12/10/2021
JE UNAFAHAMU KUNA MAKUNDI KADHAA YA KUUMA KICHWA❓*
Na makundi hayo yamegawanywa ifuatavyo kutokana na visababishi.
¶. Maumivu ya kichwa ya awali (Primary headache)
- Haya ni maumivu ambayo husababishwa na kuongezeka kwa hisia za maumivu katika viungo vinavyotaambua maumivu ndani ya ubongo.
Maumivu haya ya awali hayamaanishi kuwa kuna ugonjwa unaendelea.
Mfumo wa kemikali katika ubongo, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu ya nje ya fuvu ama misuli ya shingo na kichwa huchangia katika kusababisha maumivu ya kichwa ya awali.
Baadhi ya watu wamebeba vinasaba vinavyosababisha wao kupata maumivu haya maishani mwao.
Aina hii ya maumivu ya kichwa nayo imegawanyika katika makundi makubwa mawili
1. Kipandauso (Migrain)
- Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali ndiyo iliyoenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili.
- Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo.
Aina hii ya maumivu ya kichwa huwa ni ya “kichwa kugonga” (throbbing pain) na huambatana na dalili k**a vile kichefuchefu au kutapika, kizunguzungu, macho kushindwa kuona vizuri, macho kuuma yanapoangalia mwanga.
- Aina hii ya maumivu ya kichwa huzidishwa na kutembea au kujisogeza kwa namna yoyote, na mgonjwa hujisikia nafuu akipumzika/kulala kwa kawaida, maumivu haya huwa makali kwa muda wa masaa 1-2, na yanaweza kuchukua kati ya saa 4 hadi 72.
Vitu ambavyo huweza kusababisha mtu mwenye tatizo la migraine kuanza kuumwa kichwa (triggers) ni k**a vile vinywaji vyenye kemikali ya caffeine au pombe/sigara, mawazo, uchovu/usingizi, hasira, kwa kinadada k**a akiwa anakaribia siku zake, au kwenye siku zake, mwanga mkali/sauti.
- Aina hii ya maumivu ya kichwa pia huwasumbua zaidi wanawake ambao wako katika umri wa kuweza kushika mimba ambao ndio wameanza kupata hedhi zao kipindi cha karibuni.
Pia migraine huweza kurithiwa kutoka kwa wazazi kwa sababu mara nyingine husababishwa na vitu ambavyo viko kwenye vinasaba (genetics) za uzao husika.
Pia aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hutanguliwa na dalili za kabla (aura), ambazo hutokea kwa kati ya dakika 5-20, na hudumu si zaidi ya dakika 60; dalili hizi za kabla zinaweza kuwa kizunguzungu, kichefuchefu,mwili kukosa nguvu, n.k.
Maumivu mkazo (Tension Headache
Aina hii ya maumivu ya kichwa kwa kawaida huwa ni ya ‘kugandamiza/kukaza (pressing/tightening), na huwa yanatokea kwenye pande zote za paji la uso kuelekea utosin (frontal-occipital) na hayazidi pale mgonjwa anapotembea/kujisogeza (tofauti na migraine).
Aina hii ya maumivu ya kichwa yanaweza kudumu kwa kati ya dakika 30 hadi siku 7; Na hayaambatani na dalili za kichefu-chefu/kutapika/kizungu-zungu k**a ilivyo kwa migraine!! Pia hakuna dalili za awali (aura).
Mara nyingi maumivu haya huanza pale mtu anapokuwa na msongo wa mawazo; na huambatana na kukosa usingizi (insomnia).
2. Maumivu ya kichwa ya upili (Secondary headache)
- Aina hii ya maumivu ya kichwa husababishwa na tatizo lingine amblo lipo ndani ya mwili na mgonjwa hupata maumivu haya k**a matokeo ya tatizo hilo lingine mwilini.
Maumivu ya kichwa ya aina hii kwa kawaida huambatana na dalili zingine ambazo nazo zimekuwa zimesababishwa na tatizo la msingi.
Dalili hizo ni;
~ Maumivu ya viungo/mifupa
~ Kuishiwa damu
,~ Homa,
~Kupungua uzito
~Dalili za mfumo wa fahamu (kuchanganyikiwa, kuzimia, kupungua kwa hali ya ufahamu, macho kushindwa kuona, mwili au sehemu ya mwili kupooza)
~ Maumivu mapya ya kichwa kwa mtu mwenye umri wa miaka 50 na zaidi ambaye hakuwahi kuwa na tatizo la maumivu ya kichwa
Historia ya kuwahi kuumia kichwa/kupata ajali ya kichwa.
Mara nyingi, visababishi vya maumivu ya aina hii ya kichwa huwa ni k**a ifuatavyo,
~ Presha ya kupanda/kushuka,
~ matatizo ya mishipa ya fahamu,
~ Maambukizi ya bakteria/virusi
~ Upungufu wa maji mwilini (dehydration)
~ Saratani ya ubongo,
~ Matatizo ya macho,
~ Kiharusi.
~ Damu kuvilia kwenye ubongo
⚠️TUNALO SULUHISHO...NIELEZE NIKUSAIDIE
Piga simu 0623992857 au njoo moja kwa moja WhatsApp