Kwimbadc

Kwimbadc Ijue Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba,
Matukio mbalimbali na Miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani Kwimba.

KWIMBA YAPONGEZWA KWA KUONGOZA MATUMIZI MAZURI YA MFUMO WA MANUNUZI (NeST)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya y...
09/02/2024

KWIMBA YAPONGEZWA KWA KUONGOZA MATUMIZI MAZURI YA MFUMO WA MANUNUZI (NeST)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga apokea tuzo, baada ya Halmashauri ya Kwimba kuongoza Kitaifa katika matumizi mazuri ya mfumo wa manunuzi NeST, tuzo hiyo imetolewa na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Akikabidhi tuzo hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Mfumo wa Taifa wa Manunuzi wa Kielektroniki (NeST) hauna mbadala katika kufanya mchakato wa manunuzi kwenye ngazi ya halmashauri.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo leo jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba iliyoibuka kinara nchini katika matumizi ya Mfumo wa Taifa wa Manunuzi wa Kielektroniki (NeST).

Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa halmashauri na taasisi zinazolegalega kutumia mfumo wa NeST kuanza kuutumia kwani hakuna mbadala, hivyo watendaji wote walio chini ya OR-TAMISEMI wanapaswa kujifunza na kuutumia kikamilifu.

Ameongeza kuwa, kitendo cha Halmashauri ya Kwimba kupata tuzo ni somo kwamba hakuna mjadala kuhusu matumizi wa mfumo wa NeST kwa halmashauri zote zilizopo pembezoni ambazo husingizia changamoto ya mtandao.

“Halmashauri ya Kwimba ipo mbali lakini imefanikiwa katika matumizi ya mfumo wa NeST hivyo sijui ni kwanini Halmashauri zilizopo mijini zinashindwa kuutumia mfumo huu wakati wana umeme na mitandao wa uhakika,” Waziri Mchengerwa amehoji.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amemtaka Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuzielekeza Halmashauri zote kuhusu matumizi ya mfumo wa NeST.

Mfumo wa Taifa wa Manunuzi wa Kielektroniki (National e-Procument System of Tanzania-NeST) unasimamiwa na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma(PPRA).

UZINDUZI KITUO CHA AFYAZaidi ya wakazi elfu kumi na tisa wa kata ya Sumve na kata Jirani wanatarajiwa kuondokana na adha...
06/01/2024

UZINDUZI KITUO CHA AFYA

Zaidi ya wakazi elfu kumi na tisa wa kata ya Sumve na kata Jirani wanatarajiwa kuondokana na adha ya kupata huduma za afya baada ya kukamilika kwa kituo cha afya Budushi kilichopo wilayani Kwimba mkoani Mwanza

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija amezindua kituo hicho cha afya pamoja na jengo la wodi ya wanaume na wanawake na kuwataka wakazi hao kukitumia kwa ajili ya kupata huduma na kuacha Kwenda kwa waganga wa kienyeji pindi wanapougua

“Ndugu zangu wananchi wa Sumve kituo hiki ni mali yenu lakini mmeletewa watalaamu na Rais Samia anahakikisha kila sehemu kinapojengwa kituo cha afya kunakuwa na watalaamu na dawa za kutosha kwa ajili yenu kupata huduma za afya kwahiyo mnapoumwa msisite kuja kupatiwa matibabu hapa”amesema Ludigija

“Nimeingia kwenye chumba cha dawa nimeona vyandarua nimeambiwa na mfawidhi ni kwa ajili ya wajawazito watakapokuja kliniki sasa ukipewa chandarua hakikisha unakitumia kwa matumizi yanayotakiwa na kuacha kutumia kwa ajili ya kutega Samaki”

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kwimba Hapiness Msanga amewashukuru wakazi wa kata hiyo kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya na kusema jengo la OPD limejengwa kwa fedha za ndani shilingi milioni 160, matundi Matano ya vyoo shilingi milioni 12.5, majengo matatu yamejengwa kwa fedha za TASAF ambayo ni jengo la maabara lililogharimu shilingi milioni 90.6, jengo la wazazi milioni 136.4, la upasuaji milioni 139

katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Kwimba amewataka wazazi wote kuhakikisha jumatatu shule zinapofunguliwa wanawapeleka shule watoto waliofikisha umri wa Kwenda shule na kuwaonya watakaojaribu kukiuka agizo hilo

“Rais analeta fedha amesema diwani wenu namna fedha zilivyoletwa za kujenga madarasa sasa wapelekeni watoto wenu shule, ni marufuku kuwakatisha watoto Kwenda shule na kuwapeleka kupanda mipunga sasa watakaojaribu kuwaacha watoto nyumbani sitawaacha salama”

MKURUGENZI AWATA WAKUU WA SHULE NA WATENDAJI KUSHIRIKIANAMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happ...
27/12/2023

MKURUGENZI AWATA WAKUU WA SHULE NA WATENDAJI KUSHIRIKIANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewataka wakuu wa shule, walimu wakuu na watendaji wa Kata na vijiji kuhakikisha wanashirikiana katika kutekeleza majukumu ya kusimamia miradi na taaluma.

