Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali The Vision of Mbarali District Council is to be: "capable and Efficient Local Government Authority to attain Sustainable Social and Economic Development

Heri ya Mwaka Mpya
31/12/2025

Heri ya Mwaka Mpya

Mimi Brig Jen Maulid Hassan Surumbu, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, naungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...
31/12/2025

Mimi Brig Jen Maulid Hassan Surumbu, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, naungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na viongozi wenzangu, kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya, wananchi wa Mbarali na wananchi wote wa Tanzania.

Tanzania yetu ni moja; tofauti ni sehemu ya demokrasia, na umoja wetu ndio msingi wa maendeleo endelevu.

Tuukaribishe Mwaka 2026 kwa amani, mshik**ano na imani thabiti kwamba kesho itakuwa bora kuliko jana.






25/12/2025

SHERIA YA NDOA INAVYOTESA MIMBA ZA UTOTONI, DOCTOR RAY SALANDI AONYA WAZAZI NA WALEZI

25/12/2025
Mkuu wa wilaya ya Mbarali Mhe. Brig. Jen. Maulid Hassan Surumbu anawatakia Heri ya Sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya Wa...
24/12/2025

Mkuu wa wilaya ya Mbarali Mhe. Brig. Jen. Maulid Hassan Surumbu anawatakia Heri ya Sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya Watumishi wote, viongozi wote, Wananchi wote wa Wilaya ya Mbarali na Watanzania kwa jumla, Tusheherekee kwa amani na utulivu.

MBUNGE JIMBO LA MBARALI AFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mh...
19/12/2025

MBUNGE JIMBO LA MBARALI AFANYA KIKAO KAZI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo amefanya Kikao kazi na watumishi wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kuwataka wafanye kazi kwa uweredi na kuwajali wananchi .

Kikao hicho kilichofanyika Leo kwenye Ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kuudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Raymond Mweli na Makam mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mheshimiwa Chuki Jeremia Mbwanjine na watumishi wote wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Akizungumza na watumishi hao Mheshimiwa Ndingo amewasisitiza watumishi hao kuhakikisha wanatembelea maeneo yenye Miradi ili kuhakikisha Miradi inakamilika kwa Wakati uliopangwa ili kuwapunguzia usumbufu Wananchi wa Wilaya ya Mbarali

"sisi k**a Viongozi tunawategemea Sana ninyi katika kuzimaliza changamoto za Wananchi wetu hivyo Kila mmoja wetu analojukumu la kutimiza wajibu wake na ni jukumu la Kila mtu kwenye Idara yake kufika site za Miradi ili kusimamia utekelezaji wake uwe wa Ubora unaohitajika ,pia Tuhakikishe tunatatua migogoro mbalimbali inayojitokeza . Pia katika Utekelezaji wa Miradi hii Tuhakikishe tunawashirikisha Viongozi ngazi ya Kata Vijiji na hata Vitongoji pia wananchi ili wajue jinsi serikali inavyo Fanya kazi kuhakikisha wanapata huduma zote za kijamii Yote haya yatawezekana k**a tutashirikiana kwa karibu baina yetu "

Sanjari na hilo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Raymond Mweli Amesema k**a Halmashauri wamekusudia kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na tutahakikisha tunakusanya mapato kwa haki na kusimamia Miradi yote ya Maendeleo kuhakikisha inakamilika kwa wakati

"Sisi k**a watumishi wa serikali jukumu letu namba Moja ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha tunatatua Kero zao zote hivyo k**a Mkurugenzi sita vumilia vitendo vyovyote vya uzembe katika kusimamia Miradi ya Maendeleo na Ndio Maana Kila Miradi kwa sasa tumempa project manager wa kuusimamia na sitashindwa kumchukulia hatua mtumishi yoyote anayeipaka matope Halmashauri kwa kwenda kudai asilimia 10 kwa mafundi au wazabuni maana hiyo hana jema kwa serikali lakini ili Miradi hii ikamilike tunahitaji Fedha na Fedha hizo zinatokana na Kodi na ushuru hivyo tukusanye Kodi pasipo kumuonea mtu yoyote na tusiruhusu mianya ya upotevu wa mapato"

Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wamemshukuru na kumpongeza mheshimiwa Ndigo kwa kuja kuongea nao na kumuomba kuwasaidia kupata fursa zitakazo wasaidia wao kuboresha maisha yao

MAAFISA MIFUGO WAKABIDHIWA PIKIPIKI KWA AJILI YA UTOAJI WA CHANJO MBARALI Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wi...
18/12/2025

