Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Government Organization, 229, Sumbawanga.

SUMBAWANGA YAJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA NA EL NIÑO.Katika kuhakikisha jamii na taasisi mbalimbali zinakuwa ta...
04/09/2026

SUMBAWANGA YAJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA NA EL NIÑO.

Katika kuhakikisha jamii na taasisi mbalimbali zinakuwa tayari kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazozidi wastani pamoja na tishio la El Niño, Kamati ya Usimamizi wa Maafa Wilaya ya Sumbawanga imefanya kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya maandalizi kabla na wakati wa msimu wa mvua.

Kikao hicho kilichofanyika Septemba 3, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nyakia Ally Chirukile.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Chirukile amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua za mapema na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na hatari zinazoweza kujitokeza, ili kupunguza madhara na maafa yanayoweza kusababishwa na mvua zinazozidi wastani pamoja na El Niño.

Aidha, Mhe. Chirukile amesisitiza umuhimu wa mamlaka husika kuwafikia wafugaji na kutoa elimu kuhusu namna bora ya kudhibiti na kuhifadhi mifugo yao wakati wa maafa, pamoja na kufanya utambuzi na kubaini idadi ya mifugo iliyopo katika vijiji, hatua itakayosaidia kurahisisha uokoaji na utoaji wa msaada endapo maafa yatatokea.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Gabriel Masinga, amezitaka mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna bora ya kujikinga, kuchukua tahadhari na kuepuka maeneo hatarishi, ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa maafa.

Ameongeza kuwa, maandalizi ya mapema na ushirikiano kati ya Serikali, taasisi mbalimbali na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha Wilaya ya Sumbawanga inakuwa tayari kukabiliana na athari za mvua na majanga mengine yanayoweza kujitokeza.

SUMBAWANGA YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TUNDUMA, YAVUTIWA NA UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATOTUNDUMA. Mwenyekiti wa Halmashauri ...
01/09/2026

SUMBAWANGA YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TUNDUMA, YAVUTIWA NA UBUNIFU WA VYANZO VYA MAPATO

TUNDUMA.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Ephraim Konta, ameipongeza Halmashauri ya Mji Tunduma kwa ubunifu katika kubuni na kuendeleza vyanzo vya mapato ya ndani, pamoja na kutumia mapato hayo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mhe. Konta ameyasema hayo wakati wa ziara ya mafunzo iliyofanywa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Halmashauri ya Mji Tunduma, ikiwa na lengo la kujifunza na kupata uzoefu kuhusu namna ya kubuni vyanzo vya mapato, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutumia mapato hayo katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ugeni huo uliongozwa na Mhe. Ephraim Konta na kujumuisha Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Katika ziara hiyo, ugeni ulipokelewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Salum Kiyambi, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Mariam Chaurembo, ambao waliwasilisha namna Halmashauri hiyo ilivyoweka mikakati ya kuongeza mapato ya ndani na kuyatumia katika utekelezaji wa miradi yenye tija kwa wananchi.

Ugeni ulipata fursa ya kutembelea na kujionea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Tunduma, ikiwemo mradi wa upimaji wa viwanja katika eneo la Ostabei ya Chipaka.

Katika eneo hilo, ugeni ulijionea namna Halmashauri ilivyojipanga katika kuwekeza kwenye ardhi kwa ajili ya kuongeza thamani na hatimaye kuongeza mapato. Viwanja hivyo vinatarajiwa kuuzwa hivi karibuni na kuwa miongoni mwa vyanzo vitakavyosaidia kuongeza mapato ya Halmashauri.

Aidha, ugeni ulitembelea mradi wa ujenzi wa Soko la Machinga, unaotekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri. Mpaka sasa, Halmashauri ya Mji Tunduma imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 katika mradi huo, ambao ukikamilika unatarajiwa kugharimu takribani Shilingi bilioni 6 na kuhudumia wafanyabiashara zaidi ya 1,000.

Vilevile, ugeni ulitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa lenye vyuma 10 vya madarasa katika Shule ya Msingi makambini.Hata hivyo wametembelea mradi wa parking ya maroli chini ya Halmashauri ya Mji Tunduma.

31/08/2026

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA ATOA KAULI BAADA YA ZIARA YA KUJIFUNZA MBINU ZA UKUSANYAJI MAPATO NA UWEKEZAJI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Ephraim Konta, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Zimba, akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara ya siku ya kwanza jijini Mbeya.

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna Halmashauri ya Jiji la Mbeya inavyotekeleza mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, usimamizi wa vyanzo vya mapato, pamoja na kutambua na kutumia fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuongeza mapato na kuchochea maendeleo ya wananchi.

Ziara hiyo imehusisha Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, ambao wametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na kumalizia Halmashauri ya Mji wa Tunduma kwa lengo la kujifunza mbinu bora zinazoweza kuigwa na kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.





KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEOKamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wil...
26/08/2026

KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imefanya ziara ya siku mbili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri, kuanzia tarehe 25 hadi 26 Agosti 2026.

Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Idara ya Afya, Elimu ya Msingi na Sekondari, pamoja na miradi ya uwekezaji, kwa lengo la kujiridhisha na maendeleo ya utekelezaji wake, ubora wa kazi na matumizi sahihi ya fedha za miradi.

Baada ya kukamilika kwa ziara hiyo, Kamati ilifanya kikao cha majumuisho kilichoongozwa na Mheshimiwa Ephraim Konta, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Zimba.

Katika majumuisho hayo, Kamati imebainisha maeneo na miradi inayohitaji hatua za haraka ili kuhakikisha changamoto zilizobainika zinapatiwa ufumbuzi na miradi yote inakamilishwa kwa wakati, kwa kuzingatia viwango na thamani halisi ya fedha zilizotengwa.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Laela, mkandarasi mwenye dhamana ya utekelezaji wa mradi huo, Sumli, ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa, ili wananchi waweze kupata huduma bora na stendi hiyo itumike ipasavyo.

Kwa ujumla, ziara hiyo imekuwa muhimu katika kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kubaini changamoto zinazohitaji hatua za haraka. Kamati imesisitiza kwa wahusika wote kuhakikisha maelekezo yaliyotolewa katika majumuisho yanafanyiwa kazi kwa wakati, ili miradi ikamilike kwa ubora unaostahili na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

25/08/2026

Vibe la ushindi baada kumchapa vikali wanaume wa Dar City Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam moja kwa mtungi 😀😀😃😃

#

SHAMSI DADY, MBEYAWAZIRI SHIMEDO AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA SHIMISEMITA 2026Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawa...
23/08/2026

SHAMSI DADY, MBEYA

WAZIRI SHIMEDO AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA SHIMISEMITA 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, leo Agosti 23, 2026, amefungua rasmi Mashindano ya Shirika la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) katika viwanja vya Shule ya Sekondari Iyunga, Jijini Mbeya.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo, Prof. Shemdoe amesema Serikali inaona michezo ya watumishi kuwa sehemu muhimu ya uwekezaji katika rasilimali watu, huku ikichangia kujenga Taifa lenye afya, nidhamu na mshikamano.

Amesema michezo si burudani pekee, bali ni nyenzo muhimu katika kuboresha afya ya mwili na akili, kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na kazi na kuimarisha mahusiano pamoja na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa umma.

«“Michezo si burudani pekee, michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu na ni nyenzo muhimu katika kujenga Taifa lenye afya, nidhamu, mshikamano na tija,” amesema Prof. Shemdoe.»

Mashindano hayo yameanza rasmi leo Agosti 23, 2026 na yanatarajiwa kuhitimishwa Agosti 29, 2026, yakihusisha timu za wanamichezo kutoka Halmashauri 177 kati ya Halmashauri 184 za Tanzania Bara.

Mashindano hayo pia yanaweka msisitizo katika kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa Serikali za Mitaa, huku yakiwa sehemu ya maandalizi kuelekea AFCON 2027.

“TUPO TAYARI KWA AFCON 2027.”

# Mbeya MichezoYaWatumishi TupoTayariKwaAFCON2027 SumbawangaDistrict Rukwa #

20/08/2026

Mchezaji wa mpira wa wavu (volleyball) akizungumza mara baada ya ushindi dhidi vibonde Mkuranga District Council 😀😀😃 kwenye mashindano ya shimisemita mkoani mbeya .

Vipi Mnatuweza??

.

⚽ FULL TIME | SHIMISEMITA 2026 🏆📍 Mkoani MbeyaSUMBAWANGA DC 1️⃣ – 1️⃣ DODOMA CCMatokeo ya mwisho katika mchezo wa mpira ...
18/08/2026

⚽ FULL TIME | SHIMISEMITA 2026 🏆

📍 Mkoani Mbeya

SUMBAWANGA DC 1️⃣ – 1️⃣ DODOMA CC

Matokeo ya mwisho katika mchezo wa mpira wa miguu wa Mashindano ya SHIMISEMITA 2026. Timu zote zimeonesha ushindani mkubwa na kupambana hadi dakika ya mwisho. 💪⚽

🤝 Hongereni Sumbawanga DC kwa mapambano!

Mbeya UshindiWetuFursaYetu

18/08/2026

Address

229
Sumbawanga

Opening Hours

Monday 01:29 - 21:30
Tuesday 01:30 - 21:29
Wednesday 01:29 - 21:29
Thursday 01:30 - 21:30
Friday 01:30 - 21:30
Saturday 01:30 - 12:30
Sunday 01:29 - 13:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga:

Shortcuts

Share