Chadema Jimbo la Monduli

Chadema Jimbo la Monduli Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Chadema Jimbo la Monduli, Political organisation, Monduli.

02/09/2016
Chama Cha demokrasia na Maendeleo   Wilya ya Monduli kimeazimia na kuunga mkono Tamko la Kamati Kuu ya Chama Kuwa na Maa...
09/08/2016

Chama Cha demokrasia na Maendeleo Wilya ya Monduli kimeazimia na kuunga mkono Tamko la Kamati Kuu ya Chama Kuwa na Maandalizi kwa ajili ya September Mosi 2016 katika Operation .
Na kikao Hiki kilikuwa ni Kikao na Wadau wa Chama Wilaya ya Monduli katika kuelekea kwenye kilele cha September 1...
Imara Imara...
Peopleeeeees......!!!!

Chama Cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO-CHADEMA Wilaya ya Monduli Kimeendelea na Vikao Vyake vya Ndani katika kuhakikisha Cham...
24/07/2016

Chama Cha DEMOKRASIA NA MAENDELEO-CHADEMA Wilaya ya Monduli Kimeendelea na Vikao Vyake vya Ndani katika kuhakikisha Chama Kinasonga Mbele na Kujadili kwa kina hali Halisi ya Kisiasa Wilayani na Taifa kwa Ujumla.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) Wilaya ya Monduli Mh.Martin Kubena akiwa na vijana Toka Kata ya Moto wa Mbu,Maj...
18/07/2016

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA) Wilaya ya Monduli Mh.Martin Kubena akiwa na vijana Toka Kata ya Moto wa Mbu,Majengo na Migungani katika kuandaa mizinga ya kufuga nyuki, na kuwahamasisha Vijana kujitegemea na kutegemewa na Taifa.
VIJANA "NGUVU YA MABADILIKO"

Ilikuwa ni Finali za mpira wa miguu iliyokuwa ikaratibiwa na kuandaliwa na chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Monduli   ...
18/07/2016

Ilikuwa ni Finali za mpira wa miguu iliyokuwa ikaratibiwa na kuandaliwa na chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Monduli , Ambapo Mgeni Rasmi katika kufunga mashindano hayo alikuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. na Viongozi wa Chama Wilaya ya Monduli,
Mashindano hayo yalijumuisha timu zote za mpira wa Miguu ndani ya Wilaya ya Monduli ambapo katika Mashindano hayo Timu ya Mwalimu Anna FC Ilishinda kwa mikwaju ya Penalti dhidi ya timu ya Serena FC, Hata Hivyo katika mashindano Hayo Mbunge alikabidhi zawadi ya Ng'ombe kwa mshindi wa kwanza,kitita sh.100,000 na na kuahidi kutengeneza uwanja wa Mpira katika viwango na kila timu iliyoshiriki mashindano Hayo itapewa Jezi moja kwa timu 14 zilizoshiriki Mashindano Hayo k**a kutia motisha kwenye Michezo.

08/06/2016
22.5.2016  Ilikuwa ni ziara ya Kuimarisha Chama Ndani ya Wilaya ya Monduli Kata ya Moita ....Iliyohudhuriwa na Naibu Kat...
24/05/2016

22.5.2016 Ilikuwa ni ziara ya Kuimarisha Chama Ndani ya Wilaya ya Monduli Kata ya Moita ....
Iliyohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zanzibar Mh.Salum Mwalim akiambatana na Mbunge wa Monduli Mh Julius Kalanga pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Mh Edward Lowassa

21.5.2016 Ilikuwa ni ziara ya Kuimarisha Chama Ndani ya Wilaya ya Monduli,Kata ya Mto wa Mbu..... Iliyohudhuriwa na Naib...
24/05/2016

21.5.2016 Ilikuwa ni ziara ya Kuimarisha Chama Ndani ya Wilaya ya Monduli,Kata ya Mto wa Mbu.....
Iliyohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zanzibar Mh.Salum Mwalim,Mbunge wa Monduli Mh Julius Kalanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Mh Edward Lowassa

07/05/2016
02/05/2016
29/04/2016

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi.

Kutokana na umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya wananchi yanayobeba matakwa yao katika mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa CHADEMA hakitashiriki Kura ya Maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada ya kubadili na kuondoa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

Badala yake, CHADEMA kitaendelea kuweka agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika jamii kutokana na matatizo mbalimbali k**a vile ukosefu wa haki, migogoro ya ardhi, wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii zikiwemo elimu, maji na afya.

Dkt. Mashinji ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini.

Dkt. Mashinji pia amekishukuru chama hicho kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika mradi ambao unahusisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku akisisitiza kuwa CHADEMA kiko tayari kwa ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani ya nchi.

“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi k**a ilivyowasilishwa kwenye rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya Wananchi.

“Jana na leo tumewasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakisema kuwa wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile iliyochakachuliwa bungeni.

“Katiba Mpya iliweka masuala kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua namna ya kuvuka tukishafika mtoni,” amesema Katibu Mkuu Dkt. Mashinji.

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji amesisitiza kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo imara ya demokrasia na uongozi bora ni muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu uliopo.

Akisisitiza umuhimu wananchi kuwa Katiba inayotokana na wananchi, Dkt. Mashinji alitolea mfano wa nchi ya Norway ambayo miaka mingi nyuma ilikuwa sawa na Tanzania, lakini ilifanikiwa kuondokana kuwa taifa maskini kutokana na uwepo wa uongozi bora, mifumo na taasisi imara za kidemokrasia ambazo ziliweza kusimamia ustawi wa taifa hilo kutokana na uchumi wa gesi na mafuta na sasa ni kati ya mataifa yaliyoendelea barani Ulaya na duniani kwa ujumla.

Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party, Knut Olsen, umesema kuwa chama hicho kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa katika jamii ya wananchi wa maeneo ya pembezoni.

“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji, vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki mchakato wa maamuzi. Tunatarajia kuendelea kupata ushirikiano katika hatua ya pili,” amesema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa Mradi hapa nchini.

Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa Centre Party ni pamoja ni Katibu Mkuu wa Vijana Sara Hamre, Katibu Mkuu wa Wanawake, Eline Stokstad-Oslan na Katibu Mkuu wa Wazee, Kristin Madsen.
Mradi huo wa Elimu ya Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini ya ufadhili wa chama hicho, katika awamu ya kwanza ulihusisha kata za Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo, Mayanga na Madimbwa.

Imetolewa leo Alhamis, Aprili 28, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

24/04/2016

Address

Monduli

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Chadema Jimbo la Monduli posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share