MAAFISA MIFUGO WAKABIDHIWA PIKIPIKI KWA AJILI YA UTOAJI WA CHANJO MBARALI

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bi Glory Komba amekebidhi Pikipiki kwa Maafisa Mifugo ngazi ya Kata ili kuisaidia kuharakisha zoezi la utoaji chanjo kwa Mifugo

Akizungumza wakati wa Ugawaji wa Pikipiki hizo Bi Komba amesisiitiza matumizi sahihi ya Pikipiki hizo ili kuinua sekta ya Mifugo na sio kutumia Pikipiki hizo kwa matumizi binafsi k**a boda boda

"K**a mnavyojua Wilaya ya Mbarali Ina Mifugo mingi Sana hivyo Serikali inapotoa Vitendea kazi k**a Hivi ujue inataka ufanisi uongezeke ili wafugaji wafikiwe kwa wakati na wapate huduma stahiki kutoka kwenu wataalam wetu , Ni matumaini yangu Vitendea kazi hivi vitatumika kwa makusudi tarajiwa tu na si vinginevyo pia Tuhakikishe tunavitunza Vitendea kazi hivi ili vitumike kwa muda mrefu "

Kwa upande wake Eng. Karoli Lihala Kaimu mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali amewataka watumishi hao kuzingatia matunzo ya Pikipiki hizo ili ziwafae kwa muda mrefu

"Sasa ninatarajia Mtawafikia wananchi kwa urahisi Sana hivyo kwa kutumia Pikipiki hizi nendeni mkahakikishe Kila Mfugo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali unapata chanjo ili kuondoa magonjwa nyemerezi kwa Mifugo yetu"

Maafisa Mifugo Kata walio kabidhiwa Pikipiki hizo ni kutoka Kata za Luhanga , Rujewa na Ipwani

AFISA MIPANGO HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI AHIMIZA KASI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NA KUONGEZA NGUVU KWENYE ...
17/12/2025

AFISA MIPANGO HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI AHIMIZA KASI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NA KUONGEZA NGUVU KWENYE UKUSANYAJI WA MAPATO

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Venance Sarifu ameongoza Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata ya Madibira.

Miradi iliyotembelewa siku ya Leo ni pamoja na Jengo la mionzi yaani X-ray na Ultrasound kwenye kituo cha Afya Madibira, ujenzi wa Bweni la wasichana Shule ya sekondari Miyombweni, Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Nyakadete na Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Madibira

Aidha Ndugu Venance amefanya Kikao kazi na wataalam ngazi ya Kata ya Madibira kuhakikisha wanasimamia Miradi ya Maendeleo ipasavyo na kwa ukaribu pia amewataka kuhakikisha wanaongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa mapato ili kuongezea Mapato serikali

"Sisi k**a watumishi wa serikali tunalo jukumu la kuhakikisha tunakusanya mapato ili kuwezesha serikali kukamilisha Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa mapato ya ndani kwani mapato tunayokusanya Ndio Maendeleo yetu "

Katika Ziara hiyo Ndugu Venance aliambatana na Afisa Elimu Msingi, Afisa Elimu sekondari na Mhandisi wa Wilaya

Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Kesho kwenye Kata za Igava na Ipwani

TIMU YA WATAALAMU MBARALI WAHIMIZA KASI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA MBARALI Timu ya Wataalamu kutoka Ha...
16/12/2025

TIMU YA WATAALAMU MBARALI WAHIMIZA KASI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA MBARALI

Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wakiongozwa na Afisa Mipango wa Wilaya ya Mbarali Ndugu Venance Sarifu imewataka wasimamizi wa Miradi kuhakikisha Miradi inakamilika kabla ya January

Hayo yameelezwa wakati timu hiyo ilipopita kufanya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Akizungumza wakati wa Ukaguzi huo Ndugu Venance amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanaongeza Kasi katika Utekelezaji wa Miradi hiyo k**a serikali inavyoelekeza

"Ni jukumu letu k**a wasimamizi wa Miradi kuhakikisha vifaa vinafika site kwa wakati na mafundi wanakuwepo site ili kuharakisha Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo inakamilika ili kuwapunguzia usumbufu Wananchi wa kupata huduma za kijamii k**a Shule na zahanati "

Katika Ziara hiyo timu imefanikiwa kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Jamuhuri Iliyopo Kijiji cha Igarako, Shule ya Msingi Ilongo , zahanati ya Kijiji cha Nsonyanga, Ujenzi wa Maabara Shule ya sekondari Chamlindima, Ujenzi wa Maabara Shule ya sekondari Mengere , Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Igurusi,Ujenzi wa Madarasa ya awali na Msingi Shule ya Msingi Uturo, Ujenzi wa Bweni Shule ya sekondari ya wasichana Uturo na Ujenzi wa Bweni jipya kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi igomelo

