Ikulu habari Zanzibar

Ikulu habari Zanzibar Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Jummah Mubarak.
21/08/2026

Jummah Mubarak.

19/08/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza leo, tarehe 19 Agosti 2026, wakati alipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyeambatana na Mkurugenzi wa Divisheni ya Benki hiyo anayesimamia Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Firas Raad, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
19/08/2026

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

19/08/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza alipokutana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi aliyefika Ikulu Zanzibar leo tarehe 19 Agosti 2026 ,kujitambulisha rasmi kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.

RAIS DKT. MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA DUNIARais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh...
19/08/2026

RAIS DKT. MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA DUNIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika kuimarisha sekta za elimu, afya, nishati na miundombinu, huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wananchi wanufaike kwa wakati.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 19 Agosti 2026, alipokutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika Mashariki na Kusini, Dkt. Ndiamé Diop, aliyeambatana na Mkurugenzi wa Divisheni ya Benki hiyo anayesimamia Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe, Bw. Firas Raad, katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar. Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndg. Khamis Abdulla Said, pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali na Benki ya Dunia.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha uwekezaji katika sekta za kipaumbele, kutoa fursa kwa Sekta Binafsi na kuimarisha mafunzo ya amali ili vijana wapate ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.

Kwa upande wake, Dkt. Ndiamé Diop amesema Benki ya Dunia imeridhishwa na kasi ya maendeleo Zanzibar na itaendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo yenye vipaumbele vya pamoja.

RAIS DKT. MWINYI: NINA IMANI NA UWEZO WA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBARRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Ma...
19/08/2026

RAIS DKT. MWINYI: NINA IMANI NA UWEZO WA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, kwa uteuzi wake na kumtaka kutekeleza majukumu yake kwa bidii, huku akiahidi kumpatia ushirikiano zaidi.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 19 Agosti 2026, alipokutana na Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, aliyefika Ikulu Zanzibar kujitambulisha rasmi kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, pamoja na kupokea maelekezo kuhusu utekelezaji wa majukumu yake mapya.

Amesema ana imani na uwezo wake kutokana na uzoefu na utendaji aliouonesha alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, huku akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na viongozi na watendaji wa Chama katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ndg. Abdi Mahmoud Abdi amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushauri na maelekezo aliyompatia, na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na viongozi na watendaji wenzake katika kutekeleza majukumu ya Chama.

18/08/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza leo, 18 Agosti 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa AFCON pamoja na Bandari ya Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.

RAIS DKT. MWINYI: UWANJA WA AFCON FUMBA KUWA CHACHU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZANZIBARRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraz...
18/08/2026

RAIS DKT. MWINYI: UWANJA WA AFCON FUMBA KUWA CHACHU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Uwanja wa AFCON unaojengwa Fumba utakuwa uwanja wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa na chachu ya kufungua fursa mbalimbali kwa wananchi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 18 Agosti 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa AFCON pamoja na Bandari ya Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kunufaika na fursa za biashara, huduma na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazotokana na ongezeko la wageni, hususan wakati wa Michuano ya AFCON 2027.

Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuhakikisha miundombinu inayozunguka uwanja huo inajengwa kwa ubora na viwango vinavyokubalika kimataifa, ili kuongeza thamani ya eneo hilo na kuleta tija kwa Zanzibar kwa muda mrefu.

Kwa sasa, ujenzi wa Uwanja wa AFCON umefikia takribani asilimia 80, huku miundombinu mbalimbali ikiendelea kujengwa, ikiwemo barabara ya kisasa itakayoboresha usafiri na kuongeza haiba ya eneo hilo.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali inaendelea kujenga viwanja vya michezo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kupata fursa za kushiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Ameipongeza Kampuni ya Orkun kwa utekelezaji wa ujenzi wa uwanja huo kwa kuzingatia ubora na hadhi ya kimataifa, pamoja na kuweka miundombinu inayouwezesha kuhudumia shughuli mbalimbali za michezo na kijamii.

Uwanja wa AFCON Fumba utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 36,500, pamoja na viwanja viwili vya nje vyenye uwezo wa kuchukua watazamaji 5,000 kila kimoja.

Uwanja huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba 2026, ikiwa ni sehemu muhimu ya maandalizi ya Zanzibar kuelekea AFCON 2027.

17/08/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy, aliyefika Ikulu Zanzibar kuaga na kupokea maelekezo kabla ya kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Malaysia.

RAIS DKT. MWINYI AHIMIZA KUIMARISHWA KWA DIPLOMASIA YA UCHUMI NA MALAYSIARais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Map...
17/08/2026

RAIS DKT. MWINYI AHIMIZA KUIMARISHWA KWA DIPLOMASIA YA UCHUMI NA MALAYSIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemtaka Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy, kutumia nafasi yake kuimarisha diplomasia ya uchumi, hususan katika kuvutia uwekezaji, kukuza biashara na kuongeza watalii kutoka Malaysia wanaotembelea Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 17 Agosti 2026, alipokutana na Balozi Mkeremy, aliyefika Ikulu Zanzibar kuaga na kupokea maelekezo kabla ya kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Malaysia.

Amesisitiza umuhimu wa kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar katika utalii, hoteli na makaazi, uvuvi, mafuta na gesi pamoja na maeneo mengine ya Uchumi wa Buluu.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemtaka Balozi Mkeremy kuimarisha ushirikiano wa Zanzibar na Malaysia katika elimu, ikiwemo kuongeza fursa za ufadhili wa masomo na ushirikiano baina ya vyuo vikuu.

Naye Balozi Mkeremy amesema amepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi katika utekelezaji wa majukumu yake nchini Malaysia.

Address

Zanzibar
Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ikulu habari Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share