Tanzania Cotton Board

Tanzania Cotton Board Pamba!!Dhahabu Nyeupe

HERI YA SIKUKUU YA WAKULIMA   2026
08/08/2026

HERI YA SIKUKUU YA WAKULIMA 2026

31/07/2026

SIKUKUU YA MKULIMA 2026.

Tunawatakia wadau wa tasnia ya pamba na Watanzania wote heri ya sikukuu ya Sabasaba na tunawakaribisha katika banda letu...
07/07/2026

Tunawatakia wadau wa tasnia ya pamba na Watanzania wote heri ya sikukuu ya Sabasaba na tunawakaribisha katika banda letu lililopo katika viwanja vya maonesho ya 50 ya Biashara ya kimataifa Sabasaba, Dar es Salaam

   #2026/2027
12/05/2026

#2026/2027

BEI YA PAMBA YAPANDA HADI SHILINGI 1,240 KWA KILO MSIMU WA 2026/2027Igunga, Tabora – Mei 10, 2026Serikali imezindua rasm...
10/05/2026

BEI YA PAMBA YAPANDA HADI SHILINGI 1,240 KWA KILO MSIMU WA 2026/2027

Igunga, Tabora – Mei 10, 2026

Serikali imezindua rasmi msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2026/2027 huku ikitangaza kupanda kwa bei elekezi ya pamba kufikia Shilingi 1,240 kwa kilo kutoka 1150/= ya msimu uliopita wa 2025/26, hatua inayolenga kuongeza motisha kwa wakulima na kuendelea kuimarisha mchango wa zao hilo katika uchumi wa Taifa.

Akizindua msimu huo katika kijiji cha Mwamashimba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mkuu wa wa wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Mtondoo aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha ambaye alikuwa ndiye Mgeni Rasmi amesema ongezeko hilo la bei ni matokeo ya jitihada za Serikali za kuimarisha mfumo wa uzalishaji na masoko ya pamba pamoja na kulinda maslahi ya wakulima nchini.

Amesema Serikali itaendelea kusimamia mfumo wa ununuzi wa pamba kwa uwazi, ushindani na haki ili kuhakikisha wakulima wanapata malipo stahiki kwa wakati pamoja na kuongeza tija katika mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo.

Katika hotuba hiyo, Serikali imewahimiza wakulima kuongeza uzalishaji kwa kutumia mbegu bora, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa ugani na kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza mavuno na ubora wa pamba.

Aidha, Serikali imeeleza kuwa itaendelea kuimarisha uwekezaji katika sekta ya pamba kupitia upatikanaji wa pembejeo za ruzuku, utekelezaji wa programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) pamoja na kuendeleza matumizi ya zana na teknolojia za kisasa katika kilimo.

Kwa upande wake, Bodi ya Pamba Tanzania imesema maandalizi ya msimu wa ununuzi yamekamilika ikiwa ni pamoja na usajili wa wanunuzi, usimamizi wa mizani pamoja na utoaji wa elimu kwa wadau ili kuhakikisha msimu unaendeshwa kwa ufanisi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Serikali, wadau wa sekta ya pamba, vyama vya ushirika, wanunuzi na mamia ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora na kanda ya pamba kwa ujumla.

Kauli mbiu ya msimu wa mwaka 2026/2027 ni:
“Pamba ni Dhahabu Nyeupe: Uwekezaji thabiti kwa tija,ubora na tasnia ya pamba Endelevu.”

10/05/2026

WAKULIMA WAPO TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2026/27

  2026
01/05/2026

2026

MHE. CHONGOLO: UHAKIKA WA PEMBEJEO, MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULETA TIJA YA ZAO LA PAMBAWaziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongo...
19/04/2026

MHE. CHONGOLO: UHAKIKA WA PEMBEJEO, MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULETA TIJA YA ZAO LA PAMBA
Waziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongolo amesema serikali imeboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa kuhakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu.
Ameongeza kuwa juhudi hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Chongolo ameyasema hayo katika mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba uliofanyika tarehe 16 Aprili katika ukumbi wa Jakaya kikwete jijini Dodoma huku kauli mbiu ya mkutano huo ikiwa ni "Nguvu ya pamoja kwa Tasnia ya Pamba Endelevu"

Aidha amesema Sera ya kilimo ya mwaka 2023 inaeleza kwamba kila kijiji kinatakiwa kuwa na Afisa ugani mmoja ambapo Dhamira ya Serikali ni kukuza uchumi wa mkulima kufikia 2030.
Ameeleza kuwa wakulima wengi wa pamba bado wanatumia mbinu za zamani za kilimo, hali inayochangia kushuka kwa tija licha ya baadhi yao kuwa na mashamba makubwa.

Kutokana na changamoto hiyo, serikali imeendelea kuweka mikakati bora ya kuwahamasisha wakulima kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji.
Sanjari na hayo serikali imeongeza Jitihada Kukuza Uzalishaji wa Pamba huku ikiendelea kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kuinua uchumi wa wakulima pamoja na wananchi kwa ujumla,
Chongolo amesisitiza kuwa mkutano huo ni muhimu katika kujadili mikakati madhubuti ya kuendeleza sekta ya pamba, ambayo ni miongoni mwa mazao muhimu ya biashara nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameishukuru Bodi ya Pamba kwa kuweza kuchagua mkoa huo kufanya mkutano wao akiongeza kuwa "k**a mkoa tumejipanga kuhakikisha tunasapoti juhudi za Serikali katika Wizara ya Kilimo"

