Tanzania Forestry Research Institute

Tanzania Forestry Research Institute Tanzania Forestry Research Institute (TAFORI) was established by Act No. 5 of 1980.

Kazi na Utu Tunasonga Mbele
01/09/2026

Kazi na Utu Tunasonga Mbele

☪️🌙
25/08/2026

☪️🌙

08/08/2026

Ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Palamagamba Aidan Kabudi (Mb) Banda la TAFORI na TFS Maonesho ya Nanenane Morogoro.

07/08/2026

Mkurugenzi Mkuu TAFOR Afanya ziara Banda la TAFORI na TFS, Maonesho ya Nanenane, awasihi wadau na wananchi wote kutumia matokeo ya tafiti za misitu na nyuki kijikwamu kiuchumi na kuongeza kipato.

NAIBU WAZIRI CHANDE AITAKA TAFORI KUENDELEA KUCHOCHEA UBUNIFU KUPITIA UTAFITIMorogoro | Agosti 7, 2026. Naibu Waziri wa ...
07/08/2026

NAIBU WAZIRI CHANDE AITAKA TAFORI KUENDELEA KUCHOCHEA UBUNIFU KUPITIA UTAFITI

Morogoro | Agosti 7, 2026. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande (Mb), ameihimiza Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kuendelea kufanya tafiti katika sekta ya misitu na ufugaji nyuki ili kuchochea ubunifu na kuongeza tija katika sekta hizo.

Mhe. Chande ametoa wito huo leo alipokuwa akitembelea banda la TAFORI na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Morogoro, ambapo alipata fursa ya kupata elimu na kujionea ubunifu wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao ya misitu na ufugaji nyuki.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri pia amepata fursa ya kujionea shughuli za utafiti na uhifadhi zinazofanywa na taasisi hizo, pamoja na matokeo ya tafiti yanayowasilishwa kupitia bidhaa na huduma mbalimbali za kitaifiti.

Maonesho ya Nanenane, yanaongozwa na kaulimbiu “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.”

06/08/2026

KARIBU UJIFUNZE NAMNA UFUGAJI NYUKI UNAWEZA KUINUA KIPATO CHAKO.

06/08/2026

MAONESHO YA NANENANE 2026 KARIBU TUKUHUDUMIE

MENEJA KITUO CHA TAFORI KIBAHA AFANYA ZIARA BANDA LA TAFORI NANENANEMorogoro | Agosti 5, 2026. Meneja wa Kituo cha Utafi...
05/08/2026

MENEJA KITUO CHA TAFORI KIBAHA AFANYA ZIARA BANDA LA TAFORI NANENANE

Morogoro | Agosti 5, 2026. Meneja wa Kituo cha Utafiti TAFORI Kibaha, Dkt. Nancy Pima, leo ametembelea banda la TAFORI katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, Morogoro, kwa lengo la kujionea shughuli za utafiti zinazotolewa na taasisi kwa wadau wa sekta ya misitu na ufugaji nyuki.

Katika ziara hiyo, Meneja Dkt. Pima amepata nafasi ya kuona namna matokeo ya tafiti yanavyowasilishwa kwa wadau katika maonesho hayo, yanayolenga kuunganisha watafiti na wadau pamoja na kuhamasisha matumizi ya matokeo ya utafiti katika kuongeza tija katika sekta hizo.

TAFORI YATOA ELIMU YA UTAFITI KUONGEZA TIJA KATIKA MASHAMBA YA MITI NANENANENanenane, Morogoro. Taasisi ya Utafiti wa Mi...
05/08/2026

TAFORI YATOA ELIMU YA UTAFITI KUONGEZA TIJA KATIKA MASHAMBA YA MITI NANENANE

Nanenane, Morogoro. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imeendelea kutumia Maonesho ya Wakulima Nanenane, kuwaelimisha wakulima wa mashamba ya miti kuhusu matumizi ya matokeo ya utafiti katika kuongeza ubora na tija ya shughuli zao.

Kupitia maonesho hayo, TAFORI imetoa elimu kwa wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia umri sahihi wa uvunaji wa miti, ili kupata mbao zenye ubora zinazoweza kutumika katika ujenzi na utengenezaji wa samani.

Aidha, wadau wamepatiwa elimu kuhusu namna ya kutambua na kukabiliana na magonjwa na wadudu wanaoweza kusababisha miti kudhoofika, kukauka, pamoja na kanuni za msingi za upandaji na utunzaji wa miti kwa kuzingatia aina ya udongo na mazingira ya eneo husika.

TAFORI imeeleza kuwa matokeo ya tafiti yanaonesha umuhimu wa kuzingatia eneo linalofaa kwa kila aina ya mti, kwa kuwa si kila aina ya mti inafaa kupandwa katika kila eneo. Uelewa huo unalenga kuwasaidia wakulima kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi wa aina za miti na maeneo ya kuipanda.

Maonesho ya Nanenane yanaongozwa na kaulimbiu “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”.

Katika Maonesho ya Nanenane 2026, TAFORI inakuletea maarifa ya utafiti yanayoweza kubadili namna unavyofanya shughuli za...
05/08/2026

Katika Maonesho ya Nanenane 2026, TAFORI inakuletea maarifa ya utafiti yanayoweza kubadili namna unavyofanya shughuli za misitu na ufugaji wa nyuki.

🌳 *Unamiliki shamba la miti?*
Jifunze mbinu bora za kupanda, kutunza na kusimamia mashamba ya miti kwa tija zaidi.

🐝 *Unataka kufuga nyuki kibiashara?*
Fahamu aina za nyuki, mazingira yanayofaa kwa ufugaji na mbinu zinazoweza kukusaidia kuongeza uzalishaji wa asali yenye ubora.

📚 *Unahitaji maarifa ya kuaminika?*
Pata majarida, machapisho ya utafiti na miongozo mbalimbali kuhusu kilimo cha miti na ufugaji wa nyuki.

Kutana na wataalamu wa TAFORI katika banda letu, uliza maswali yako, pata ushauri na gundua ubunifu unaotokana na tafiti za misitu na ufugaji nyuki.

📍Karibu TAFORI – Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Morogoro.

*Usipite Nanenane bila kutembelea TAFORI.*

Tafiti Leo, kwa Maendeleo ya Kesho.🌱

Address

Kingolwira
Morogoro

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Telephone

+255232604532

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Forestry Research Institute posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Forestry Research Institute:

Shortcuts

Share