Kutoka Kisiwandui

Kutoka Kisiwandui Ukurasa MAALUM wa MATUKIO na SHUGHULI za MAENDELEO Zinazofanywa na CCM na Serikali. (SMT/SMZ)
(1)

26/05/2026
Mbeto: Rais  Mwinyi agoma kuvunja Katiba ili abaki Madarakani Zanzibar Chama Cha Mapinduzi kimepongeza  uamuzi wa Rais w...
24/05/2026

Mbeto: Rais Mwinyi agoma kuvunja Katiba ili abaki Madarakani Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimepongeza uamuzi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Rais Dk Hussein Ali Mwimyi kwa kushinda majaribu ya wapambe walioanza kumshinikiza avunje katiba na kuongeza muda wa kubaki Madarakani Zanzibar.

CCM kimesema ni fedheha kwa wapambe na mashabiki walioanza kumshawishi kiongozi huyo abaki madarakani kinyume na Katiba ya CCM na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, aliyesema huo ndio uamuzi na msimamo wa CCM.

Mbeto alisema kwa mujibu wa Mila na Utamaduni wa CCM , na kwa matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na katiba ya CCM ,Rais atakaa Madarakani vipindi viwili vya Miaka kumi na hatawania tena nafasi hiyo.

Alisema matamshi yaliotamkwa na baadhi ya wapambe kwa utashi wao binafsi, ulikuwa na dhamira batili, kwani hakuna Rais kupitia CCM anayeweza kupata nafasi ya kuongeza muda wa kubaki madarakani kinyume na taratibu.

"Hata iweje kwa Rais aliye Madarakani akitokea ameleta maajabu ya kiutendaji katika kusimamia maendeleo, muda wake kikatiba utabaki kuwa ule ule wa miaka kumi madarakani .Kila Rais akimaliza miaka hiyo atawapisha wengine. "Alisema Mbeto.

Aidha ,Katibu huyo Mwenezi aliliita tangazo la Rais Dk Mwinyi kukataa kubaki ikulu ifikapo mwaka 2030 , hana fikra wala mpango wa kuongeza muda ili abaki madarakani ni aibu kwa walioanza kumshabikia.

"Kiongozi yeyote muungwana huheshimu Katiba aidha ya chama na katiba ya nchi. Kuvunja ahadi na miadi au kufanya kinyume chake hiyo ni dalili ya kiongozi huyo kukosa utu na ustaarabu" Alisisitiza.

Mbeto alisema Tanzania hususan ndani ya CCM, kuna wanachama wengi wenye uwezo wa kubeba dhamana ya Urais na kuitumikia nchi kwa uzalendo,uadilifu na uaminifu, hivyo nafasi ya kiongozi mmoja kubaki madarakani milele haipo.

"Nafasi zaidi ya miaka mitano ilitolewa kwa Waasisi Wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume .Baada ya wao hatatokea yeyote wa kuongeza muda zaidi ya kuongoza aidha kwa Zanzibar

24/05/2026
23/05/2026

RAIS DKT. MWINYI ASITISHA MJADALA WA KUONGEZA MUDA WA URAIS,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hana nia ya kuongeza muda wa Urais zaidi ya muda uliowekwa kikatiba na kuagiza kusitishwa mara moja kwa mijadala kuhusu suala hilo.

Dkt. Mwinyi amesema kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo Baraza la Wawakilishi, kumekuwa na mijadala na mapendekezo ya kuongeza muda wa Urais badala ya miaka 10 iliyowekwa na Katiba ya Zanzibar, lakini amesisitiza kuwa hana dhamira hiyo na kwamba mjadala huo hauna tija kwa nchi kwa sasa.

Amesema viongozi wameapa kuilinda Katiba ya Nchi na kuwataka wananchi na viongozi kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa maendeleo ya taifa. Ameeleza kuwa kipindi kilichobaki cha uongozi wake kitakuwa cha utekelezaji mkubwa na wa kasi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 23 Mei 2026 alipofungua Jukwaa la Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma lililofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali haitakuwa tayari kuendelea kubeba mashirika ya umma yanayoshindwa kujiendesha na kuendelea kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

Amesema bado yapo mashirika ya umma yanayolipwa mishahara na kuendeshwa kwa fedha za Serikali jambo alilosema limepitwa na wakati, huku akiitaka taasisi hizo kujipanga na kujiendesha kwa tija na faida.

Halikadhalika Dkt. Mwinyi amesema Serikali itatoa muda kwa mashirika hayo kufanya mageuzi ya kiutendaji na yale yatakayoshindwa kujiendesha Serikali haitakuwa tayari kuendelea nayo.

Vilevile Dkt. Mwinyi amesisitiza kuendelea kwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050 pamoja na miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi na uimarishaji wa bandari, viwanja vya ndege, viwanja vya michezo na miundombinu ya barabara ili kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi wa kisasa na endelevu.

RAIS DKT. MWINYI ASITISHA MJADALA WA KUONGEZA MUDA WA URAIS,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. ...

HONGERA
22/05/2026

HONGERA

Address

Stone Town

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kutoka Kisiwandui posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share