26/01/2026
FANYENI KAZI KWA MALENGO - BI. JULIANA MANYAMA
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Mtwara - Mikindani Bi. Juliana Manyama amewahimiza maafisa usafirishaji wa manispaa hiyo kufanya kazi kwa kujiwekea malengo ili kujikwamua kiuchumi.
Bi. Manyama Ameyasema hayo leo tarehe Januari 26, 2026 katika mafunzo ya Ujasiliamali kwa vikundi vya maafisa Usafirishaji ( Bodaboda) vilivyoomba mkopo katika Manispaa hiyo.
Aidha, amewasihi maafisa hao kuzingatia usalama wa abiria na wao wenyewe pamoja na kuwa na uadilifu na kutumia lugha nzuri kwa wateja wao.
Kwa upande wake, Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Bi. Mary Mwakyosi amewataka maafisa hao kuwa waaminifu katika marejesho ya mikopo itakayotolewa na Manispaa hiyo pamoja na Kuwaasa maafisa hao kuwa na ushirikiano mzuri baina ya wao na serikali.
Sambamba na hilo, amewataka maafisa hao kujiwekeza katika kumiliki ardhi kupitia biashara yao na kuhakikisha kipato kinakuwa kikubwa kuliko matumizi.