26/08/2025
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeomba kukutana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dharura ili kimuwasilishie maoni ya Wadau mbalimbali juu ya changamoto ambazo zinapaswa kutatuliwa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ili kulifanya Taifa kuingia kwenye uchaguzi likiwa na amani na kurejesha imani ya Wananchi kwenye Mamlaka za uchaguzi.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo August 26, 2025 Jijini Dar es salaam, Rais wa TLS Boniface Mwabukusi amesema “TLS imewasiliana na Ofisi ya Rais ili kuwasilisha maazimio ya Wadau, tukipata nafasi ya kukutana na Rais, tutatoa ushauri wa hatua za haraka za kuchukuliwa ili kurudisha imani ya Wananchi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa shirikishi, shindani na wenye uhalali wa kisiasa”
“Hadi hivi sasa hatujapata majibu kutoka Ofisi ya Rais ila kuna umuhimu wa TLS kuwasilisha maoni hayo, tunayo nafasi ya kusimama imara k**a Taifa kwa kusikilizana na kuelewana kwenye masuala muhimu ya kitaifa k**a suala la uchaguzi mkuu”