TFS-Tree seed Production

TFS-Tree seed Production Tree Seed Production station (TSPS) ni kituo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu

Njoo viwanja vya 88 ilikupata mahitaji ya Miche mbalimbali
02/08/2026

Njoo viwanja vya 88 ilikupata mahitaji ya Miche mbalimbali

Karibu tukuhudumie
02/08/2026

Karibu tukuhudumie

Naibu waziri wa Maliasili na utalii alipotembelea Banda la wizara ya Maliasili na utalii sehemu ya Wakala wa Huduma za M...
08/07/2026

Naibu waziri wa Maliasili na utalii alipotembelea Banda la wizara ya Maliasili na utalii sehemu ya Wakala wa Huduma za Misitu alipongeza Kwa kazi nzuri inayofanywa na Kituo Cha Mbegu za Miti

TFS YAKABIDHI SERIKALI GAWIO LA SHILINGI BILIONI 29.4, YATUNUKIWA TUZO YA UFANISIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
01/07/2026

TFS YAKABIDHI SERIKALI GAWIO LA SHILINGI BILIONI 29.4, YATUNUKIWA TUZO YA UFANISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea gawio la Shilingi Bilioni 29.4 kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakati wa hafla ya Gawio Day 2026 iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Juni 30, 2026.

Gawio hilo lilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFS, Luteni Mstaafu Chiku Abdallah Gallawa, pamoja na Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Huduma Saidizi na Utawala, Emanuel Wilfred Kiboko, kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TFS.

Mbali na kukabidhi gawio hilo, TFS pia ilitunukiwa Tuzo ya Mshindi wa Pili (1st Runner-Up) katika kipengele cha Seven-Year Consistent Remitters kwenye Gawio Day – Excellence Awards 2026, ikiwa ni kutambua rekodi yake ya kuwasilisha gawio kwa Serikali kwa miaka saba mfululizo. Tuzo hiyo inaonyesha uthabiti wa TFS katika kuchangia mapato ya Serikali na kuzingatia misingi ya uwajibikaji wa kifedha.

Mchango huo ni sehemu ya jumla ya Shilingi Trilioni 1.32 zilizowasilishwa serikalini na taasisi za umma na mashirika ya Serikali, ukiakisi mchango mkubwa wa TFS katika kuongeza mapato ya Serikali kupitia usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki.

TFS - Kituo Cha Mbegu za Miti tulipata nafasi  ya kuwatembelea wadau wetu Chuo Cha Ualimu  Dakawa na Muhonda .Tumewatemb...
12/06/2026

TFS - Kituo Cha Mbegu za Miti tulipata nafasi ya kuwatembelea wadau wetu Chuo Cha Ualimu Dakawa na Muhonda .Tumewatembelea Kuona maendeleo ya miche ambayo tulipanda mwezi February 2026 .Miche imestawi na inaendelea vizuri ,Aidha Makamu mkuu wa Chuo ameendelea kutoa shukran kwa kuwatembelea na Kuona maendeleo ya upandaji wa miti iyo chuoni hapo .

26/05/2026
30/04/2026

TFS YATOA MICHE 500, YAONGOZA MAPAMBANO YA UHIFADHI BWAWA LA MINDU

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MOROGORO — Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kupitia Kituo cha Uzalishaji Mbegu za Miti Morogoro, umetoa miche 500 ya miti ya midodoma na kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti katika hifadhi ya chanzo cha maji cha Bwawa la Mindu, ikiwa ni juhudi za kulinda usalama wa maji kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro na maeneo jirani.

Zoezi hilo la pamoja limewakutanisha watumishi wa umma, wastaafu kutoka taasisi mbalimbali pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa na lengo la kurejesha na kuhifadhi vyanzo vya maji vinavyotegemewa na zaidi ya wakazi 500,000.

