13/05/2026
Tofauti kati ya maskini na tajiri sio saa wanazopewa na Mungu, bali ni jinsi wanavyozitumia saa hizo. Maskini anauza muda wake kupata pesa, tajiri ananunua muda wa wengine ili apate muda zaidi wa kufikiri. Ukiona unatumia muda mwingi kulala, kubishana mitandaoni, au kufuatilia maisha ya watu, ujue bado hujajua thamani ya sekunde zako. Muda ukishapita haurudi, na kila dakika unayopoteza ni fursa ya kujiimarisha inayotokomea. Leo, piga hesabu: masaa yako 24 unayatumia kuzalisha nini?