Katika Ziara hiyo Ndugu Venance aliambatana na Afisa Elimu sekondari Wilaya na Mhandisi wa Wilaya

Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea siku ya Kesho kwa kutembelea Miradi Iliyopo Kata za Madibira, Miyombweni na Igava

DAS SICHALWE AWATAKA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI KUBEBA SURA YA SERIKALI KWENYE UTEN...
16/12/2025

DAS SICHALWE AWATAKA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI KUBEBA SURA YA SERIKALI KWENYE UTENDAJI KAZI

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Frank Sichalwe amewataka watendaji wa Kata na vijiji pamoja na Watumishi wote katika ngazi za vijiji na Kata kuhakikisha wanafanya kazi vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.

Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha Watendaji Kata wote wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Sichalwe amesema watendaji wote wa serikali ni picha halisi ya Serikali kwani utendaji wa kila Mtumishi, utoaji wa huduma ndio unabeba muonekano wa Serikali pamoja na Mheshimiwa Raisi,

"Sisi ni picha ya Serikali, ni picha ya Mheshimiwa Rais, ni picha ya Chama cha Mapinduzi, tusiitukanishe Serikali. Sura ya Serikali ni wewe unavyotoa huduma" Amesema Katibu Tawala Sichalwe.

Aidha Katibu Tawala Sichalwe amewataka watendaji ambao ni wabovu wawajibishwe haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha hakuna mzaha katika utendaji kazi na utekekelezaji wa majukumu ya Serikali. Hata hivyo, ameagiza Watendaji Kata kuiitisha vikao vya haraka kwa Watumishi waliopo chini yao ikiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kiutendaji hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Raymond Mweli amesema katika utendaji kazi kumekuwa na baadhi wa Watendaji hawana umakini katika suala la ukusanyaji wa mapato na ndio wamekuwa kikwazo katika ukusanyaji wa mapato.

"Lack of seriousness (Kukosa umakini) kwa Watendaji wengi ndio unatuangusha" Amesema Ndugu Raymond huku akiendelea kusisitiza kuwa hata sita kuchukua hatua kwa Watendaji ambao wataonesha kukwamisha Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Kikao hicho kimefanyika leo Disemba 16, 2025 kikiwakutanisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Wakuu wa Idara pamoja na Watendaji wa Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

CHANGAMOTO YA UMEME MDOGO MBARALI SASA BASI Wamiliki wa viwanda na mashine za kukoboa mpunga kutoka maeneo ya Mpakani , ...
16/12/2025

CHANGAMOTO YA UMEME MDOGO MBARALI SASA BASI

Wamiliki wa viwanda na mashine za kukoboa mpunga kutoka maeneo ya Mpakani , Ubaruku,Imalilo songwe na Madibira wamelalamikia voltage ndogo ya umeme inayopatikana Wilaya ya Mbarali na kukwamisha uzalishaji na kuwatia hasara wafanyabiashara hao

Hayo yameelezwa kwenye Kikao cha Baraza la biashara Wilaya ya Mbarali likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mheshimiwa Brigedia Jenerali Maulid Hassan Surumbu ambaye ni mwenyekiti wa Baraza hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndugu Raymond Mweli ambaye ni Katibu wa Baraza hilo linalohisisha wafanyabiashara kutoka Sekta binafsi na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hii Mheshimiwa Surumbu amewaelekeza shirika la umeme Tanesco Wilaya ya Mbarali kulifanyia kazi hilo tatizo ili kuwaepushia usumbufu wafanyabiashara hao "Ninaagiza shirika la umeme Tanesco Mbarali kuhakikisha mnapambana kutatua changamoto hii kwani hawa wamiliki wa viwanda hivi ndio walipa Kodi wetu hivyo ni muhimu kuwasikiliza na kuwatatulia shida yao"

Aidha mwakilishi wa meneja wa Tanesco Wilaya ya Mbarali Daudi Luzina ametolea ufafanuzi changamoto hiyo na kueleza jitihada alizochukua kuimaliza tatizo hilo

"Tayari tumeanza kuvuta umeme kutoka Halmashauri ya Wilaya ya wanging'ombe ili kuongeza nguvu kwenye laini yetu hii ili kuendana na matumizi yaliyopo kwenye Wilaya yetu "

Address

Rujewa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali:

Share