Akizungumza kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji Mbegu za Miti Morogoro, Mhifadhi Mwandamizi (SCO) Helman Ndanzi amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa TFS katika kuimarisha uhifadhi wa mazingira, hususan katika maeneo nyeti ya vyanzo vya maji.

Amesisitiza kuwa uhifadhi wa mazingira haupaswi kuachwa kwa taasisi moja pekee bali unahitaji ushirikiano wa wadau wote, akibainisha kuwa TFS itaendelea kusambaza miche bora na kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha juhudi hizo zinakuwa endelevu.

Kwa upande wake, Meneja wa Mazingira na Usafi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), Mhandisi Hafidhi Lacha amesema zoezi hilo linaendana na maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, akieleza kuwa upandaji miti ni nguzo muhimu katika kulinda vyanzo vya maji.

“Uwepo wa miti katika maeneo ya vyanzo vya maji unasaidia kuhifadhi unyevunyevu wa ardhi, kuzuia mmomonyoko na kuhakikisha upatikanaji wa maji unaendelea kuwa wa uhakika kwa wananchi,” amesema.

Naye Diwani wa Viti Maalum (CCM) wa Kata ya Maghorofani, Immaculate Mhagama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauguzi Wastaafu, ametoa wito kwa jamii na makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kampeni za upandaji na utunzaji wa miti ili kulinda mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema ushiriki wa wananchi ni nguzo muhimu katika kufanikisha juhudi za uhifadhi na kwamba kila mmoja ana wajibu wa kutunza miti inayopandwa ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya yaliyokusudiwa.

Zoezi hilo linaakisi dhamira ya Serikali kupitia TFS na wadau mbalimbali katika kuhakikisha rasilimali za misitu na maji zinalindwa kwa manufaa ya maendeleo endelevu ya taifa.

30/04/2026

TFS YASHIRIKI UZINDUZI MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA MOROGORO

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Kituo cha Uzalishaji wa Mbegu za Miti, wameshiriki uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi mazingira unaotekelezwa na Shirika la UECO – Unganisha Environmental Conservation kwa kushirikiana na mradi wa Imarika chini ya Mtandao wa PELUM Tanzania.

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 17 Aprili 2026 katika Kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro, ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Mheshimiwa M***a Kilakala.

Katika uzinduzi huo, jumla ya mizinga 50 ya kisasa iligawiwa kwa vikundi vya vijana na wanawake kutoka mitaa inayozunguka Mlima wa Mguruwandege ambayo ni Mawasiliano, Kilongo, Kilongo B na Mguruwandege, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha wananchi kiuchumi sambamba na kuhifadhi mazingira.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Kilakala alisisitiza umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa kutumia mbinu endelevu k**a ufugaji nyuki na upandaji miti, ambazo huchangia kulinda vyanzo vya maji na bioanuwai huku zikitoa kipato kwa wananchi.

Akimwakilisha Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji Mbegu za Miti, Mhifadhi Herman Ndazi alisema TFS itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora za miti na kuhamasisha upandaji miti katika maeneo ya hifadhi na nje ya hifadhi ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira.

Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii ni nguzo muhimu katika kufanikisha juhudi za uhifadhi wa misitu na mazingira kwa ujumla.

Mradi huo unalenga kuimarisha uhifadhi wa Mlima wa Mguruwandege kwa kuwajengea uwezo wananchi katika shughuli mbadala za kiuchumi ambazo haziharibu mazingira, hivyo kuchangia maendeleo endelevu ya jamii zinazouzunguka mlima huo.

Usikose  kupanda mti.
26/01/2026

Usikose kupanda mti.

Address

Kihonda
Morogoro
373

Opening Hours

Monday 07:30 - 17:30
Tuesday 07:30 - 17:30
Wednesday 07:30 - 17:30
Thursday 07:30 - 17:30
Friday 07:30 - 17:30
Saturday 08:00 - 12:00
Sunday 09:00 - 12:00

Telephone

+255232935617

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TFS-Tree seed Production posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share