mmoja akamwambia mwenzake.
"Acha bana. Mimi namkubali sana huyo kaka."
"Kweli?"
"Kabisa!"
Wengine wakacheka kwa sauti.
"Mimi nikiona anachelewa kunitongoza, nitamtongoza mwenyewe."
Fatuma alisema huku akiwafanya wenzake wapige kelele za mshangao.
Lakini Sara, aliyekuwa k**a kiongozi wao, alitikisa kichwa.
"Mimi huyo simwelewi kabisa."
"Kwa nini?"
"Ni mpole kupita kiasi. Nimeshawahi kukutana naye club, lakini huwezi kujua anafikiria nini."
Wote wakaanza kujadili tabia ya Beatho.
Kwa wengi, ilikuwa ajabu kuona kijana mwenye sura nzuri, mwenye juhudi na anayeheshimika, lakini bado asiwe na mazoea ya kuwakimbilia wasichana k**a vijana wengi walivyofanya.
Jioni ilipowadia, Beatho na rafiki yake Alto walikuwa kwenye mizunguko yao ya kawaida wakikusanya CD walizokuwa wamekodisha.
Baada ya kupitia sehemu nyingi, Alto alisisitiza waishie kwa Aisha.
Mwisho walifika nyumbani kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ushindi, Mzee Omari Rashimu Abdullah, ambaye alikuwa baba yake Aisha.
Alto alibisha hodi.
Aisha akafungua mlango.
"Samahani, ile CD ya Naina bado sijamaliza. Nitakurudishia kesho."
"Hakuna shida. Tatizo si CD."
"Basi?"
"Kuna mtu anakuhitaji nje."
"Nani?"
"Beatho."
Aisha alishtuka kidogo.
"Aje mwenyewe basi."
Alto alijaribu kumbembeleza, lakini Aisha alibaki msimamo wake.
Baada ya kufikiria kwa haraka, Alto akamshika mkono na kumvuta taratibu.
"Jamani Alto, sitaki..."
Mdomo ulikataa, lakini miguu iliendelea kufuata.
Dakika chache baadaye walifika pale alipokuwa amesimama Beatho.
Beatho mwenyewe hakuwa na habari ya mpango huo.
Alikuwa tayari amewasha pikipiki ili kuondoka.
Lakini Alto alimkaribia, akachomoa funguo na kumnong'oneza:
"Mimi kazi yangu imeisha. Huyu hapa. Ongea naye."
"Lakini..."
"Lakini nini? Uwanja ni wako."
Alto akaondoka na kuwaacha wawili hao wakitazamana.
Sasa, kwa mara ya kwanza, Beatho na Aisha walikuwa uso kwa uso.
Na hakuna aliyekuwa tayari kuvunja ukimya.
⚛️⚛️⚛️ Itaendelea......
next k**a umeipenda,