01/06/2026
Habari yako , nimeona umepost stori ya Binti mmoja hapo anasema toka atembee na baba mmoja aliye kuwa anampa pesa sana Hedhi yake inakuja Mfululizo bila mpangilio.
Naomba ukipata muda upost hiki kisa changu, baada ya kuona hiyo stori nimekumbuka kitu kimoja, Mimi nimewahi kwenda Kwa Mganga kutafuta utajiri ila masharti mengi niliyo kuwa napewa nilishindwa kwakweli japo mengine yali onekana ni mepesi ila Roho yangu ilikuwa ngumu Kukubaliana.
Niliwahi kwenda Kwa huyo Mganga akanipa sharti jepesi akaniambia nitakuwa Natembea na mabinti watatu Kila wiki, na hao mabinti inatakiwa wawe chini ya miaka 20, nikamwuliza Sasa nitakuwa nawajuaje? Akaniambia kwenye pesa hakishindikani kitu, akaniambia atanipa dawa ya kutambua umri wao na Wala siyo kazi ngumu.
Nikamwuliza, Sasa nikisha tembea nao itakuwaje? Akaniambia ndo pesa hizo, Sasa shida ilikuja nilipo mwuliza k**a hao mabinti hawapati madhara? Ndo akaniambia hawapati madhara ila maisha yao yote hawato ishi Kwa amani, Yani hawawezi tena kupata mahusiano ya kueleweka, hata akipata mwanaume aliye siriaz baada ya muda huyo mwanaume lazima abadilike ghafla, Kwa kifupi maisha Yao yote ni kuteseka, na hata akiolewa lazima aachike, na hakuna atakacho fanya akafanikiwa kwenye maisha yake yote.
Mganga aliniambia, hayo mateso kwenye maisha Yao ndo pesa zinavyo miminika kwako, hawapati madhara yoyote zaidi ya kukosa amani kwenye maisha yao, kuchukiwa n,k.
Nilitafakari hayo mambo nikaona hapana siyo sawa, Sasa nilivyo ona hiyo post nikakumbuka hiki kitu ni k**a vina endana na hili tukio Langu.
Na kitu Cha mwisho Cha kuwaambia watu, wajiulize kwanini matajiri wengi Wana penda mabinti wadogo? Hiyo ni Siri kubwa sana ukipenda kukaa na matajiri ndo utajua Siri hiyo. member