03/09/2026
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, ameeleza kuridhishwa na kazi inayofanywa na timu ya mpira wa wavu ya Korosho Queens, baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano 2026 lililofanyika Zanzibar.
Akizungumza Septemba 3, 2026, Mtwara, wakati timu hiyo ilipomkabidhi kombe hilo, ameitaka Korosho Queens kuendelea kuwa balozi wa tasnia ya korosho kwa kuhamasisha ulaji wa korosho, ubanguaji na matumizi ya bidhaa zitokanazo na zao hilo.
Kwa upande wake, Meneja wa timu, Hussein Kibombwe, amesema kauli mbiu ya “Kula Korosho kwa Afya” imeendelea kuleta matokeo chanya, huku Korosho Queens ikiendelea kutumia michezo na matukio mbalimbali kuitangaza tasnia ya korosho na kuhamasisha jamii kuhusu faida za ulaji wa korosho.
,
.cashew.go.tz