04/05/2016
Nimetumiwa na Mtu:
STORI FUPI YA KUCHÉKESSHA
Siku moja nikiwa stand ya mabasi nikiwa naenda kumsindikiza rafiki yangu....nikamuona binti mrembo saana! Aliyevaa nguo za thamani kubwa sana yaani ukimuangalia huna haja ya kujiuliza mara mbili kuwa huyu ni tajiri au mtoto wa tajiri flani ...basi yule binti mrembo alishuka katika gari ya bei mbaya Range Rover SUV huku akiwa analia...na akiwa amempigia magoti mkaka mmoja mchafu aliyedhoofu sana inaonyesha labda alikuwa hapati chakula yaani ukimuangalia haraka huwezi kumtofautisha na wale waokota vyakula barabarani...basi yule dada mrembo akiwa kapiga magoti alianza kumbembeleza yule kaka "mimi sitaki pesa , sitaki nyumba, staki wigs, staki brazillian yaani staki chochote kutoka kwako bali ninachotaka ni penzi lako tu,busu lako tu,na joto lako tu..huyu dada mrembo alitamka maneno haya kwa hisia sana hulu akilia kilio si cha kitoto, nilipoyasikia hayo maneno ya huyo dada kwanza sikuamini, pili nilichanganyikiwa kabisa sababu huyo kaka chokoraa hata habari hakuwa nayo na alikuwa hata hamtizami japo usoni huyo dada mrembo, nikasema huu upuuzi sasa huyu kaka k**a hampendi huyu dada na kashindwa kumwelewa na kuthamini pendo la kweli la yule dada... dadeki mi kidume najitosa kwa huyu dada liwalo na liwe!.....nikatoka pale niliposimama nikaelekea alipo yule msichana alipopiga magoti ili nikafanye yangu maana mrembo alitia huruma hatari......nikamfikia yule mrembo...mara mkaka mmoja akanishika bega...unajua alichonambia??OYAA WE JAMAA UNAZIBA CAMERA WE HUONI TUNASHOOT FILAM HAPA.....😂😂😂Ungekuwa wewe ungefanyaje?? Mimi nusura nizimieee