16/07/2019
Ziara ya Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kilosa kata kwa kata katika MAANDALIZI ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo baadae
Katika Ziara hiyo Katibu Wa CCM Wilaya comrade AZIZA Aziza Isimbula amembatana na Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg Jafari Kunambi, Katibu wa UVCCM Wilaya ndg Philbert Kipenda, Katibu wa UWT Wilaya ndg Agnes Chuma pamoja na Katibu wa WAZAZI Wilaya Bi Scholastica Salim
Katika Ziara Sekretarieti imeendelea kuhimiza umoja baina ya Wana CCM, kuvunja makundi hasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini pamoja na kuendelea kuhimiza juu ya watu wenye sifa kujitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali na kwamba Chama hakitambeba mgombea asiye na sifa
AIDHA Chama kimeendelea kuhimiza juu ya umuhimu wa mabalozi katika kuwaweka wanachama pamoja na kwamba kinatambua thamani ya mabalozi wake wote ndani ya Chama kwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa mno kuhakikisha CCM inashinda