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Christopher Gachuma akichangia katika mkutano huo, amekiri kuwa changamoto ya bei ndogo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kutegemea soko la kimataifa. Wakati bei ya dunia inaposhuka, mkulima wa ndani anajikuta katika wakati mgumu.
Ili kukabiliana na hali hii, Gachuma ameshauri serikali na sekta binafsi kuwekeza zaidi katika viwanda vya ndani. “Tukichakata pamba yetu wenyewe, tutatengeneza soko la uhakika la ndani ambalo halitayumbishwa na bei za New York au Liverpool,” amesema Gachuma. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa zao la pamba
Naye mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amesema Bodi ya Pamba Tanzania(TCB) ilianzishwa kwa Sheria ya Pamba namba 2 ya mwaka 2001,utendaji wa bodi ya pamba unaongozwa na sheria hiyo sura 201 R.E 2023 na marekebisho ya mwaka 2025 pamoja na kanuni zake za mwaka 2011
Kwa upande wa wakulima ambao ni moja ya wadau muhimu walioshiriki mkutano huo maalum, wameiomba Serikali kuendelea kusogeza huduma za ugani karibu na mmoja wa wakulima waliowasilisha maoni yao Bw. Walwa Malimi kutoka Chato alieleza namna alivyaonza na kilimo cha kuvuna kilo 200 za Pamba kwa ekari; ambapo baada ya kuimarishwa kwa huduma za ugani amefanikiwa kuzalishaji wa kilo 2,000 kwa ekari moja.
Washiriki kwenye Mkutano ni pamoja na Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Wakulima; Wabunge na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la Pamba; Wanaushirika; Wafanyabiashara; na Wawekezaji.

Serikali itaendeleza jitihada za kuimarisha zao la Pamba kwa kutoa elimu na pembejeo kwa wakulima ili kuleta tija na bei yenye uhalisia kwa manufaa yao na wadau wa mnyororo mzima wa zao hilo.

Amesema Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba tarehe 16 Aprili 2026, Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga, amesema kuwa zao hilo ni la kimkakati kwa uchumi wa nchi na limelengwa kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani milioni 1 ifikapo mwaka 2030. Ameeleza kuwa Bodi ya Pamba imeratihu utoaji wa huduma za Ugani kupitia programu ya BBT-Ugani Pamba ambayo imewezesha kuongeza wigo wa uzalishaji wa zao hilo ambapo katika ~mwaka~ msimu huu wa ~mwaka~kilimo wa 2025/2026 tani laki 3 zinatarajiwa kuzalishwa.

Maoni mbalimbali yaliyotolewa yamejikita katika kuiomba Serikali kufanya tathmini za kina kuhusu bei ya Pamba ili imnufaishe mkulima; kuleta teknolojia za kısasa za kilimo zitakazoongeza uzalishaji wenye tija; ruzuku za viuadudu na pembejeo.

Kwa upande wa wakulima, wameiomba Serikali kuendelea kusogeza huduma za ugani karibu na wakulima na mmoja wao akieleza kuwa alianza na kilimo cha ekari moja wilayani Chato na kuvuna kilo 200 za Pamba; ambapo baada ya kuimarishwa kwa huduma za ugani amefikia uzalishaji wa kilo 2,000 kwenye hiyo ekari moja.

Washiriki kwenye Mkutano ni pamoja na Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Wakulima; Wabunge na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la Pamba; Wanaushirika; Wafanyabiashara; na Wawekezaji.

MKUTANO WADAU TASNIA YA PAMBA 2026Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Pamba Tanzania Ndg. Christopher Gachuma akizu...
19/04/2026

MKUTANO WADAU TASNIA YA PAMBA 2026

Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Pamba Tanzania Ndg. Christopher Gachuma akizungumza wakati wa mkutano maalum wa wadau wa tasnia ya pamba uliofanyika Aprili 16, 2026 jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Christopher Gachuma, amekiri kuwa changamoto ya bei ndogo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kutegemea soko la kimataifa. Wakati bei ya dunia inaposhuka, mkulima wa ndani anajikuta katika wakati mgumu.

Ili kukabiliana na hali hii, Gachuma ameshauri serikali na sekta binafsi kuwekeza zaidi katika viwanda vya ndani. “Tukichakata pamba yetu wenyewe, tutatengeneza soko la uhakika la ndani ambalo halitayumbishwa na bei za New York au Liverpool,” amesema Gachuma. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa zao la pamba

Mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa Mhe, Daniel Chongolo Waziri mwenye dhamana ya sekta ya kilimo nchini, ambapo wakati akifungua mkutano huo aliwahikishia wadau wa tasnia ya pamba kuwa Serikali itaendeleza jitihada za kuimarisha zao la Pamba kwa kutoa elimu na pembejeo kwa wakulima ili kuleta tija na bei yenye uhalisia kwa manufaa yao na wadau wa mnyororo mzima wa zao hilo

Kwa upande wa wakulima ambao ni moja ya wadau muhimu walioshiriki mkutano huo maalum, wameiomba Serikali kuendelea kusogeza huduma za ugani karibu na mmoja wa wakulima waliowasilisha maoni yao Bw. Walwa Malimi kutoka Chato alieleza namna alivyaonza na kilimo cha kuvuna kilo 200 za Pamba kwa ekari; ambapo baada ya kuimarishwa kwa huduma za ugani amefanikiwa kuzalishaji wa kilo 2,000 kwa ekari moja.

Washiriki kwenye Mkutano ni pamoja na Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Wakulima; Wabunge na Wakuu wa Mikoa inayolima zao la Pamba; Wanaushirika; Wafanyabiashara; na Wawekezaji.

Address

Nyamagana
Mwanza

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Cotton Board posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share