Ameyasema hayo leo Desemba 27,2023 katika kikao kazi cha Walimu wakuu, wakuu wa shule na watendaji kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Ngudu

"tunaenda Januari shule zinafunguliwa, hakikisheni Walimu mnashirikiana na watendaji ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni kwa wakati" amesema Msanga

Mkurugenzi huyo amehamasisha ushirikiano baina ya viongozi hao ili kutokomeza utoro na kuongeza kasi ya ufaulu wa wanafunzi.

Aidha amewataka walimu ambao shule zao zimefanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba zikiongozwa na shule ya msingi Dodoma ambayo imekuwa ya mwisho Kiwilaya kujitafakari na kubadirisha namna ya ufundishaji ili mitihani ijayo wafanye vizuri.

Pia amewapongeza walimu ambao shule zao zimefanya vizuri zikiongozwa na Shule ya Msingi Ilula ambayo imeingia kumi bora za Mkoa wa Mwanza.

Katika kikao hicho Mkurugenzi amekabidhi Komputa 16 na projekta mbili kwa Walimu wa shule ya msingi Malya na Bupamwa ( kila shule komputa nane na projekta moja) ambapo shule hizo zimeteuliwa kuwa mahali pa kujiongezea ujuzi kwa walimu wote wa msingi na Sekondari.

Walimu walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi

" sisi watumishi tulioshiriki kikao hiki tunaahidi kwenda kutekeleza maagizo yote na maelekezo yaliyotolewa, pia tutaongeza ushirikiano katika kuboresha elimu" amesema Mwalimu Mponeja Maduka Afisa elimu Kata ya Ngudu

15/12/2023
ZAIDI YA KAYA 7000 ZA TASAF KUFANYIWA UHAKIKISerikali imeendelea kuboresha maisha ya walengwa wa kaya masikini TASAF kwa...
14/12/2023

ZAIDI YA KAYA 7000 ZA TASAF KUFANYIWA UHAKIKI

Serikali imeendelea kuboresha maisha ya walengwa wa kaya masikini TASAF kwa kuendelea kuwapatia ruzuku ya fedha kila baada ya miezi miwili fedha inayosaidia kujikimu mahitaji yao ya msingi.

Mwaka 2014/15 Serikali ilianzisha mpango wa Tasaf katika vijiji 86 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ambavyo leo Desemba 14,2023 vimeanzà kufanyiwa tathimini na uhakiki ili kubaini k**a fedha wanazopata kupitia ruzuku ya Tasaf zimewainua kiuchumi au la!

' lengo la kufanya uhakiki ni kubaini kaya zilizoimarika kiuchumi na zilizokizi vigezo vya kuondolewa kwenye mpango" amesema Elias Onesmo, Muwezeshaji

Muwezeshaji huyo amewataka walengwa wote watakaohojiwa kutoa taarifa sahihi ili kurahisisha kazi hiyo

Aidha Onesmo amewashauri walengwa watakaoondolewa kwenye mpango kutokana na vigezo vilivyowekwa wasiwalaumu viongozi wa vijiji kwani kwa mujibu wa vigezo wataondolewa walioimarika kiuchumi tu

" mtakapohojiwa mjibu kwa usahihi na usiseme kitu ambacho hauna maana majibu unayotoa ndiyo yatapelekea wewe kuonekana umekizi vigezo vya kuondolewa kwenye mpango au uendelee kuwemo, semeni ukweli" amesma Onesmo

Naye Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Ndugu Hamis Fundi amesema asilimia kubwa ya walengwa wa kaya maskini bado hawajajiimarisha kiuchumi hivyo kupitia uhakiki huu walengwa wachache watahitimu na kuondolewa kwenye mpango

" walengwa wanafundishwa kuanzisha miradi ya ufugaji, kilimo na biashara ndogondogo ili miradi hiyo iwawezeshe kuwa na kipato cha kudumu lakini wengi bado hawajaanzisha miradi kwahiyo uchumi wao bado haujaimarika, tunatarajia wachache watahitimu lakini wengi wao bado" amesema Hamis Findi

Uhakiki unafanyika katika vijiji 86 ambapo kaya zaidi ya 7745 zinatarajiwa kuhojiwa ili kubaini mabadiriko ya kiuchumi waliyoyapata kupitia ruzuku za Tasaf.

Tangazo
13/12/2023

Tangazo

13/12/2023
Tangazo
13/12/2023

Tangazo

MKUU WA MKOA AZINDUA MIUNDOMBINU YA MABWENI MWAMASHIMBA NA SHULE MPYA YA MWALULYEHOMkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos ...
28/11/2023

MKUU WA MKOA AZINDUA MIUNDOMBINU YA MABWENI MWAMASHIMBA NA SHULE MPYA YA MWALULYEHO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo novemba 28, 2023 amezindua Miundombonu ya Kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Mwamashimba wilayani Kwimba iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.

Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, Mhe. Makalla ameupongeza uongozi wa shule hiyo na halmashauri kwa usimizi mzuri wa Mabweni 3, Vyumba vya Madarasa 8 na Matundu ya vyoo 13 utakaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa na mabweni.

"Nimeona mabweni mazuri yenye mpangilio mzuri wa vitanda, madarasa na matundu ya vyoo vyote kwenye hali ya usafi na unadhifu mzuri, tumieni jitihada hizi za uboreshaji kutulia na kusoma kwa bidii na nina imani baadae tutawapata viongozi wazuri kutoka kwenye shule hii." Makalla.

Vilevile, Mhe. Makalla ameagiza kulindwa kwa eneo la shule hiyo kwa kutambua na kuweka mipaka na kuweka uzio ili kuwalinda wanafunzi na kuepusha migogoro ya ardhi inayosababishwa na wananchi kuingia kwenye maeneo ya taasisi hususani yasiyo na mipaka inayofahamika.

Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amemhakikishia kiongozi huyo wa Mkoa kuwa ufaulu utaongezeka kwani pamoja na kuondoa msongamano wanafunzi kwenye shule hiyo watapata fursa nzuri ya kusoma kwenye mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa wanafunzi wa kidato cha tano na sita wapo zaidi ya Mia 600 lakini kwa uwepo wa mabweni haya hivi sasa kila mwanafunzi atalala kwenye kitanda chake, hakuna tena msongamano bweni wala darasani." Amefafanua Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happness Msanga.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa amezindua Shule mpya ya Msingi Mwalulyeho katika kijiji cha Chasalawi Kata ya Bupamwa iliyojengwa kwa zaidi ya Milioni 250 ambayo imesaidia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kuelekea shule ya Chasalawi.

"K**a mlikua na kiu ya kupata shule, sasa mmejengewa tumeiona ni nzuri yenye samani za kutosha, basi waleteni watoto kwenye hii shule wasome maana hawa 303 wamehamia hivyo wazazi hakikisheni watoto wote wanakuja shule ifikapo mwezi januari 2024 asibaki nyumbani hata mmoja mweye umri wa kuanza shule" amesema Makalla

RC MAKALLA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA JENGO LA UTAWALA KABLA YA DISEMBA 30Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos  Makal...
28/11/2023

RC MAKALLA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA JENGO LA UTAWALA KABLA YA DISEMBA 30

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amemtaka Mkandarasi Kwiyera Interprises Limited kukamilisha ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kufikia Disemba 30,2023 ili awamu zingine za ujenzi ziendelee na kuwapatia watumishi na wananchi huduma nzuri.

Ametoa agizo hilo mapema leo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye wilaya ya Kwimba alipotembelea ujenzi huo unaofanyika kwenye kata ya Ngudu kwa zaidi ya Bilioni 4 ambapo bilioni 1.3 zitatumika kwa awamu ya kwanza.

"Mkandarasi leo umechelewa na umeshaongezewa mara nne muda wa kukamilisha nami kwa kuzingatia ucheleweshaji wa malipo ya fedha kwa mkandarasi huyo nakutaka sasa ukamilishe jengo hili hadi disemba 30 mwaka huu."

Aidha, Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kutenga fedha zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa jengo hilo (Bilioni 1.3 awamu ya kwanza) ambapo amebainisha kuwa litasaidia kuwaweka watumishi kwenye mazingira nadhifu ya kufanyia kazi na wananchi kupata huduma nzuri.

Awali Mkuu wa Wilaya ya kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija alifafanua kuwa Mkandarasi huyo amekua na mwenendo wa kusuasua kwenye ujenzi hadi kufikia hatua ya kuongezewa muda kwa mara tatu baada ya muda wa awali kuisha kwa mujibu wa mkataba pamoja na kupatiwa fedha.

Akikagua hali ya utoaji huduma kwenye Hospitali ya Wilaya iliyojengwa kwa zaidi ya Bilioni 4 kwenye eneo la Icheja kuanzia mwaka 2018/19 CPA Makalla amewapongeza Kwimba kwa kukamilisha ujenzi ambapo wagonjwa zaidi ya 475 wanalazwa kwa mwezi na kusaidia mtiririko wa huduma.

"Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za ujenzi na vifaa vya kisasa, tunatambua kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa afya ila lazima tusimamie matumizi ya lugha nzuri kwa wagonjwa kwani inaleta matumaini hata kabla ya kuanza kutoa huduma yenyewe" Amesisitiza CPA Makalla.

Akitoa taarifa ya Ujenzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Happness Msanga amebainisha kuwa fedha hizo zilitoka kwa ajili ya ukarabati wa iliyokua hospitali ya wilaya eneo la kakora lakini kutokana na ufinyu wa eneo waliamua kujenga hospitali mpya.

Address

Ngudu
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kwimbadc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Kwimbadc:

Share