05/09/2025
DIAMOND NI KITABU CHA MKOSA FADHILA HAKIWEZI KUANDIKA SHUKRANI.
Na George Kabadi
Mafanikio ni sawa na Madaraka, Madaraka yanalevya na Mafanikio yanalevya ni vileo ambavyo ukiruhusu vikuongoze badala ya kuviongoza unaweza kuua mke, watoto na wazazi wako ili kuimarisha himaya yako.
Mungu humwinua mtu kupitia watu na humbariki mtu kupitia watu, haiwezekani kuwa binadamu ukawa kiongozi wa mawe na haiwezekani kuwa mwanamuziki mwenye ndoto za kuwaimbia ng'ombe, na katika ndoto zako ukatarajia kupokea mafanikio ya ng'ombe kuja kwenye SHOW zako kwa kulipa viingilio na kupakua nyimbo zako mtandaoni; HAIWEZEKANI! Mtu kufanikiwa pasipo na watu.
Kuna wanaofanikiwa na wanafanikiwa kurudisha fadhila kwa jamii zao kwa sababu wanaelewa mchango wa anayekukatisha tamaa na anayekutia moyo ni muhimu kuliko mchango wa aliyekaa kimya katika harakati zako na kuna wanaofanikiwa na wanafanikiwa kulewa na mafanikio, hawa hata Mungu aliyewapa mafanikio kupitia watu humkosoa, Mtu alikuwa Mwanaume atataka kuwa mwanamke; NDIYO! atafanya yale yanayompendeza yeye na si yaliyowapendeza watu nyakati za kuinuliwa kwake.
DAIMODI amekosa fadhila, anasahau anaowatukana na kuwadhihaki baada ya kulewa na mafanikio, ndiyo waliyokuwa wanahudhuria SHOW zake, wakati hajui kuoga vizuri, ndiyo waliyokuwa wanauza vitumbua na kubeba zenge ili wapate bando la kuingia mtandaoni na kupakua nyimbo zake. Dunia haijawahi kumsaliti mtu, bali mtu husalitiwa na mtu.
Kioo cha Jamii ya Watu, Kimegeuka kuwa Toilet paper ya Choo cha Stendi ya wanasiasa.
George Kabadi
Nakala.