Bavicha Hai

Bavicha Hai Ukurasa Maalam wa Baraza la Vijana Chadema Hai (BAVICHA- Hai).

Asanteni Watanzania kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 236.6, na sasa tumebakiza T...
27/07/2026

Asanteni Watanzania kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 236.6, na sasa tumebakiza TSh. Milioni 97.4 pekee kufikia lengo letu la TSh. Milioni 334 kwa ajili ya Baraza Kuu la Umma.

CHANGIA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo

22/07/2026

Mhe. Tundu Lissu akiwasili mahakamani leo ambapo Shauri linalohusu vikwazo vya kumwona gerezani litaendelea.

TUENDELEE KUCHANGIA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo

23/06/2026

“Said Issa Mohamed na wenzake wameisababishia Chadema hasara ya zaidi ya bilioni 100 na mawakili wao wameshiriki kusababisha hiyo hasara. Tutawasaidia waweze kulipa kwa namna inavyostahiki.” – Mhe. Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa Chama.

23/06/2026

Chimala.

14/06/2026

Anaandika Mhe. NTELE Benjamin, Katibu wa Kanda ya Pwani

"Tanzania tuna matatizo mengi ila Tatizo la Ukosefu wa Maji hasa katika Jiji la Dsm ni tatizo la aibu kubwa sana.

Mwenyezi Mungu ametupatia neema tuna Mito Mikubwa inayoturirisha Maji masaa 24, Tuna maziwa Makubwa zaidi ya 5 lakini ardhi ya dsm ina maji ya Kutosha ila Serikali imeshindwa kupata ufumbuzi wa mtego huu wa umaskini.

hatuoni Jitihada zozote wanazozifanya Kuhakikisha Changamoto hii inatatuliwa kabisa badala yake wamekua watu wa excuse kila mara.

Ni aibu kuwa na Wizara ya Maji tena ina Wakurugenzi na watendaji Kila Mkoa,Wilaya hadi Kata wanaolipwa kwa Kodi za wananchi ila wanashindwa Kutatua Kero ya Maji miaka zaidi ya 69 ya Uhuru.

Waziri wa Maji ni muhimu utueleze Changamoto ya Maji itakoma lini hasa katika Jiji la Dsm na Maeneo Mengi pamoja na mpango mahususi wa kumaliza Changamoto hiii ya aibu."

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuuarifu umma kuwa shauri la Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati...
10/06/2026

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuuarifu umma kuwa shauri la Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Tundu Antiphas Lissu, ambalo lilipangwa kuendelea kesho, tarehe 11 Juni 2026, limeahirishwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania, shauri hilo sasa limepangwa kwa ajili ya Judgments, Rulings & Orders siku ya Jumatatu, tarehe 6 Julai 2026, saa 3:00 asubuhi.

Leo, tarehe 07 Juni 2026, Kamati Maalum ya CHADEMA Zanzibar imeketi katika kikao chake kilichofanyika Kisiwani Pemba. Ki...
07/06/2026

Leo, tarehe 07 Juni 2026, Kamati Maalum ya CHADEMA Zanzibar imeketi katika kikao chake kilichofanyika Kisiwani Pemba. Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Said Mzee Said, na kuhudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika.

Kikao hicho kinajikita katika kujadili hali ya siasa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla, kwa lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa kisiasa na kuweka mwelekeo wa hatua za chama katika kipindi kijacho.

Aidha, kikao hicho kinajadili na kupitisha Mpango Mkakati wa CHADEMA Zanzibar wa miaka mitano, utakaokuwa mwongozo wa utekelezaji wa shughuli, sera na vipaumbele vya chama kwa kipindi husika.

“Tutahakikisha kwamba wajumbe wa taasisi za uchaguzi wako huru. Chadema itazifanya taasisi za uchaguzi kuwa zao la Katib...
05/06/2026

“Tutahakikisha kwamba wajumbe wa taasisi za uchaguzi wako huru. Chadema itazifanya taasisi za uchaguzi kuwa zao la Katiba katika Katiba ya Wananchi ili kuhakikisha kuna chaguzihuru na za haki na ambazo haziingiliwi kwa namna yoyote ile”

09/04/2026

Hivi ndivyo Mhe. Tundu Lissu alivyokamatwa na Jeshi la Polisi tarehe 09 Aprili 2025 katika Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma akiendelea na Oparesheni .

Mhe. Lissu leo ametimiza siku 365 (mwaka mmoja) tangu akamatwe.

11/02/2026

Shangwe la kumlaki Mwenyekiti CHADEMA Mh Tundu Lissu akiingia katika ukumbi wa Mahakama Kuu leo 11.02.2026.
Raisi, Raisi, Raisi......

Address

Chademahai@gmail. Com
Moshi
25312

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bavicha Hai posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share