Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi

Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Katavi.

07/07/2026

06/07/2026

VIDEO: Kwa Watu wenye changamoto za Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo tunawakaribisha katika Hospitali yetu kwani tunatoa huduma za matibabu ya Kibingwa, Karibuni sana tuwahudumie.

  from   Leo tarehe 25,Juni,2026 Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Vitiligo.
25/06/2026

from Leo tarehe 25,Juni,2026 Tanzania inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Vitiligo.

Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Dharura na Maafa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na CIHEB Tanzani...
24/06/2026

Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Dharura na Maafa kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na CIHEB Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani pamoja na wadau wa sekta ya afya, inaendelea kuimarisha huduma za dharura, ajali na uangalizi wa wagonjwa mahututi nchini kupitia usimamizi shirikishi na mafunzo kwa vitendo ya utayari dhidi ya ugonjwa wa Ebola yanayotolewa sehemu ya kazi kwa watumishi wa afya wanaohudumu katika Idara za Dharura (EMD) na Wagonjwa Mahututi (ICU).

Jitihada hizo zinalenga kuongeza uwezo wa kitaalamu kwa watoa huduma za afya ili kuboresha utayari, ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa wakati wa matukio ya dharura za afya, ikiwemo utambuzi wa mapema, kinga dhidi ya maambukizi, utoaji wa huduma salama pamoja na hatua za awali za kukabiliana na wagonjwa wanaohisiwa kuwa na Ebola.

Aidha, zoezi hilo ni mwendelezo wa mpango wa kitaifa unaolenga kuendelea kujenga uwezo wa watumishi wa afya nchini kupitia mafunzo ya vitendo na usimamizi wa karibu unaowezesha matumizi sahihi ya miongozo na taratibu za huduma za dharura.

Mafunzo haya yamefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo watumishi wa afya wanaendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo yanayolenga kuimarisha utayari dhidi ya Ebola, matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga pamoja na utoaji wa huduma kwa kuzingatia usalama wa mtoa huduma na mgonjwa.

Sambamba na hilo, mafunzo hayo yanaendelea kuwawezesha watumishi wa afya kuimarisha ujuzi wa kitaaluma, kubadilishana uzoefu na kuongeza uwezo wa vituo vya kutolea huduma kukabiliana na changamoto mbalimbali za afya ya umma na dharura zinazoweza kujitokeza nchini.

23/06/2026

Je, Unafahamu dalili za ugonjwa wa Ebola zinaweza kuanza kujitokeza baada ya muda gani?

Sikiliza ujumbe huu kutoka .

18/06/2026

VIDEO: "SERIKALI IMEIMARISHA ULINZI WA AFYA MIPAKANI KUDHIBITI EBOLA", Amesema Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Juni 18, 2026 akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu tathmini ya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania na hali ilivyo kwa sasa.

© CrownTV

17/06/2026

VIDEO: "Adhabu kali kwa Watoto inaweza kupelekea changamoto ya afya ya akili", Dr. Edward Bucheye, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Kwa changamoto zozote zile za afya ya akili, Karibu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi upatiwe ushauri, uchunguzi na matibabu.

12/06/2026

VIDEO: AJIFUNGUA PACHA WANNE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI.

Karibu Katavi RRH upate huduma za Kibingwa za uzazi na Magonjwa ya Akina Mama.

11/06/2026

m-mama imepanua wigo wa utoaji wa huduma za usafiri wa dharura kwa akina Mama na Watoto wachanga. Kwa kupata huduma hii Piga 115 Bure.

Kutana na Dr. Lemmy Kasungu kwenye Kliniki ya Kibingwa ya Magonjwa ya Akina Mama kila siku Jumatatu hadi Ijumaa.
10/06/2026

Kutana na Dr. Lemmy Kasungu kwenye Kliniki ya Kibingwa ya Magonjwa ya Akina Mama kila siku Jumatatu hadi Ijumaa.

Address

P. O BOX
Mpanda
449

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hospitali Ya Rufaa Mkoa Katavi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share